Camara AirCamara Air

MAKIPA wawili kutoka timu za Kariakoo, Yanga na Simba wamekuwa kwenye vita yao nzito kwelikweli ndani ya uwanja katika kutimiza majukumu ambapo kila mmoja anapambania kuonyesha uwezo wake ndani ya dakika 90 uwanjani msimu wa 2024/25.

Hapa tunakuletea rekodi za makipa wawili ikiwa ni Djigui Diarra wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi akiwa kacheza mechi zote za ushindani msimu huu kwenye ligi bila kufungwa.

Diarra ameanza langoni mechi zote tano za Yanga ambapo hawajafungwa zaidi ya kushuhudia timu hiyo ikishinda mfululizo na kukomba pointi 15 mazima ndani ya ligi kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

MATOKEO YA DIRRA MADAKA MISHALE WA YANGA

Ateba na Diarra
Lioel Ateba na Diarra kwenye Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa, Oktoba 19 2024. Source: Simba.

Kagera Sugar 0-2 Yanga mchezo huu ulichezwa Uwanja wa Kaitaba, Agosti 29 2024 na mtupiaji wa bao la kwanza ni Maxi Nzengeli ndani ya Yanga kwenye ligi.

Ken Gold 0-1 Yanga huu ulikuwa mchezo wa pili kwa Yanga ugenini ilikuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya mtupiaji alikuwa ni Ibrahim Bacca ambaye alitumia pasi ya Aziz Ki Septemba 25 2024.
Yanga 1-0 KMC, mchezo wa kwanza wakiwa Uwanja wa Azam Complex msimu wa 2024/25 ilikuwa Septemba 29 2024.

Yanga 4-0 Pamba Jiji ushindi mkubwa kwa Yanga ndani ya 2024/25 walikuwa Azam Complex  ilikuwa Oktoba 3 2024. Kwenye mchezo huu kiungo Aziz Ki alifunga bao lake la kwanza ndani ya msimu ilikuwa kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Jean Baleke aliyechezewa faulo ndani ya 18 na wapinzani wao Pamba Jiji.

Oktoba 14 2024, Simba 0-1 Yanga mchezo wa kwanza kupoteza mtupiaji ni Maxi Nzengeli dakika ya 86. Yanga ipo nafasi ya 3 safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 9 kinara ni Maxi mwenye mabao manne na mkali wa pasi ni Aziz Ki mwenye pasi tatu za mabao. Oktoba 22 Yanga itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Azam Complex.

HUYU HAPA CAMARA

Camara Pinpin
Camara Pinpin kipa wa Simba akiwa kwenye uwanja wa mazoezi. Source: Simba.

Mussa Camara yeye ni kipa namba moja wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids akiwa kwenye mtihani mzito kurejesha hali ya kujiamini kutokana na kufungwa kwenye mechi za hivi karibuni. Mechi moja Simba ilipata pointi moja na mchezo mwingine ilipoteza mazima pointi tatu ikiwa nyumbani.

Ikumbukwe kwamba kipa huyo kwenye mechi nne mfululizo ambazo alianza kikosi cha kwanza katika mechi za Ligi Kuu Bara hakufungwa na alikuwa imara kwenye kucheza na kutoa maelekezo kwa wachezaji wenzake ndani ya uwanja.

Mchezo wa kwanza kufungwa ilikuwa dhidi ya Coastal Union kwa msimu wa 2024/25 ambapo katika mchezo huo walitoshana nguvu na wapinzani wao kwa kufungana mabao 2-2 wakigawana pointi mojamoja.

Wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga, Camara katika harakati za kuokoa alitema mpira uliokuwa mikooni mwake na kuuludisha ndani ya 18 jambo lililompa nafasi Maxi Nzengeli kufunga bao dakika za lala salama.

Ni mechi sita ambazo Simba imecheza dakika 540, kipa huyo kafungwa mabao matatu kwenye mechi mbili mfululizo ambazo ni dakika 180. Oktoba 22 2024 Simba ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Tanzania Prisons mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Ipo wazi kuwa Simba inapokutana na Tanzania Prisons kazi huwa nzito kwa timu zote mbili kutokana na kila mmoja kujipanga kusepa na pointi tatu muhimu ndani ya uwanja baada ya dakika 90.

HIZI HAPA MECHI ZA CAMARA

Camara
Camara Mussa kipa namba moja wa Simba 2024/25. Source: Simba.

Simba 3-0 Tabora United mchezo huu ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa Agosti 18 2024 ni mchezo wa kwanza kwa Simba kwenye ligi na mtupiaji bao la kwanza ni Che Malone ilikuwa dakika ya 14 akitumia pasi ya Jean Ahoua.

Simba 4-0 Fountain Gate, huu ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Simba ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa Agosti 25 2024.

Azam FC 0-2 Simba huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Simba kucheza ugenini ulichezwa Uwanja wa New Amaan Complex Septemba 26 2024.

Dodoma Jiji 0-1 Simba ilikuwa Septemba 29 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma walisepa na pointi tatu kwenye mchezo huu.

Simba 2-2 Coastal Union uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa ni Oktoba 4 2024.

Prince Dube
Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube akipambana kwenye mchezo dhidi ya Simba Uwanja wa Mkapa, Oktoba 19 2024. Source: Yanga.

Oktoba 14 2024, Simba 0-1 Yanga mchezo wa kwanza kupoteza mtupiaji ni Maxi Nzengeli dakika ya 86.

 

Share this: