Bacca v AtebaBacca v Ateba

NGOMA imegota mwisho dakika 90 kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza kwa wanaume 22 kufanya kazi kubwa katika msako wa pointi tatu ambazo mwisho ni Yanga waliibuka wababe kwenye mchezo huo huku tambo zikipoa.

Mtoto hakutumwa dukani na mvua ilinyesha Uwanja wa Mkapa mwisho mbabe alikuwa Yanga mchezo wa kwanza msimu wa 2024/25 huku Maxi Nzengeli aliyetoa krosi iliyoleta bao baada ya beki wa Simba Kelvin Kijili kujifunga dakika ya 86 kwenye harakati za kuokoa akiibuka kuwa mchezaji bora.

Hapa tunakuletea rekodi za mastaa wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ndani ya uwanja Oktoba 19 2024 kwenye Kariakoo Dabi ilikuwa namna hii:-

DJIGUI DIARRA

Ateba na Diarra
Leonel Atebba mshambuliaji wa Simba akipambana na Diarra, Kariakoo Dabi. Source: Simba.

Kipa namba moja wa Yanga alikuwa kwenye ubora wake akicheza mchezo wa 5 mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa ndani ya dakika 450. Tukirudi kwenye Kariakoo Dabi alikomba dakika 90 na hakufungwa.

Hatari aliokoa zaidi ya mbili kubwa kuliko ni ile dakika ya 5 kutoka kwenye miguu ya Leonel Ateba wa Simba, dakika ya 44, 55, 55, 73. Mguu wenye nguvu ni ule wa kulia alitoa pasi zaidi ya 8 ambazo ziliwafikia walengwa na mguu wa kushoto alitoa pasi zaidi ya tatu.

YAO

Yao alichezewa faulo dakika ya 15, alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 41 na alikomba dakika zote 90.

LADACK BOCCA

Beki mwenye spidi uwanjani alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 38 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 26, alichezewa faulo dakika ya 28, 45 alicheza faulo dakika ya 37 alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ramadhan Kayoko.

JOB

Dickson Job beki wa kazikazi alikomba dakika 90 aliokoa hatari dakika ya 45 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 46.

BACCA

Bacca na Ateba
Bacca na Ateba Uwanja wa Mkapa kwenye Kariakoo Dabi, Oktoba 19 2024. Source: Yanga.

Ibrahim Bacca alikuwa na vita yake na mshambuliaji Leonal Ateba ni dakika ya 54 alionyeshwa kadi ya njano alikomba dakika zote 90 licha ya kumpisha Jonas Mkude katika dakika zile 7 za nyongeza.

AUCHO

Khalid Aucho kiungo wa kati alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 78 alicheza faulo pia dakika ya 62 na alikomba dakika zote 90.

MAXI

Maxi na Baleke
Maxi Nzengeli akishangilia bao baada ya kufunga dakika ya 86 Uwanja wa Mkapa, Kariakoo Dabi.Source: Yanga.

Maxi Nzengeli alikuwa na code za Mnyama alikomba dakika 90 alifunga bao dakika ya 86, alipiga kona dakika ya 69 na alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 22.

MUDATHIR YAHYA

Mudathir Yahya alicheza faulo dakika ya 30, 71 alichezewa faulo dakika ya 27, 31, 44 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 78 alikomba dakika 90 licha ya kumpisha Nondo katika dakika 7 za nyongeza.

PRINCE DUBE

Prince Dube alichezewa faulo dakika ya 51, alicheza faulo dakika ya 3, 34, 45 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 24 alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 56 alikomba dakika 61 nafasi yake ilichukuliwa na Clement Mzize.

AZIZ KI

Aziz KI V Chemalone
Aziz KI V Chemalone kwenye Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa, Oktoba 19 2024. Source: Yanga.

Kiungo Aziz Ki, alichezewa faulo dakika ya 12, 20, 23 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 11 alipiga kona dakika ya 28, alicheza faulo dakika ya 43, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 59 alikomba dakika 84 nafasi yake ikachukuliwa na Clatous Chama aliyepiga faulo dakika ya 86.

PACOME

Kiungo Pacome alikomba dakika 62 nafasi yake ilichukuliwa na Kennedy Musonda. Pacome alicheza faulo dakika ya 34, alichezewa faulo dakika ya 17 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 41.

 

MECHI ZIJAZO ZA YANGA KWENYE LIGI

Baada ya ushindi wa Yanga kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi kuna mechi za ligi ambazo zinafuata kwa timu hiyo inayodhaminiwa na SportPesa. Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa watetezi walitwaa taji hilo msimu wa 2023/24 baada ya kukamilisha ligi wakiwa na pointi 80 walipocheza jumla ya mechi 30 uwanjani.

JKT Tanzania watakaribishwa na Yanga mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Oktoba 22 Uwanja wa Azam Complex.
Coastal Union watawakaribisha Yanga itakuwa ni Oktoba 26 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kete ijayo ya funga kazi ndani ya Oktoba itakuwa dhidi ya Singida Black Stars, Oktoba 30 Uwanja wa New Amaan.

NENO LA SEMAJI

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa malengo makubwa ni kuona wanapata matokeo kwenye mechi ambazo wanacheza na wanatambua kazi ni kubwa kila mchezo kutokana na ushindani uliopo.

“Kazi ni kubwa kwenye mechi ambazo tunacheza na tunatambua kwamba mchezo ni mgumu, uzuri ni kwamba wachezaji wanatambua ambacho tunahitaji kwenye mechi zetu zote zilizobaki, pongezi kwa wachezaji namna ambavyo walijituma mwanzo mwisho kutafuta matokeo.

“Tunamshukuru Mungu kwa matokeo ambayo tumeyapata bado tunaendelea kufanya kazi kwenye mechi zetu zote mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani kila kitu kinawezekana kutokana na uwezo wa wachezaji tulionao.”

Share this: