FIFA Kombe la Dunia ---- ratiba ya BrazilFIFA Kombe la Dunia ---- ratiba ya Brazil
  • FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil, ni miongoni mwa ratiba ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa.
  • Timu ya Taifa ya Brazil ni miongoni mwa timu zenye mashabiki wengi Duniani kote, hii ni kutokana na vipaji na mafanikio makubwa ya kihistoria waliyonayo.
  • Brazil ni mabingwa wa kihistoria wa mashindano ya Kombe la Dunia, ambapo ndiyo timu pekee ambayo imeshinda ubingwa wa Dunia mara 5.
  • Kikosi cha Brazil kilicho chini ya kocha ‘Don’ Carlo Anceloti kinaundwa na mastaa wengi wakubwa wakiwemo; Neymar Jr, Vinicius Jr, Raphinha, Casemiro, Cunha n.k

Mechi za FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil, ni miongoni mwa ratiba inazosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Brazil ni miongoni mwa timu zenye mashabiki wengi Duniani kote, hii ni kutokana na vipaji na mafanikio makubwa ya kihistoria waliyonayo. Mabingwa hao wa kihistoria wa Kombe la Dunia, ndiyo timu pekee ambayo imeshinda ubingwa wa Dunia mara 5. Kikosi cha kocha ‘Don’ Carlo Anceloti kinaundwa na mastaa wengi wakubwa wakiwemo; Neymar Jr, Vinicius Jr, Raphinha, Casemiro, Cunha n.k nah ii hapa ni ratiba yao.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa.

Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator

Brazil wamepangwa Kundi gani?

Brazil imepangwa Kundi C pamoja na timu za mataifa ya Morocco, Haiti na Scotland. Hili ni miongoni mwa makundi yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, hasa dhidi ya Morocco ambayo wataanza nao mechi ya kwanza, ikumbukwe Morocco ilifanya vizuri katika Kombe la Dunia la mwaka 2022. Scotland ya kiungo wa zamani wa Manchester United, Scott McTominay nayo sio timu ya kubeza. Huu hapa chini ni msimamo wa Kundi hilo, kabla ya kuanza kwa mechi za hatua ya makundi.

Msimamo wa Kundi C

NafasiTimuMechiUshindiSareKufungwaMagoli ya KufungaMagoli ya KufungwaTofauti ya MagoliPointi
1Brazil00000000
2Morocco00000000
3Scotland00000000
4Haiti00000000

Kumbuka: Jedwali hili linaonyesha hali ya kundi kabla ya kuanza kwa mechi za Kombe la Dunia 2026. Timu zote zinaanza zikiwa na pointi sifuri, huku nafasi halisi zikitarajiwa kubadilika baada ya kila mchezo wa hatua ya makundi.

SOMA HII PIA: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil

Carlo Ancelotti
Carlo Ancelotti

13 Juni 2026

Brazil vs Morocco

Uwanja: MetLife Stadium, New Jersey

19 Juni 2026

Brazil vs Haiti

Uwanja: Lincoln Financial Field, Philadelphia

24 Juni 2026

Scotland vs Brazil

Uwanja: Hard Rock Stadium, Miami

Ratiba hiyo itakuwa muhimu katika kuamua kama Brazil itamaliza kileleni mwa Kundi C au la.

SOMA HII ZAIDI: Sheria mpya za mechi Kombe la Dunia 2026 zashtua! Nini kimebadilishwa?

Hiki hapa kikosi Kamili cha Brazil Kombe la Dunia 2026

Kikosi cha Brazil
Kikosi cha Brazil

Makipa

Alisson Becker

Bento

Hugo Souza

Mabeki

Marquinhos

Gabriel Magalhães

Bremer

Alex Sandro

Alexsandro Ribeiro

Danilo

Carlos Augusto

Vanderson

Wesley

Léo Ortiz

Beraldo

Viungo

Casemiro

Bruno Guimarães

Andreas Pereira

Ederson

Gerson

Washambuliaji

Neymar Jr

Vinicius Junior

Raphinha

Matheus Cunha

Gabriel Martinelli

Endrick

Luiz Henrique

Igor Thiago

Rayan

SOMA HII ZAIDI: Sheria 7 FIFA Kombe la Dunia 2026 | SportPesa Blog

Wachezaji wa Kuangaliwa

Vinicius Junior

Huyu ni nyota wa klabu ya Real Madrid, ambaye anatajwa kuwa ndiye tegemeo kubwa la safu ya ushambuliaji ya Brazil kutokana na kasi yake na uwezo wa kufunga magoli muhimu.

Neymar Jr

Neymar
Neymar

Licha ya umri kuongezeka na majeraha ya mara kwa mara, Kocha Carlo Ancelotti ameamua kumrejesha Neymar kwenye kikosi cha Brazil. Japo atamtegemea zaidi, Vinicius Junior kuwa nyota mkuu wa timu hiyo katika mashindano haya, lakini mchango wa Neymar Jr ni zaidi ya kiwango cha Uwanjani. Ikumbukwe, Neymar bado anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Brazil.

Raphinha

Aliingia kwenye rekodi ya 3 bora ya kinyang;anyiro cha mchezaji bora wa Dunia ‘Ballon d’or msimu jana. Mwaka huu pia ameiongoza Barcelona kutwaa ubingwa wa Hispania kwa msimu wa pili mfululizo. Anatajwa kuwa miongoni mwa washambuliaji hatari duniani kwa sasa.

Endrick

Endrick
Endrick

Amekuwa na nyakati nzuri nchini Ufaransa msuimu ulioisha alikokuwa akicheza kwa mkopo, kiasi wamiliki wake Real Madrid wametangaza kumrudisha. Amekuwa na nyakati nzuri katika mechi za maandailzi ya mashindano haya. Mshambuliaji huyo kijana anatarajiwa kuwa moja ya nyota zitakazong’ara zaidi katika Kombe la Dunia 2026.

SOMA HII PIA: Kombe la Dunia 2026 |Linaanza lini? Timu ngapi? Kuchezwa wapi? Kuna Sheria mpya? Ronaldo au Messi? Haya hapa majibu ya maswali yote muhimu unayojiuliza

Hitimisho

FIFA Kombe la Dunia ---- ratiba ya Brazil (-)
FIFA Kombe la Dunia 2026 ratiba ya Brazil – credit football 90 minutes

FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil, ndiyo inatajwa kuwa Habari kubwa kuelekea kuanza kwa mashindano hayo. Brazil inaingia Kombe la Dunia 2026 ikiwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kutwaa ubingwa, ikiwa na mchanganyiko wa uzoefu wa Neymar, Casemiro na Marquinhos pamoja na ubora wa Vinicius Junior, Raphinha na Endrick. Kikosi hiko cha Seleção, kina kila sababu ya kuota kurejesha kombe hilo nyumbani kwa mara ya sita katika historia yake hata hivyo ni ukweli kuwa haitakuwa rahisi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.