Jordan vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026Riyad Mahrez
  • Pambano kali Kundi J, Jordan vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026 kupigwa Juni 23,2026.
  • Muda wa wababe hawa wawili kukutana Uwanja wa Levi’s kati ya Jordan vs Algeria ni saa 12:00 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki
  • SportPesa Blog tumekuletea odds, uchambuzi na rekodi muhimu kuelekea mchezo huu muhimu

Jordan vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026 ni mchezo unaofuata Kundi J. Timu zote bado hazijapata pointi baada ya kupoteza mechi zao za kwanza zinakutana katika pambano kali lenye ulazima kushinda.Uwanja wa Levi’s Stadium, San Francisco, utachezwa siku ya Jumanne, 23 Juni 2026 saa 12:00 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Jordan walipoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Austria, Algeria wakichapwa 3-0 na Argentina.

Ratiba ya mechi zote Kombe la Dunia 2026 hii hapa:Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mecchi za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Jordan vs Algeria, angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa uwajibikaji.

Jordan
Jordan vs Algeria

Jordan vs Algeria, maelezo ya mechi

Jordan vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026
Al-Taamari
KipengeleMaelezo
MashindanoKombe la Dunia la FIFA 2026 — Kundi J, Mechi ya Pili
Tarehe na muda wa kuanzaJumanne, tarehe 23 Juni 2026 saa 12:00 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)
UwanjaLevi’s Stadium, Santa Clara (eneo la San Francisco Bay), California, Marekani
Msimamo wa Kundi JBaada ya mechi za kwanza: Argentina pointi 3, Austria pointi 3, Jordan pointi 0, Algeria pointi 0
Kilicho hatariniTimu itakayopoteza itakuwa katika hatari kubwa ya kuaga mashindano. Jordan na Algeria zinahitaji ushindi ili kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu.
Jukwaa la kubashiriSportPesa

Jordan vs Algeria taarifa muhimu

Jordan wanashiriki fainali za Kombe la Dunia la FIFA kwa mara ya kwanza katika historia yao. Ingawa walipoteza mabao 3-1 dhidi ya Austria katika mechi ya kwanza, matokeo hayo hayakuonyesha kuwa ni timu isiyo na uwezo. Bao la Ali Olwan liliwapa matumaini, huku ubunifu wa Musa Al-Taamari ukionyesha kuwa Jordan wanaweza kuzisumbua safu za ulinzi.

Changamoto kubwa ipo kwenye safu ya ulinzi. Kuruhusu mabao matatu dhidi ya Austria kulidhihirisha mapungufu ambayo viungo kama Ali Olwan na Noor Al-Rawabdeh watalazimika kusaidia kuyarekebisha kwa kufanya kazi kubwa zaidi ya kujilinda. Kocha Ali Barakeh atahitaji maboresho makubwa ya kiulinzi ikiwa Jordan wanataka kuepuka kipigo cha pili mfululizo.

Algeria, kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Argentina hakikushangaza kutokana na ubora wa wapinzani wao. Kilichotia wasiwasi zaidi kwa kikosi cha kocha Vladimir Petkovic ni namna walivyofungwa. Udhaifu wa safu yao ya ulinzi ulionekana wazi dhidi ya kasi na mabadiliko  ya Argentina.

Licha ya matokeo hayo, Algeria wana uzoefu mkubwa zaidi kuliko Jordan. Kikosi chao kinaundwa na wachezaji wanaocheza katika ligi kubwa za Ulaya, huku safari yao ya kufuzu Kombe la Dunia ikiwa ya kuvutia.

Riyad Mahrez, mmoja wa wachezaji wenye ufundi mkubwa zaidi kwenye mashindano haya, anaongoza safu ya ubunifu pamoja na Fares Chaibi na Ibrahim Maza katika eneo la kiungo cha ushambuliaji. Mohamed Amoura anaongoza safu ya ushambuliaji kwa kasi na uwezo wake wa kupenya.

Katika safu ya ulinzi, Ramy Bensebaini na Aïssa Mandi wanaleta uzoefu mkubwa, huku Rayan Aït-Nouri akiongeza nguvu ya kushambulia kupitia beki ya kushoto. Golini, macho mengi yatakuwa kwa Luca Zidane, mtoto wa gwiji wa soka Zinedine Zidane, ambaye anatarajiwa kuanza kama kipa wa kwanza.

Algeria pia walionyesha ubora wao katika mechi za kirafiki kabla ya mashindano haya kwa kuzifunga Uholanzi na Bolivia. Matokeo hayo yalithibitisha uwezo wa kikosi hiki kinapokuwa katika kiwango chake bora. Kwa kuwa hatima ya kufuzu ipo mikononi mwao.

Jordah vs Algeria h2h

TareheMashindanoMechiMatokeo
14 Julai 1988Kombe la Mataifa ya KiarabuJordan vs. Algeria2–1
30 Mei 2004Mechi ya KirafikiAlgeria vs. Jordan1–1
Septemba 1974Kuneitra CupAlgeria vs. Jordan6–0

Jordan vs Algeria taarifa za majeraha na watakaokosekana

Jordan

Hakuna majeraha yaliyoripotiwa. Inatarajiwa kutumia kikosi kilekile.

  • Mshambuliaji mkuu wa ubunifu: Musa Al-Taamari
  • Fowadi: Ali Olwan anaongoza safu ya ushambuliaji
  • Kiungo: Al-Rawabdeh na Sadeh katikati ya uwanja
  • Mpango: 4-4-2
  • Kikosi kinachotarajiwa: hakijabadilika kutoka mchezo uliopita

Algeria

Hakuna majeraha yaliyothibitishwa.

  • Tishio kubwa la ubunifu: Riyad Mahrez (upande wa kulia)
  • Fowadi: Mohamed Amoura anaongoza mashambulizi
  • Ulinzi: Ramy Bensebaini na Aïssa Mandi wanatoa uzoefu na uimara
  • Kipa: Luca Zidane
  • Mpango: 4-3-3

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza

Hivi vikosi si rasmi ni utabiri. Vikosi rasmi vitatolewa saa moja kabla ya mchezo.

Jordan (4-4-2)

  • Abulaila (GK)
  • Al-Arab (RB)
  • Haddad (CB)
  • Nasib (CB)
  • Abualnadi (LB)
  • Al-Rawabdeh (RM)
  • Ayed (CM)
  • Sadeh (CM)
  • Al-Taamari (LM)
  • Olwan (ST)
  • Abu Zrayq (ST)

 Algeria (4-3-3)

  • L. Zidane (GK)
  • Ait-Nouri (RB)
  • Mandi (CB)
  • Bensebaini (CB)
  • Belghali (LB)
  • Maza (DM)
  • Zerrouki (CM)
  • Chaibi (CM)
  • Mahrez (RW)
  • Amoura (ST)
  • Gouiri (LW)

Jordan vs Algeria takwimu muhimu

  • Jordan ni mara ya kwanza kabisa kucheza Kombe la Dunia
  • Walipoteza 3-1 dhidi ya Austria kwenye mchezo wa kwanza wa kundi
  • Ali Olwan alifunga bao la kwanza la Jordan kwenye historia ya Kombe la Dunia
  • Fomu ya Jordan: L L D D D
  •  Algeria walipoteza 3-0 dhidi ya Argentina
  • Fomu ya Algeria: L W D W W
  • Riyad Mahrez ndiye kiungo muhimu wa ubunifu
  • Mohamed Amoura anaongoza mashambulizi kwa kasi na mipira ya haraka

Mtazamo wa mchezo

Algeria wanaonekana kuwa na ubora zaidi wa kikosi na uzoefu wa kimataifa, hivyo wanachukuliwa kuwa wana nafasi kubwa zaidi ya kushinda. Hata hivyo, Jordan si timu ya kudharauliwa wameonyesha uwezo wa kufunga mabao, hasa kupitia Olwan na ubunifu wa Al-Taamari.Jordan watahitaji kutumia mashambulizi ya kushitukiza, wakati Algeria wataegemea kasi ya Amoura na ubunifu wa Mahrez.

