Ubelgiji vs Misri utabiri FIFA Kombe la Dunia 2026, taarifa kuhusu timu, muda wa mchezo Kundi G | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

June 13, 2026
Ubelgiji vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026Lukaku RomeluLukaku Romelu

Ni Ubelgiji vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026 zitashuka uwanjani kwa lengo la kusaka tiketi kufuzu hatua inayofuata. Huu ni mchezo wa Kundi G utakaopigwa jijini Seattle usiku wa Jumatatu, Juni 15, 2026.Timu hizi mbili zinapewa nafasi kubwa ya kufuzu kutoka kundi hilo.

SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026.Kwa mechi ya Ubelgiji vs Misri angalia odds, linganisha fomu ya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini. Beti kwa uwajibikaji.

Belgium
Ubelgiji vs Misri FIFA Kombe la Dunia.

Ubelgiji vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026 viwango vya timu

Wababe hawa wawili Ubelgiji vs Misri wanakutana kila mmoja akiwa kwenye ubora. Ubelgiji walipenya kwenye mashindano haya baada ya kumaliza hatua za kufuzu bila kupoteza mchezo wowote. Walishinda mechi tano na kutoka sare mara tatu, huku Norway pekee wakifunga mabao mengi zaidi yao katika hatua hizo. Kwa sasa, Ubelgiji wanashika nafasi ya tisa katika viwango vya ubora vya dunia na wanaingia kwenye mchezo wakiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi.

Kwa upande wa Misri, wanakabiliwa na mtihani mgumu dhidi ya kikosi chenye vipaji vingi. Licha ya kuwa moja ya mataifa makubwa ya soka barani Afrika, Mafarao hawajawahi kushinda hata mchezo mmoja katika historia yao ya Kombe la Dunia. Rekodi hii inawatesa jambo litakalowafanya wajitutumue kupata matokeo.

Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Misri kushiriki fainali za Kombe la Dunia, wakitumaini kufuta rekodi yao mbaya katika mashindano hayo. Ni Honduras pekee waliocheza mechi nyingi zaidi bila kupata ushindi kuliko Misri katika historia ya michuano hiyo. Ushindi kwa Misri inawezekana, ila itahitajika juhudi kubwa sana kuizuia Ubelgiji, timu ambayo imeonyesha ubora mkubwa kupitia kizazi chake kipya cha wachezaji wenye vipaji.

Utabiri unasemaje kuhusu mchezo huu?

Ubelgiji vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026
Mo Salah nyota wa timu ya taifa ya Misri. Source: ESPN

SOMA HII: Netherlands vs Japan FIFA Kombe la Dunia 2026 kundi F, utabiri, h2h | SportPesa Blog

Kwa mujibu wa rekodi inaonyesha kuwa Ubelgiji, huu ni ushiriki wao wa 15 katika Kombe la Dunia. Ni rekodi kubwa zaidi kwa taifa la Ulaya ambalo bado halijawahi kutwaa taji hilo la dunia. Kutokana na uzoefu huu kuna nafasi kubwa kupata ushindi dhidi ya Misri katika mchezo wa hatua ya makundi.

Hata hivyo, takwimu zinaendelea kuwapa matumaini Ubelgiji wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya mechi zao 15 za mwisho za hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia. Rekodi hiyo inaweza kuwapa morali kubwa kuelekea pambano hili muhimu la ufunguzi. Ushindi unaweza kuwa magoli 2-0 kwa Ubelgili, lakini haya ni maoni sio matokeo kamili.

Mechi ya Belgium vs Misri itaanza saa ngapi?

Mchezo kati ya Ubelgiji na Misri utapigwa saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (E.A.T) katika Uwanja wa Lumen Field, Seattle, ukiwa ni sehemu ya mechi za Kundi G za Kombe la Dunia 2026.

Habari za kikosi cha Ubelgiji

Ubelgiji vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026
Timu ya taifa ya Ubelgiji.

SOMA HII: FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil | Mechi zote | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika | Je, Neymar Jr yuko tayari?

Kiungo mkongwe Kevin De Bruyne anatarajiwa kucheza Kombe lake la Dunia la mwisho, na ataanza katika kikosi cha kwanza baada ya kufunga bao katika mchezo wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Tunisia.Viungo Youri Tielemans wa Aston Villa na Amadou Onana, wameonyesha ushirikiano mzuri katikati ya uwanja na wanatarajiwa kuendelea kupewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Katika eneo la ushambuliaji, Charles De Ketelaere huenda akaanzia benchi licha ya kufunga bao dhidi ya Tunisia katika mechi ya kirafiki. Mshambuliaji mkongwe na kinara wa mabao wa muda wote wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, ataiongoza safu ya ushambuliaji ya Red Devils.

Winga wa Manchester City, Jeremy Doku, alikuwa katika kiwango bora wakati wa mechi za kufuzu baada ya kufunga mabao manne. Nyota huyu anatarajiwa kuanza upande mmoja wa ushambuliaji huku Leandro Trossard akicheza upande wa pii.

Habari za kikosi cha Misri

Misri pia ina baadhi ya nyota wakongwe wanaotarajiwa kucheza Kombe lao la Dunia la mwisho, huku Mohamed Salah akiongoza orodha hiyo. Nyota huyo wa Liverpool atakuwa tegemeo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Mafarao wanapojaribu kufuzu kutoka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.Wachezaji Omar Marmoush na Trezeguet wote wapo fiti na wanatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza.

Sehemu kubwa ya kikosi cha Misri itabaki kama ilivyokuwa katika mchezo wao wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Brazil, huku kocha akiamini mchanganyiko huo unaweza kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Ubelgiji.Pambano hili linatarajiwa kuwa la kuvutia, likiwakutanisha nyota wakubwa kama Kevin De Bruyne, Romelu Lukaku na Mohamed Salah katika harakati za kuwania mwanzo mzuri wa Kombe la Dunia 2026.

Share this: