Ronaldo (-)Ronaldo (-)
  • Portugal vs Uzbekistan Kombe la Dunia 2026, ratiba inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki, has awa Ureno
  • Mechi hii ya Kundi K Kombe la Dunia la FIFA 2026, inatarajiwa kupigwa 23 June 2026 saa 2 usiku, kwa saa za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Houston.
  • Je, Cristiano Ronaldo atafufuka na kuwaziba midomo wakosoaji wake?
  • Nakala hii inachambua kitaalamu kuhusu utabiri, h2h, lineups, stats, na Habari za timu za mechi hii.

Baada ya mwanzo usiotarajiwa wa sare ya bao 1-1 dhidi ya DR Congo, Portugal watavaana na Uzbekistan katika mchezo wao wa pili wa Kundi K Kombe la Dunia la FIFA 2026. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa 23 June 2026 saa 2 usiku, kwa saa za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Houston, au NRG. Nakala hii inachambua kitaalamu kuhusu utabiri, h2h, lineups, stats, na Habari za timu za mechi hii.

Portugal vs Uzbekstan
Portugal vs Uzbekistan

Muhtasari wa mechi ya Portugal vs Uzbekistan

Portugal vs Uzbekistan Kombe la Dunia 2026
Matokeo ya mechi ya kwanza ya Portugal

Kikosi cha Ureno ya kocha Roberto Martinez kilikwama baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya DR Congo katika mechi yao ya kwanza ya Kundi K. Matokeo hayo yamewafanya Portugal kusalia nafasi ya tatu wakiwa na alama moja. Vinara wa Kundi K ni Colombia, ambao wanaongoza kundi hilo kwa alama tatu baada ya kuifunga Uzbekistan mabao 3-1 katika mchezo wao wa ufunguzi.

Joao Neves aliifungia Portugal bao lao pekee dakika ya sita, kabla ya bao la kusawazisha la Yoane Wissa. Portugal wanawania kutwaa taji lao la kwanza kabisa katika historia ya la Kombe la Dunia, hivyo wanahitaji ushindi ili kuendelea na matumaini ya kutimiza ndoto hiyo. Cristiano Ronaldo, ambaye anaelezwa kuwa anashiriki mashindano haya kwa mara ya mwisho, ataiongoza nchi yake.

Uzbekistan, kwa upande mwingine, wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao. Abbosbek Fayzullaev aliandika historia kwa kufunga bao lao la kwanza kabisa katika mashindano hayo, licha ya timu yao kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Colombia. Portugal wanaingia kwenye mashindano haya wakiwa nafasi ya 5 duniani, huku Uzbekistan wakiwa katika nafasi ya 50.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII PIA: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Wapi kwa kutazama (How to watch) Portugal vs Uzbekistan Kombe la Dunia 2026

Mashabiki wanaweza kufuatilia mechi ya Argentina vs Austria kupitia watangazaji rasmi wa FIFA World Cup 2026 katika nchi zao. Kwa Tanzania, angalia ratiba ya matangazo ya washirika rasmi wa FIFA, na fuatilia SportPesa Blog kwa live score, matokeo, highlights na taarifa za mchezo.

Habari za Timu

Hakuna majeruhi walioripotiwa kutoka kambi za timu zote mbili mpaka sasa. Hivyo vikosi kamili kinatarajiwa kuanza. Hii hapa listi ya vikosi vinavyotarajiwa kuanza, vikosi hivi vinatokana na tathmini ya takwimu za wachezaji na utimamu wao wa mwili, listi kamili itatolewa pale vikosi rasmi vitakapothibitishwa kabla ya mechi kuanza.

