Che Malone v PrisonsChe Malone v Prisons

WAKIWA ugenini Simba walipambana kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons, haukuwa mchezo mwepesi ni bao moja lilipatikana likifungwa dakika ya 5 kupitia kwa beki Che Malone ambaye anafikisha mabao mawili ndani ya ligi msimu wa 2024/25.

Ubao wa Uwanja wa Sokoine kwenye mchezo huo ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Simba. Ikumbukwe kwamba pigo la faulo dakika ya 5 ilikuwa kazi ya Kibu Dennis lilimshinda mlinda mlango Mussa Mbisa kwenye harakati za kuokoa ukakutana na Che Malone.

Hapa tunakuletea rekodi za mastaa wa timu zote mbili baada ya walichofanya ndani ya uwanja namna hii:-

Camara Air
Camara Air kipa namba moja wa Simba 2024/25. Source: Simba.

MOUSSA CAMARA

Kipa wa Simba alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 53, 54, 59, 82 alipiga faulo dakika ya 74. Alikomba dakika 90 na hakufungwa.

CHE MALONE

Alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo, alifunga bao dakika ya 5 akiwa ndani ya 18, alicheza faulo dakika ya 29, aliokoa hatari dakika ya 85.

AWESU AWESU

Awesu Awesu
Awesu Awesu kiungo wa Simba alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Tanzania Prisons. Source: Simba.

Alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 46, alipiga kona dakika ya 51 alichezewa faulo dakika ya 27, 28, alipiga krosi dakika ya 41 na alikomba dakika 61 nafasi yake ilichukuliwa na Joshua Mutale ambaye alipiga kona dakika ya 76, 78, alichezewa faulo dakika ya 77, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 62.

LADACK CHASAMBI

Alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 63, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 28, alikomba dakika 84 nafasi yake ilichukuliwa na Mzamiru Yassin.

KIBU DENNIS

Alipiga faulo Kibu Dennis dakika ya 5, 38, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 31, alichezewa faulo dakika ya 60, 74.

MOHAMED HUSSEN

Alipiga faulo dakika ya 35, alichezewa faulo dakika ya 38, alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 39, 49 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 40. Alikomba dakika 61 nafasi yake ilichukuliwa na Edwin Balua ambaye alipiga faulo dakika ya 73, 77.

SHOMARI KAPOMBE

Kapombe
Kapombe Shomari beki wa kupanda na kushuka Simba 2024/25.Source: Simba.

Aliokoa hatari dakika ya 36 alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 45, 90 alipiga faulo dakika ya 67.

LEONEL ATEBA

Alichezewa faulo dakika ya 28, alipiga krosi dakika ya 52, 63, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 69 shuti ambalo lililenga lango dakika ya 58. Alikomba dakika 72 nafasi yake ilichukuliwa na Steven Mukwala aliyepiga mashuti yaliyolenga lango dakika ya 76, 85.

CHA MOAH

Alichezewa faulo dakika ya 7 aliokoa hatari dakika ya 45, 88 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 47.

 

MUSSA MBISA

Kipa namba moja wa Tanzania Prisons alianza langoni kutimiza majukumu yake, dakika ya 5 alitunguliwa bao moja na Che Malone kwa kosa la kutema mpira uliopigwa na Kibu Dennis.

Aliokoa hatari dakika ya 37, 41, 55, 56, 64, 73, 76. Alikomba dakika 90 kwenye mchezo huo wakiwa nyumbani.

HAJI MUSSA

Anaingia kwenye orodha ya nyota walioonyeshwa kadi ya njano ilikuwa dakika ya 27.

HARUNA CHANONGO

Alipiga krosi dakika ya 53 alichezewa faulo dakika ya 29 alikomba dakika 67 nafasi yake ilichukuliwa na Jumanne Elifadhili.

EZEKIEL MWASHILINDI

Alicheza faulo dakika ya 38, 77 alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 35.

JEREMIA JUMA

Alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 36, alipiga krosi dakika ya 54, alikomba dakika 67.

ISMAIL MHESA

Kibu
Kibu Dennis dhidi ya Ismail Mhesa kwenye mchezo wa ligi, Uwanja wa Sokoine. Source: Simba.

Aliokoa hatari dakika ya 43, 50, 56 alicheza faulo dakika ya 40, 74 alionyeshwa kadi ya njano.

 

SAMSON MBANGULA

Nyota huyu alianza kikosi cha kwanza alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 42.

ZABONA MWAYOMBWA

Zabona Mwayombwa liokoa hatari dakika ya 43, alipiga krosi dakika ya 55 alikomba dakika 82.

DOTTO SHABAN

Alipiga shuti ambalo halikulenga lango ilikuwa dakika ya 86 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 75 .

SEMAJI AHMED

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa pointi tatu kwenye mchezo huo zilikuwa ni muhimu kwa kuwa zimetibu matatizo mengi ambayo yalikuwa yanawasumbua kwa wakati huo.

“Ushindi ambao tumepata dhidi ya Prisons ni ushindi muhimu kwa kuwa pointi ambazo tumezipata zimeondoa matatizo mengi yaliyokuwa yanatusumbua hivyo tunaamini wakati ujao tutazidi kuwa imara zaidi, mashabiki tuendelee kujitokeza uwanjani.”

Share this: