Yanga Vs Coastal UnionYanga Vs Coastal Union

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga wanaotamba na udhamini wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo Jumamosi watashuka katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuvaana na wenyeji wao Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku, kocha wa Yanga, Miguel Gamondi akilalamikia ugumu wa ratiba ambayo wamekuwa nayo katika siku za karibuni.

Yanga wanatarajia kuingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbuikumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu Bara ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.

ALICHOSEMA KOCHA GAMONDI

YANGA
Miguel Gamondi

Kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi katika mkutano na waandishi wa habari wa kabla ya mechi amesema: “Nimefurahi sana kuwa Arusha tena, kiukweli tuna ratiba ngumu kidogo, tumejaribu kupangilia ratiba yetu tupate angalau muda wa kupumzika. Hatupaswi kulalamika isipokuwa kupambana na hali halisi, ingawa ukweli ni kwamba hii sio ratiba nzuri ya kujiandaa na mchezo.

Yanga tuna utajiri mkubwa wa vipaji ambao unanipa wasaa wa kutumia mfumo wowote bila kuathiri ufanisi wa mchezaji mmoja mmoja. Ingawa mimi siamini sana kwenye mfumo bali namna gani sahihi ya kutengeneza nafasi na kuzitumia. Nina mawasiliano mazuri sana na wachezaji wangu wote licha ya kwamba sio wote wanapata nafasi”

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango wa timu hiyo, Khomein Abubakar amesema: “Kwanza tunamshukuru Mungu tumeamka salama na tumejiandaa vyema sana kuwapa furaha mashabiki wetu. Mwalimu ameshazungumza kila kitu muhimu ni kwenda kufuata maelekezo yake na kujituma. Yanga ni timu kubwa ina benchi la ufundi imara na kila kitu kinaenda sawa.

YANGA
Khomein Abubakar

“Hatuna presha yoyote, Tupo tayari kuisaidia timu kwa namna yoyote. Yeyote kati yetu atakayepewa nafasi basi atapaswa kuipambania timu. Naamini Diarra anasadifu mbinu za benchi letu la ufundi. Chochote kile atakachofanya Diarra ujue ni sehemu ya mbinu za timu ambazo sote kwa pamoja tunaziishi.”

Wananchi wakiwa na udhamini na Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imekuwa na mwanzo mzuri wa msimu, wakifanikiwa kushinda michezo yao yote sita ya kwanza, huku pia wakifaniwa kuandika rekodi ya kipekee ya kuwa timu pekee ambayo haijaruhusu bao msimu huu mpaka sasa.

NJIA ZA MABAO YANGA HIZI HAPA

Mpaka sasa Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wamefanikiwa kufunga mabao 11 katika michezo yao sita ambayo wamecheza huku wakiwa hawajaruhusu kufungwa bao lolote, ambapo mastaa Maxi Nzengeli, Chama, Pacome na Ibrahim Bacca wakiongoza katika kuitafutia mabao.

Maxi Nzengeli, mpaka sasa amefanikiwa kuchangia mabao matatu akifunga mabao mawili na kusaidi upatikanaji wa bao moja. Ibrahim Bacca ambaye msimu uliopita alishinda tuzo ya mlinzi bora msimu huu naye ameifungia Yanga mabao mawili huku mastaa kama Chama na Pacome wakichangia bao moja kila mmoja.

MATOKEO YA MECHI ZILIZOPITA YANGA HAYA HAPA

YANGA
Zimbwe Jr akipambana na Pacome

Mchezo wa kwanza Wananchi walikuwa ugenini mkoani Kagera kuwavaa Kagera Sugar ambapo mpaka kipyenga cha mwamuzi kuashiria kumalizika kwa dakika 90za mchezo huo ubao wa matokeo uwanjani ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga mchezo huu ulichezwa Uwanja wa Kaitaba, Agosti 29 2024 huku mmojawapo wa wafungaji katika mchezo huo akiwa ni kiungo wao wa kimataifa wa DR Congo, Maxi Nzengeli.

Bao hilo pia lilimfanya Maxi aandike rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuifungia Yanga bao msimu huu.

Mchezo wa pili ilikuwa dhidi ya ambapo ulimalizika kwa matokeo ya Ken Gold 0-1 Yanga huu ulikuwa mchezo wa pili kwa Yanga ugenini, ilikuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo mfungaji wa bao hilo pekee alikuwa, Ibrahim Bacca ambaye alitumia pasi ya Aziz Ki Septemba 25, 2024 mwaka huu na kuisaidia Yanga kukusanya pointi tatu nyingine ugenini.

Yanga 1-0 KMC, mchezo wa kwanza wakiwa Uwanja wa Azam Complex msimu wa 2024/25 ilikuwa Septemba 29, 2024. Mchezo wanne Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba Jiji ilikuwa Oktoba 3, 2024 kabla ya kuifunga Simba bao 1-0 Oktoba 19, mwaka huu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.