- Austria vs Jordan FIFA Kombe la Dunia 2026 safari inaanza Juni 17, 2026 nchini Marekani
- Uwanja wa San Francisco Bay Areasaa 7:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki
- SportPesa Blog imekuletea uchambuzi wa timu, h2h, vikosi na takwimu muhimu kuelekea mchezo
Safari ya Austria vs Jordan FIFA Kombe la Dunia 2026 itaanza Juni 17, 2026 katika Kundi J. Mchezo huu utakapigwa kwenye Uwanja wa San Francisco Bay Area (Levi’s Stadium) uliopo Santa Clara, California, Marekani. Huku mabingwa watetezi Argentina na vigogo wa Afrika Algeria wakiwa pia kwenye kundi hilo, Austria na Jordan watautazama mchezo huu kama fursa adhimu ya kujikusanyia pointi muhimu.
Hii hapa ratiba ya mechi zote 104 FIFA Kombe la Dunia 2026: FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil | Mechi zote | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika | Je, Neymar Jr yuko tayari?
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Austria vs Jordan, angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Bashiri kwa uwajibikaji.

Austria vs Jordan FIFA Kombe la Dunia 2026 taarifa muhimu kuhusu timu

Utabiri wa mechi kali ya Kundi I upo hapa: France vs Senegal utabiri Kombe la Dunia 2026 | Kundi I
Kampeni ya Austria vs Jordan FIFA Kombe la Dunia 2026 inatarajiwa kuwa na mageuzi makubwa. Hii inatokana na mbinu za Ralf Rangnick anayekinoa kikosi cha Austria tangu 2022.Baada ya kuondolewa katika hatua ya 16 bora ya Euro 2024, Austria waliimarika na kushinda mechi 11 kati ya 18 zilizofuata. Matokeo hayo yameongeza matumaini kwa mashabiki wao kuwa timu hiyo inaweza kufanya vizuri katika Kombe la Dunia la mwaka huu.
Kwa upande wa Jordan, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki Kombe la Dunia na wengi wanatarajia safari yao kuishia katika hatua ya makundi. Hata hivyo, kocha Jamal Sellami anaamini timu yake inaweza kufanya makubwa zaidi ya matarajio ya wengi.Jordan walijizolea sifa katika hatua ya kufuzu kutokana na uimara wao wa kujilinda. Safu yao ya ulinzi ilikuwa nguzo kuu ya mafanikio yao, na watahitaji kuonyesha nidhamu hiyo kwa kiwango cha juu zaidi ikiwa wanataka kuhimili ushindani mkali wa kundi hili gumu.
Kwa kuwa Argentina wanaonekana kuwa vinara wa Kundi J na Algeria wakitajwa miongoni mwa timu zenye uwezo mkubwa, pambano hili kati ya Austria na Jordan linaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuamua nani atabaki na matumaini ya kusonga mbele. Kwa hiyo, pointi tatu katika mchezo huu zinaweza kuwa hazina kubwa kwa timu yoyote itakayofanikiwa kuibuka na ushindi.
Austria vs Jordan wapata pigo kuwakosa wachezaji muhimu
Kocha Ralf Rangnick amepata pigo kuelekea FIFA Kombe la Dunia baada ya kiungo mshambuliaji Christoph Baumgartner kuumia. Kukosekana kwake kunainyima Austria mmoja wa wachezaji wao muhimu zaidi katika ubunifu wa mashambulizi na kutengeneza nafasi za magoli. Licha ya pengo hilo, Austria bado wana kikosi chenye uzoefu na ubora mkubwa, wakiongozwa na nahodha David Alaba pamoja na mshambuliaji mkongwe Marko Arnautovic.
Kocha Jamal Sellami amekumbwa na pigo kubwa baada ya mshambuliaji tegemeo Yazan Al Naimat na chipukizi mahiri Ibrahim Sabra kukosa michuano hii kutokana na majeraha. Kutokuwepo kwao kunapunguza makali ya safu ya ushambuliaji ya Jordan, jambo litakalowalazimu wachezaji wengine kujitokeza na kubeba jukumu la kuisadia timu.
Kikosi kinachotarajiwa cha Austria (4-2-3-1)

Mafarao kazini FIFA Kombe la Dunia soma hapa: Ubelgiji vs Misri utabiri FIFA Kombe la Dunia 2026, taarifa kuhusu timu, muda wa mchezo Kundi G | SportPesa Blog
Kipa:Alexander Schlager
Mabeki:David Alaba,Philipp Lienhart, Kevin Danso na Konrad Laimer
Viungo wa kati: Nicolas Seiwald na Xaver Schlager
Viungo washambuliaji:Marcel Sabitzer, Patrick Wimmer na Romano Schmid
Mshambuliaji: Marko Arnautovic
Kikosi kinachotarajiwa cha Jordan (3-4-2-1)
Kipa:Yazeed Abulaila
Mabeki:Mohammad Abualnadi, Abdallah Nasib na Yazan Al-Arab
Viungo:Mohannad Abu Taha, Noor Al-Rawabdeh, Nizar Al-Rashdan na Ehsan Haddad
Viungo washambuliaji: Odeh Fakhoury na Mousa Al-Tamari
Mshambuliaji: Ali Olwan.
Hivi vikosi sio rasmi. Muda mfupi kabla ya mchezo husika vikosi vitatambulishwa.
Austria vs Jordan kuchezwa lini?
Austria vs Jordan inatarajiwa kuchezwa Juni 17, 2026
Austria vs Jordan kundi gani?
Austria vs Jordan ni timu kutoka Kundi J
Austria vs Jordan kuchezwa saa ngapi?
Austria vs Jordan ni Saa 7:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) / Saa 4:00 UTC (Sawa na saa 3:00 usiku kwa saa za Marekani, Juni 16).
Mechi 5 Zilizopita za Austria
| Tarehe | Mpinzani | Mashindano | Matokeo |
| 1 Juni 2026 | Tunisia | Mchezo wa kirafiki | Austria 1-0 Tunisia |
| 31 Machi 2026 | Korea Kusini | Mchezo wa kirafiki | Austria 1-1 Korea Kusini |
| 27 Machi 2026 | Ghana | Mchezo wa kirafiki | Austria 5-0 Ghana |
| 18 Novemba 2025 | Bosnia na Herzegovina | Kufuzu Kombe la Dunia | Austria 1-1 Bosnia na Herzegovina |
| 15 Novemba 2025 | Cyprus | Kufuzu Kombe la Dunia | Cyprus 0-2 Austria |
Muhtasari wa Austria
Ushindi: 3 Sare: 2 Kipigo: 0 Mabao ya kufunga: 10 Mabao ya kufungwa: 2
Mechi 5 Zilizopita za Jordan
| Tarehe | Mpinzani | Mashindano | Matokeo |
| 8 Juni 2026 | Colombia | Mchezo wa kirafiki | Jordan 0-2 Colombia |
| 31 Mei 2026 | Switzerland | Mchezo wa kirafiki | Jordan 1-4 Switzerland |
| 31 Machi 2026 | Nigeria | Mchezo wa kirafiki | Jordan 2-2 Nigeria |
| 27 Machi 2026 | Costa Rica | Mchezo wa kirafiki | Jordan 2-2 Costa Rica |
| 14 Novemba 2025 | Tunisia | Mchezo wa kirafiki | Tunisia 3-2 Jordan |
Muhtasari wa Jordan
Ushindi: 0 Sare: 2 Vipigo: 3 Mabao ya kufunga: 7 Mabao ya kufungwa: 13.
H2H
Austria vs Jordan rekodi zinaonyesha hazijawahi kukutana katika mchezo wa ushindani. Juni 17, 2026 utakuwa ni mchezo wao wa kwanza FIFA Kombe la Dunia.
Hitimisho
Austria vs Jordan FIFA Kombe la Dunia 2026 ni daraja kwa timu hizi kuelekea hatua kuwania kusonga hatua inayofuata. Jordan haijawa na mwendo mzuri katika mechi 5 zilizopita ikishindwa kupata ushindi.Austria imekuwa kwenye ubora ikipata ushindi katika mechi 3 zilizopita.

