Ateba v AuchoAteba v Aucho

SIMBA imepoteza mchezo wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga katika Kariakoo Dabi iliyokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ilishinda mchezo huo ikikomba pointi tatu mazima ikiwa ugenini, hapa tunakuletea rekodi za mastaa wa Simba ndani ya uwanja namna hii:-

Mussa Camara

Camara
Camara Mussa, kipa wa Simba ambaye alianza Kariakoo Dabi Oktoba 19 2024. Source: Simba.

Alianza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids alikomba dakika zote 90 kwenye kuokoa mguu wake wenye nguvu ulikuwa ni ule wa kulia ambao ulipiga zaidi ya pasi 12. Pasi zake kwa asilimia kubwa zilikuwa zikiwafikia walengwa na alitumia mguu wa kushoto kutoa pasi zaidi ya tatu.

Katika kutimiza majukumu yake aliokoa hatari zaidi ya nne licha ya kufungwa bao moja dakika ya 86 na Maxi Nzengeli. Miongoni mwa hatari ambazo aliokoa ilikuwa dakika ya 41, 54, 56, 70, 71 hii ilitokana na pasi fupi aliyompa beki wake wakati anataka kupiga pasi akateleza, hivyo ilimlazimu kuifuata na kuokoa, dakika ya 73.

SHOMARI KAPOMBE

Legend kwenye ubora uleule wa siku zote, hakuwa na mambo mengi utulivu katika kuokoa hatari na kupiga krosi. Miongoni mwa krosi aliyopiga ilikuwa dakika ya 60.

MOHAMED HUSSEN ZIMBWE JR

Nahodha wa Simba kwenye majukumu yake, ubora uleule kazini alikuwa anapanda na kushuka aliokoa hatari ikiwa ni pamoja na dakika ya 18, 61 alipewa majukumu ya kupiga faulo ilikuwa dakika ya 55 alichezewa faulo dakika ya 80 na alikomba dakika zote 90.

ABDLUAZAK HAMZA

Alianza kikosi cha kwanza alicheza faulo dakika ya 20, 50 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 50, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 37 hakusepa na dakika 90 alipata maumivu na dakika ya 68 Chamou aliingia kuchukua mikoba yake.

CHE MALONE

Aziz KI V Chemalone
Aziz KI V Chemalone kwenye Kariakoo Dabi, Oktoba 19 2024. Source: Yanga.

Safu ya ulinzi ilikuwa inaongwa na Che Malone aliokoa hatari zaidi ya mbili na miongoni mwa hizo ilikuwa dakika ya 43, 59, 64 alikomba dakika zote 90.

KAGOMA YUSUPH

Kiungo Yusuph Kagoma alichezewa faulo dakika ya 4, 28, licheza faulo dakika ya 17 alikwama kukomba dakika 90 aligotea dakika ya 45 nafasi yake ilichukuliwa na Okejapha.

KIBU DENNIS

KIBU Dennis anaingia kwenye orodha ya mchezaji aliyechezewa faulo nyingi zaidi Kariakoo Dabi, Oktoba 19 2024.

 

Miongoni mwa hizo ilikuwa dakika ya 8, 30, 45, 46 alikutwa katika mtego wa kuotea dakika ya 9, 49 alicheza faulo dakika ya 13, 15 na alisababisha kadi ya njano moja kwa Dickson Job dakika ya 46 alikomba dakika 81 akaingia Kelvin Kijili.

 

MAVAMBO

Mavambo alicheza faulo dakika ya 23, 31, 44 na alichezewa faulo dakika ya 34 alikomba dakika 90 kwenye ubora wake.

 

ATEBA v Bacca
MSHAMBULIAJI wa Simba Leonal Ateba akipambana na beki wa Yanga, Bacca. Source: Yanga.

ATEBA

Leonel Ateba mshambuliaji wa Simba alikomba dakika 90 alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 5 iliyookolewa na kipa Djigui Diarra, alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 16 alichezewa faulo dakika ya 62, 71.

 

AHOUA

Jean Ahoa kiungo mshambuliaji wa Simba alikomba dakika 90, alicheza faulo dakika ya 12, 45 alionyeshwa kadi ya njano. Alichezewa faulo dakika ya 27, 36, 54, 78 alipiga faulo dakika ya 2, 36, 37, 48, 73.

 

Mutale
Mutale kiungo wa Simba alianza kikosi cha kwanza Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga, Oktoba 19 2024. Source: Simba.

JOSHUA MUTALE

Kiungo Mutale alipewa majukumu ya kupiga kona ilikuwa dakika ya 49, 50, 56, 57 alikomba dakika 68 nafasi yake ilichukuliwa na Edwin Balua.

 

MECHI ZIJAZO KWA SIMBA

Tanzania Prisons watawakaribisha Simba itakuwa Oktoba 22 Uwanja wa Sokoine
Namungo watakaribishwa na Simba Oktoba 25 itakuwa Uwanja wa KMC Complex
JKT Tanzania Oktoba 29 Uwanja wa KMC Complex.

HUYU HAPA SEMAJI ALLY

Ahmed Ally
Ahmed Ally Ofisa Habari wa Simba, 2024. Source: Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika namna hii: “Tunaumia kwa kupoteza mchezo wa derby lakini tunajipongeza kwa kuwa mradi wetu wa kutengeneza timu umeanza kutoa matunda tena kwa haraka sana. Wote ni mashahidi misimu kadhaa nyuma tulifungwa derby na kuzidiwa kwa dakika zote 90.

“Tumeona tofauti kubwa, tumefungwa lakini tumeutawala mchezo kwa asilimia kubwa na kama kila kitu kingekua sawa basi tungeshinda mchezo ule. Muhimu kwetu wana Simba kwanza tukubali tumepoteza na wala hakuna haja ya kuanza kuhesabu tumepoteza mara ngapi. Mpira ni maisha ya duara muda wetu utafika na sisi tutatawala derby kwani tumewahi kufanya hivyo.

“Muhimu kwa sasa ni kusahau yaliyotokea na kujipanga upya kwa vita iliyo mbele yetu. Tumebakiwa na michezo 24 nguvu kubwa iwe kushinda michezo hiyo, tumepoteza derby sio ubingwa. Na pia tuwekeze nguvu kwenye mchezo wetu Jumanne dhidi ya Tanzania Prisons. Ubaya Ubwela unaendelea.”

 

Share this: