Achraf Hakimi aandika rekodi League 1: Hat-trick ya kihistoria, mabao 5, highlights

Hat-trick ya kihistoriaHat-trick ya kihistoriaHat-trick ya kihistoria

Achraf Hakimi aandika rekodi League 1: Hat-trick ya kihistoria, mabao 5, highlights

  • Achraf Hakimi nahodha wa kikosi cha PSG, ameandika rekodi ya aina yake kwenye vitabu vya Ligi Kuu Ufaransa League 1.
  • Katika mchezo vs La Havre iliyopigwa Oktoba 30, 2026 straika huyo alifanikiwa kuhusika katika mabao 5 akifunga 3 na kuasisti 2.
  • Hii inamfanya staa huyo kuwa mlinzi pekee aliyehusika kwenye mabao 5 katika mchezo mmoja wa ligi hiyo tangu 2006/07.
  • Makala hii inachambua kupitia picha mchezo kiwango cha Hakimi

Nahodha wa kikosi cha PSG, Achraf Hakimi ameandika historia ya kipekee katika Ligi Kuu Ufaransa, maarufu League 1. Hii ni baada ya kufanikiwa kufunga hat-trick yake ya kwanza katika soka la kulipwa. Hakimi pia ameandika historia ya kuwa mlinzi pekee aliyehusika kwenye mabao 5 katika mchezo mmoja wa ligi hiyo tangu 2006/07.

SOMA HII PIA: Hawa hapa wachezaji 5 wa kuchungwa AFCON 2025 Morocco

Hattrick ya kwanza kwenye maisha yake

Achraf Hakimi
Hakimi

Hatrick hii inakuwa ya kwanza kwa Hakimi katika maisha yake ya soka la ushindani. Hii ni rekodi ambaye inahusisha timu zote ambazo amewai kuchezea. Timu hizo ni Timu ya Taifa ya Morocco, Real Madrid, Borussia Dortmund na Inter Milan. Hakimi alifunga mabao hayo katika dakika za 28, 55 na 69.

SOMA HII PIA: Prediction Uholanzi vs Morocco FIFA Kombe la Dunia 2026: Team news, Predknockout preview, h2h, odds

Zaidi ya milioni 800 inashindaniwa, cheza kindege aviator ya SportPesa ushinde sasa

image
Win big with Aviator

Rekodi ya League 1

Hakimi alivaa kitambaa cha unahodha kwenye mchezo huu
Hakimi alivaa kitambaa cha unahodha kwenye mchezo huu

Tangu msimu wa 2007/07 Hakimi anakuwa mchezaji pekee wa nafasi ya ulinzi ambaye amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 5 katika mchezo mmoja. Hii inamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji bora viraka duniani. Hakimi amekuwa na mchango mkubwa sio tu kiulinzi lakini pia katika ushambuliaji.

SOMA HII PIA: Maoni: Kwa nini FIFA inapaswa kutoa nafasi kwa wachezaji wa ligi za ndani za Afrika kwenye Kombe la Dunia?

Hitimisho

Mafaniko binafsi ya Hakimi yanathibitisha umuhimu wa juhudi katika majukumu na kujifunza kila siku na ni funzo kwa wachezaji wengine. Si ajabu kuona amekuwa rafiki wa mastaa wakubwa wa soka Duniani wakiwemo Neymar na hata Mbappe. Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.