Portugal

Portugal vs DR Congo
Baadhi ya mastaa wa kuchungwa
NafasiMchezajiKlabu (2026)Maelezo mafupi
KipaDiogo CostaFC PortoKipa tegemeo wa Portugal anayejulikana kwa utulivu wake, uwezo mzuri wa kuokoa mipira na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma.
BekiJoão CanceloAl-HilalBeki wa pembeni mwenye uzoefu mkubwa, anayependa kupanda kushambulia na kutoa pasi za mwisho zenye ubora.
BekiRúben DiasManchester CityKiongozi wa safu ya ulinzi mwenye uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, kushinda mipira ya juu na kuhamasisha wenzake.
BekiTomás AraújoBenficaBeki chipukizi mwenye utulivu na nidhamu ya hali ya juu, anayejitokeza kwa uwezo wake wa kukaba na kupiga pasi sahihi.
BekiNuno MendesParis Saint-GermainBeki wa kushoto mwenye kasi na nguvu, anayechangia kwa kiwango kikubwa katika ulinzi na mashambulizi.
KiungoVitinhaParis Saint-GermainKiungo mbunifu mwenye uwezo wa kudhibiti kasi ya mchezo na kusambaza pasi zenye usahihi mkubwa.
KiungoJoão NevesParis Saint-GermainMchezaji kijana mwenye bidii kubwa, anayesaidia kulinda safu ya ulinzi na kuanzisha mashambulizi kwa ufanisi.
KiungoBernardo SilvaManchester CityKiungo mwenye ufundi wa hali ya juu, anayejulikana kwa ubunifu, udhibiti mzuri wa mpira na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao.
MshambuliajiBruno FernandesManchester UnitedMchezaji mwenye maono makubwa uwanjani, anayebuni nafasi nyingi na kuwa tishio kupitia pasi za mwisho na mashuti ya mbali.
MshambuliajiCristiano RonaldoAl-NassrNahodha wa Portugal na mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani, anayejulikana kwa uwezo wake wa kufunga mabao katika nyakati muhimu.
MshambuliajiPedro NetoChelseaWinga mwenye kasi, ujasiri wa kuwakabili mabeki na uwezo wa kuunda nafasi za hatari katika eneo la ushambuliaji.

Uzbekistan

NafasiMchezajiKlabu (2026)Maelezo mafupi
KipaUtkir YusupovNavbahor NamanganKipa mwenye uzoefu anayejulikana kwa utulivu wake golini, uwezo wa kuokoa mipira migumu na kuongoza safu ya ulinzi.
BekiAbdukodir KhusanovManchester CityBeki kijana mwenye nguvu na kasi, anayesifika kwa uwezo wake wa kukaba, kusoma mchezo na kuzuia mashambulizi ya wapinzani.
BekiBekhruz KarimovNeftchi FerganaMlinzi mwenye nidhamu ya hali ya juu, anayechangia katika uimara wa safu ya nyuma kupitia ukabaji makini na mipira ya juu.
BekiJakhongir UrozovPakhtakor TashkentBeki mwenye uwezo wa kucheza nafasi tofauti za ulinzi, anayejulikana kwa utulivu na umakini katika maamuzi yake.
KiungoSherzod NasrullaevPakhtakor TashkentKiungo mwenye bidii kubwa anayesaidia timu katika majukumu ya ulinzi na kushambulia kupitia pasi sahihi na harakati nyingi uwanjani.
KiungoAbdulla AbdullaevDinamo SamarqandMchezaji wa katikati mwenye uwezo wa kudhibiti mpira na kusaidia kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji.
KiungoAkmal MozgovoyNasaf QarshiKiungo mbunifu mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi na kusambaza pasi muhimu katika maeneo ya hatari.
KiungoOtabek ShukurovAl-FayhaMchezaji mwenye uzoefu mkubwa katika safu ya kiungo, anayejulikana kwa uwezo wake wa kupora mipira, kupiga pasi ndefu na kuongoza wenzake.
MshambuliajiAbbosbek FayzullaevCSKA MoscowMshambuliaji kijana mwenye kipaji kikubwa, anayesifika kwa kasi, ufundi wa kupenya ulinzi na uwezo wa kufunga na kutengeneza mabao.
MshambuliajiOston UrunovPersepolisWinga mwenye kasi na ustadi wa kuwapita mabeki, anayetoa mchango mkubwa katika mashambulizi ya Uzbekistan.
MshambuliajiEldor Shomurodovİstanbul BaşakşehirNahodha na mshambuliaji tegemeo wa Uzbekistan, anayejulikana kwa uzoefu wake, uwezo wa kumalizia nafasi na kuhamasisha wachezaji wenzake.

KUJUA UCHAMBUZI WA MECHI INAYOFUATA YA SENEGAL, SOMA HII: Norway vs Senegal Prediction: FIFA Kombe la Dunia 2026 Kundi I, lineups, h2h, muda wa mchezo

Rekodi ya h2h Portugal vs Uzbekistan

Huu unatarajiwa kuwa mchezo wa kwanza kabisa katika historia kati ya Portugal kukutana na Uzbekistan. Portugal wanaingia katika mchezo huu wakiwa hawajapoteza mechi saba mfululizo. Kabla ya sare dhidi ya DR Congo, walikuwa wameshinda mechi tatu mfululizo, wakifunga mabao 6 na kuruhusu bao 1 pekee. Uzbekistan wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wamepoteza mechi tatu mfululizo, ambapo wamefungwa mabao 7 huku wao wakifunga 2 pekee.

Utabiri wa Portugal vs Uzbekistan: Portugal kushinda

Kombe la Dunia
Kombe la Dunia

Portugal wana kikosi bora zaidi ukilinganisha na Uzbekistan, na wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi. Wanahitaji ushindi huu ili kurejesha matumaini ya kampeni yao ya kutwaa Kombe la Dunia. Kutokana na presha waliyonayo ya kutafuta alama zote tatu, tunatarajia kuona kikosi cha Roberto Martinez kikitawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kumbuka haya si matokeo rasmi, hivyo Bashiri kistaarabu.

Pata Odds kubwa na Jinsi ya kuweka dau kwenye SportPesa

Chagua soko lako — Dau la Mchezo Mmoja (SB), Multi-Bet (MB), au Dau la Moja kwa Moja (LB) mechi ikianza.

Weka kiasi cha dau na uthibitishe dau lako.

Hitimisho

Utabiri wetu wa kiuhariri unaipa nafasi kubwa ya ushindi kwa Portugal, hii ni kutokana na tathmini ya ubora wa vikosi na kimbinu. Portugal pia wanatarajiwa kutawala sehemu kubwa ya mchezo huu. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Portugal vs Uzbekistan kwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Uzbekistan vs Colombia FIFA Kombe la Dunia 2026

Portugal vs Uzbekistan itaanza saa ngapi?

Mechi itaanza saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki 23 June 2026 katika Uwanja wa Houston, Marekani.

Nini kilitokea katika mechi ya kwanza ya Portugal kwenye Kombe la Dunia 2026?

Portugal walilazimishwa sare ya bao 1-1 na DR Congo vs katika mechi ya kwanza ya Kundi J.

Nini kilitokea katika mechi ya kwanza ya Uzbekistan kwenye Kombe la Dunia 2026?

Uzbekistan ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Colombia.

Je, Portugal na Uzbekistan zimewahi kukutana hapo awali?

Hapana, timu hizi hazijawahi kukutana kwenye mechi yoyote hapo kabla, hivyo huu utakuwa mkutano wao wa kwanza wa kihistoria.

Portugal na Uzbekistan zipo kundi gani katika Kombe la Dunia 2026?

Timu zote mbili zipo Kundi K pamoja na Colombia na DR Congo.

KUJUA RATIBA YA MECHI INAYOFUATA YA ARGENTINA, SOMA HII: Argentina vs Austria Kombe la Dunia 2026: prediction, Live score, lineups, vikosi, h2h, live score, odds

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.