Jordan vs Algeria Prediction

Kwa mujibu wa Opta Analyst Algeria anapewa asilimia kubwa kushinda. Ni asilimia 59.1 huku Jordan akiwa na asilimia 18.4. Jordan 1-2 Algeria huu ni ubashiri wa uhariri. Haya sio matokeo rasmi.

Jinsi ya kubeti kwenye SportPesa

Jordan
Jordan vs Algeria
  1. Fungua ukurasa wa mchezo
    Nenda kwenye ukurasa wa mechi ya Jordan vs Algeria kwenye SportPesa .
  2. Chagua aina ya bet
    • Single Bet (SB): Kubeti mchezo mmoja tu
    • Multi-Bet (MB): Kuchanganya mechi zaidi ya moja kwenye tiketi moja
    • Live Bet (LB): Kubeti wakati mchezo unaendelea (baada ya kuanza)
  3. Weka dau lako
    Ingiza kiasi cha pesa unachotaka kubeti.
  4. Thibitisha bet
    Bonyeza kuweka bet yako na usubiri matokeo ya mchezo.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQ)

Jordan vs Algeria itaanza saa ngapi?

Mchezo utaanza saa 12:00 alfajiri EAT (Jumanne, 23 Juni 2026) Uwanja wa Levi’s Stadium, Santa Clara (San Francisco Bay Area), Marekani.

Nini kilitokea kwenye mchezo wa kwanza wa Jordan?

Jordan ilipoteza 3-1 dhidi ya Austria kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kundi J.

  • Hii ilikuwa mechi yao ya kwanza kabisa kwenye historia ya Kombe la Dunia
  • Ali Olwan alifunga bao la kwanza la Jordan kwenye mashindano hayo

Nini kilitokea kwenye mchezo wa kwanza wa Algeria?

Algeria ilipoteza 3-0 dhidi ya Argentina.

  • Licha ya kupoteza kwa mabao mengi, kocha wao bado anaamini timu ina uwezo wa kusonga mbele
  • Udhaifu mkubwa ulikuwa kwenye ulinzi

Jordan na Algeria wako kundi gani?

Zote ziko kwenye Kundi J (Group J) pamoja na Argentina na Austria.

  • Argentina na Austria: pointi 3 kila moja
  • Jordan na Algeria: pointi 0 kila moja

Luca Zidane ni nani?

Luca Zidane ni kipa wa Algeria na ni mtoto wa gwiji wa soka Zinedine Zidane. Anaanza kwenye lango la Algeria katika mashindano haya.

 Wachezaji muhimu wa Algeria ni akina nani?

  • Riyad Mahrez: Mchezaji mkuu wa ubunifu upande wa kulia
  • Mohamed Amoura: Fowadi wa kasi na mashambulizi ya moja kwa moja
  • Fares Chaibi & Ibrahim Maza: Wanaosaidia katika nafasi za juu kiungo

Utabiri wa mechi ya mabingwa watetezi huu hapa usome: Argentina vs Austria Kombe la Dunia 2026: prediction, Live score, lineups, vikosi, h2h, live score, odds

Wapi kwa kutazama (How to watch) Jordan vs Algeria

Mashabiki wanaweza kufuatilia Jordan vs Algeria kupitia watangazaji rasmi wa FIFA World Cup 2026 katika nchi zao. Kwa Tanzania, angalia ratiba ya matangazo ya washirika rasmi wa FIFA, na fuatilia SportPesa Blog kwa live score, matokeo, highlights na taarifa za mchezo.

Share this: