Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026Lionel Messi
  • Kundi J, Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026 mchezo wa ufunguzi unatarajiwa kuchezwa Juni 17, 2026
  • Muda wa mchezo unaowakutanisha mabingwa watetezi Argentina vs Algeria ni saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
  • Lionel Messi na Riyad Mahrez wachezaji wakuchungwa kutokana na ubora wao uwanjani

Mabingwa watetezi Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026 ni mchezo kutoka Kundi J utakaokuwa ni ufunguzi kwa mataifa haya mawili. Argentina wameendelea kuonyesha ubora kwa kushinda mechi 5 za mwisho za kirafiki. Wana mtihani mkubwa kuhamisha kiwango hicho hadi kwenye mashindano ya Kombe la Dunia na kuendeleza walipoishia nchini Qatar, ambako walitwaa ubingwa.Saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Uwanja wa Kansas City, Missouri, Marekani.

Hii hapa ni ratiba ya mechi zote 104 FIFA Kombe la Dunia isome: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Kuna mamilioni yanakusubiri Twenzetu Duniani ya SportPesa Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Argentina vs Algeria kwa kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa wajibu.

Argentina
Argentina vs Algeria Odds zilizoimarishwa

Mabingwa Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026 taarifa muhimu kuhusu timu

Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026
Lionel Messi nahodha wa timu ya taifa ya Argentina.

Hii hapa ratiba ya Argentina isome: Ratiba ya Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mabingwa watetezi kikosi | Takwimu | SportPesa Blog

Kuelekea mchezo mkali utakaowakutanisha Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026 kila timu imejipanga kuanza vizuri mchezo wa kwanza. Algeria wanaingia kwenye michuano hii wakiwa na matokeo yanayochanganya pamoja na maoni tofauti kuhusu kocha wao, Vladimir Petkovic. Mbinu yake ya kumiliki mpira huku akicheza kwa tahadhari imekuwa ikizua mjadala miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka.

Argentina wataingia uwanjani wakiwa na dhamira ya kutuma ujumbe kwa mataifa mengine kwamba bado wamo katika harakati za kutetea taji lao la dunia. Kocha wa Argentina anatarajiwa kutumia mfumo wa 4-3-3, ukiwa na safu imara ya ulinzi ikiongozwa na Romero na Lisandro Martínez. Kiungo chenye ubunifu wa De Paul, Mac Allister na Enzo Fernández kwenye jukumu la kudhibiti mchezo, huku Lionel Messi akiongoza safu ya ushambuliaji pamoja na Julián Álvarez na Thiago Almada.

Algeria wanatarajiwa kucheza kwa mfumo wa 4-2-3-1, huku Bentaleb na Aouar wakitoa uwiano kati ya ulinzi na mashambulizi. Nahodha mwenye uzoefu Riyad Mahrez ataongoza safu ya ushambuliaji kutoka pembeni, akiungwa mkono na chipukizi mwenye kipaji Ibrahim Maza na kasi ya Mohamed Amoura, wakati Amine Gouiri akitarajiwa kuwa mshambuliaji wa kati.

Vikosi Vinavyotarajiwa kuanza Argentina vs Algeria

ArgentinaAlgeria
Emiliano MartínezLuca Zidane
Nahuel MolinaRafik Belghali
Cristian RomeroAïssa Mandi
Lisandro MartínezRamy Bensebaini
Nicolás TagliaficoRayan Aït-Nouri
Rodrigo De PaulNabil Bentaleb
Alexis Mac AllisterHoussem Aouar
Enzo FernándezRiyad Mahrez
Lionel MessiIbrahim Maza
Julián ÁlvarezMohamed Amoura
Thiago AlmadaAmine Gouiri

Hivi sio vikosi rasmi ni utabiri. Taarifa za vikosi rasmi vitatolewa muda mchache kabla ya mchezo.

H2H

Rekodi zinaonyesha kuwa Argentina vs Algeria zimekutana mara moja. Juni 5, 2007, Argentina 4-3 Algeria. Magoli 7 yalifungwa kwenye mchezo huo.Mara ya pili wanatarajiwa kukutana Juni 17, 2026 mchezo wa hatua ya makundi FIFA Kombe la Dunia.

Utabiri wa matokeo

Kwa karatasi, Argentina wanaonekana kuwa na kikosi chenye uzoefu mkubwa na ubora wa hali ya juu, hasa wakiongozwa na Lionel Messi katika harakati za kutetea ubingwa wao wa dunia. Hata hivyo, Algeria wana mchanganyiko mzuri wa uzoefu na vipaji vya vijana, jambo linaloweza kuwafanya kuwa wapinzani wagumu katika mchezo huu wa ufunguzi wa Kundi J.

Matokeo ya ubashiri inaweza kuwa Argentina 3-1 Algeria. Ushindi katika mchezo huu unaelekea kwa Argentina. Hii inatokana na aina ya wachezaji alionao na uzoefu. Haya sio matokeo rasmi ni maoni.

Lionel Messi bado ni nguvu ile ile ya mwaka 2022?

2022, Lionel Messi alikuwa katika kiwango cha kipekee kabisa. Akiungwa mkono na kikosi kilichokuwa na dhamira ya kuhakikisha anainua angalau Kombe moja la Dunia. Messi aliiongoza Argentina kwa ustadi mkubwa hadi kutwaa ubingwa kwa namna ya kuvutia.

Umaliziaji wake ulikuwa wa kiwango cha juu, pasi zake zilikuwa sahihi na zenye ubunifu mkubwa, na kila timu ilipoonekana kuyumba. Alikuwa mtu wa kuibeba mabegani na kuirejesha kwenye mstari. Alikuwa moyo na roho ya Argentina ana umri wa miaka 38 na akicheza katika ligi ya MLS akiwa na klabu ya Inter Miami.

Aidha, Julián Álvarez ameendelea kukua na kuthibitisha uwezo mkubwa aliouonyesha katika Kombe la Dunia lililopita. Hivyo, Messi ana msaada mzuri katika safu ya ushambuliaji, huku viungo na mabeki wengi walioshiriki safari ya ubingwa wa Qatar wakiendelea kuwepo.

Pia kuna vipaji vipya ambavyo bado havijajaribiwa kwenye Kombe la Dunia, kama vile Nico Paz na Thiago Almada. Kocha Lionel Scaloni ameonekana kujenga mifumo miwili yenye mafanikio: mmoja ukiwa na Messi uwanjani na mwingine bila yeye.Hata hivyo, Scaloni anatambua kuwa ikiwa Argentina wanataka kufika mbali katika ma Mshindano haya, basi nahodha wao atalazimika kuchimba ndani zaidi na kuibua tena ile X-Factor iliyowafanya kuwa mabingwa wa dunia.

Riyad Mahrez bado ni tegemeo la Algeria

Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026
Riyad Mahrez nyota wa Algeria.

Ijue ratiba ya Portugal: Ratiba ya Portugal FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika | Je, Ronaldo atabeba ubingwa?

Nyota mwingine ambaye amefikia hatua za mwisho za ubora wake lakini bado ana mchango mkubwa ni Riyad Mahrez, mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea Algeria. Mahrez bado anaonesha dalili za uchawi wake wa zamani. Ingawa ameonekana mara chache katika kiwango hicho akiwa na Klabu yake ya Al Ahli nchini Saudi Arabia, ameendelea kung’ara mara nyingi zaidi akiwa na timu ya taifa ya Algeria, hasa katika mechi za kufuzu.

Ili kuongeza nguvu ya ubunifu wa Mahrez, Algeria pia wana mshambuliaji kutoka kizazi kipya cha vipaji Ibrahim Maza, mwenye umri wa miaka 20. Maza ni mchezaji wa aina ya wapiga chenga wa asili. Akiwa katika siku yake nzuri, anaweza kuwaburudisha mashabiki na kuwasumbua mabeki kwa mbinu na ujasiri wake. Itakuwa jukumu la kocha Vladimir Petkovic kuhakikisha anamuweka katika mazingira yatakayomwezesha kuonesha uwezo wake huo.

Luca Zidane anatafuta historia

Langoni mwa Algeria, jina maarufu litakuwa kivutio kingine, Luca Zidane, mwana wa gwiji wa soka duniani Zinedine Zidane, hivi karibuni aliamua kuitumikia Algeria na ameonyesha kuwa ni kipa mwenye uwezo mkubwa wa kuwa chaguo la kwanza la timu hiyo. Akiwa nyuma ya safu ya ulinzi inayoundwa na wachezaji wenye uzoefu kama Ramy Bensebaini na Rayan Aït-Nouri, Algeria wanaonekana kuwa na msingi mzuri wa kutekeleza mtindo wa kumiliki mpira unaopendwa na kocha Petkovic.

Share this: