LEO Jumamosi usiku moto utawaka kwenye dimba la Santiago Bernabeu nchini Hispania pale mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Real Madrid watakapowakaribisha wapinzani wao wakuu, Barcelona katika mchezo mkubwa wa El Classico.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 4 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambapo habari mbaya kwa Madrid ni kukubwa na balaa la majeraha ambapo taarifa mpya ni kuwa wanatarajia kumkosa kipa wao namba moja, Thibaut Courtois na mshambuliaji Rodrygo.
Unaweza kubashiri mechi hii kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza link hii https://sportpesa.co.tz/
Kutokana na kukosekana kwa Rodrygo, kiungo wa timu ya Taifa ya England, Jude Bellingham huenda akabadilishiwa majukumu leo na kuziba pengo la Rodrygo huku mlinda mlango, Andriy Lunin akitarajiwa kuchukua nafasi ya, Courtois.
Pamoja na wachezaji hao wawili, mastaa wengine ambao wanatarajiwa kukosekana kwenye kikosi cha Real Madrid ni walinzi, David Alaba na Dani Carvajal huku nyota, Brahim Diaz akiwa kwenye hatihati ya kucheza ama kutocheza.
HABARI NJEMA KWA MADRID

Habari njema kwa Los blancos ni urejeo wa kiungo wao, Aurélien Tchouameni ambaye alitangazwa kurejea mazoezini kabla ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya, Borussia ambao waliibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Mchezo wa El Clasico ni miongoni wa mechi maarufu zaidi duniani ambayo inavuta hisia za mashabiki wengi wa soka na kuhusiha timu mahasimu wawili wakubwa nchini Hispania.
REKODI ZINASEMAJE
Real Madrid na Barcelona kwa ujumla zimekuitana katika michezo 257 ya kiushindani ambapo Real Madrid waefanikiwa kushinda mara 105, huku Barcelona wao wakiibuka na ushindi mara 100 huku mechi 52 zikiisha kwa matokeo ya sare.
Mpaka sasa Barcelona wanaongoza msimamo na ligi kuu ya Spain, La Liga na wataingia katika mchezo huu wakisaka matokeo ya ushindi ili kujiimarisha kileleni mwa msimamo.
Kuelekea katika mchezo huo kama sehemu ya hamasa, staa kinda wa Barcelona, Lamine Yamal ameonyesha seti ya vito vyake vya thamani kwa ajili ya meno yake vyenye mfano wa nyota za rangi ya bluu na nyekundu ambazo ni rangi za klabu hiyo.
Nyota huyo kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita amekuwa akiimbwa zaidi kutokana na ubora mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha kwenye kikosi cha Barcelona na timu ya Taifa ya Uhispania, hususani kwenye mashindano ya Euro akiiongoza timu hiyo kushinda ubingwa mbele ya England.
Akiwa na umri wa miaka 17 tu, tayari nyota huyo anaongoza msimamo wa wachezaji waliopika mabao mengi, akitoa asisti sita mpaka sasa huku mshambuliaji wa timu hiyo, Robert Lewandowski akiwa ameweka kambani mabao 12 katika michezo 10 aliyocheza mpaka sasa.
Mpaka sasa kikosi cha Real Madrid kiko nyuma kwa pointi tatu dhidi ya Barcelona na tofauti ya mabao inawahitaji Los Blancos kushinda mabao 11 ili kuongoza msimamo.
Yamal anatarajiwa kushinda kinyang’anyiro cha tuzo ya Kopa ambayo inatolewa kwa mchezaji mwenye umri mdogo ambaye anefanya vizuri zaidi kwa mwaka uliopita, tuzo hiyo imewahi kubebwa na mastaa kama: Jude Bellingham, Pedri na Gavi.
Kinda huyo alikuwa miongoni mwa mastaa ambao waliunda kikosi kilichoifunga Bayern Munich 4-1 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki hii.
KOMPANY AMTAJA YAMAL KUWA MRITHI WA MESSI

Kufuatia kipigo hicho, kocha wa Bayern, Vincent Kompany ameweka wazi kuwa anamtazamia, Yamal kuwa mbadala wa, Lionel Messi. Kompany amesema: “Ni jambo la kipekee kwa Barcelona kuwa na mchezaji kama Yamal muda mfupi baada ya kuondoka kwa Lionel Messi.
“Wakati nikicheza, Messi alikuwa mmoja wa alama za soka. Muda mfupi baada ya kuondoka kwa Messi tayari Barca wamepata mchezaji wa aina yake na hili ni jambo la kipekee sana.
Kompany pia amesifu ubora wa kituo cha kukuzia vipaji cha La Masia, kwa kumkuza, kumlea, kumwamini na kumpa nafasi Yamal kama ambavyo walifanya kwa Messi.
Ikumbukwe Messi alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 tu, kutokea kwao nchini Argentina ambapo kwa kipindi chake chote cha soka alicheza nchini Uhispania na kuwa gwiji wa Barcelona kabla ya kujiunga na Paris Saint German na sasa kuuwasha moto Marekani.

