Bayern Munich 2-2 Dortmund | Kane akosa Penalti, Bundesliga, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

Full timeFull timeFull time

Bayern Munich 2-2 Dortmund | Kane akosa Penalti, Bundesliga, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

  • Mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or 2026, Harry Kane jana Jumamosi alikosa mkwaju wa Penalti katika mchezo wa matokeo ya sare wa Bayern Munich 2-2 Dortmund.
  • Ni mabao ya Konrad Laimer na Dayot Upamecano kwa Bayern Munich na Serhou Guirassy na Fabio Silva kwa Dortmund ndiyo yamelisababisha timu hizo kugawana pointi.
  • Matokeo hayo yanaifanya Bayern isalie kileleni mwa msimamo na pointi zao 18 sawa na Dortmund ambao wako kwenye nafasi ya pili na wanazidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.
  • Makala hii inachambua kwa picha baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu za mchezo huu.

Akitoka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka yaani Ballon d’Or 2026, Harry Kane jana Jumamosi alikosa mkwaju muhimu wa Penalti katika mchezo wa matokeo ya sare wa Bayern Munich 2-2 Dortmund. Kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Allianz Arena ni mabao ya Konrad Laimer na Dayot Upamecano kwa Bayern Munich na Serhou Guirassy na Fabio Silva kwa Dortmund ndiyo yamelisababisha timu hizo kugawana pointi. Matokeo hayo yanaifanya Bayern isalie kileleni mwa msimamo na pointi zao 18 sawa na Dortmund ambao wako kwenye nafasi ya pili na wanazidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

 SOMA HII PIA: Bayern Munich 6-1 RB Leipzig: Luis Diaz afunga hat trick Bundesliga 2026/27

Kipindi cha kwanza Bayern Munich 1-0 Dortmund

Laimer
Laimer

Bayern wakicheza nyumbani, walianza mchezo huo kwa kasi wakitaka kupata mabao ya mapema ili kujiweka katika ya kuondoka na point izote tatu muhimu. Jitihada zao zilizaa matunda dakika ya 38 kupitia kwa kinda wao Konrad Laimer. Bao hilo lilidumu mpaka kumalizika kwa kipindi cha 1.

SOMA HII PIA: Borussia Dortmund: Profile, History, Players, Stats, fixtures, results, standings& Latest News

Shinda mpaka shilingi Milioni 800 sasa, cheza kindege ‘aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini

image
Win big with Sportpesa Aviator

Kipindi cha pili Bayern Munich 2-2 Dortmund  

Harry Ballon d'Or
Harry Ballon d’Or

Kipindi cha pili timu hizo zilirejea uwanjani huku, Dortmund wakisukuma kwa nguvu mashambulizi ili kusaka bao la kusawazisha, huku Bayern wakisaka bao zaidi. Dakika ya 56 Bayern walipata Penalti ambayo Kane aliikosa. Hatimaye dakika ya 60, Serhou Guirassy aliifungia bao la kusawazisha. Bao hilo halikudumu kwani, Dayot Upamecano aliongeza bao kwa Bayern, dakika 6 tu baadae. Huku mchezo ukionekana huenda ungeisha kwa Bayern kushinda, Fabio Silva aliifungia Bayern bao la dakika za majrehu na mchezo ukaisha kwa sare ya 2-2.

SOMA HII PIA: Harry Kane ameshinda tuzo ya Ballon d’Or 2026: Orodha ya washindi 10 bora | Sadio Mane

Hitimisho

Matokeo haya yanatoa taswira ya vita kali ya ubingwa. Timu zote sasa zimefikisha pointi 18 kwenye msimamo. Huku Ligi hiyo ikiingia mzunguko wa 9, swali kubwa ni je, nani ataweza kushikilia bomba na kushinda mechi zake? Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.