Pacome tenaPacome tena

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Oktoba 22 2024 walikomba pointi tatu mbele ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa sita kwa timu hiyo kushinda.

Ikumbukwe kwamba Yanga inadhaminiwa na SportPesa ilitoka kupata ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba kwenye Kariakoo Dabi kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-1 Yanga bao likifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 86.

Hapa tunakuletea rekodi za miamba wa timu zote mbili kwa namna walivyofanya kazi ndani ya uwanja kwenye msako wa pointi tatu ilikuwa namna hii:-

DJIGUI DIARRA

Diarra
Diarra Djigui kipa namba moja wa Yanga msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

Kipa namba moja wa Yanga mchezo wake wa sita mfululizo ambazo ni dakika 540 amekaa langoni bila kufungwa. Mbele ya JKT Tanzania alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90 na mwamuzi Ahmed Arajiga.

CLATOUS CHAMA

Chama v Kichuya
Chama Clatous kiungo wa Yanga akiwa kwenye majukumu yake dhidi ya JKT Tanzania. Source: Yanga.

Kiungo wa Yanga alianza kikosi cha kwanza na alifunga bao moja kwa pigo huru dakika ya 43, alitoa pasi ya bao dakika ya 23 alichezewa faulo dakika ya 79 alikomba dakika 72 nafasi yake ilichukuliwa na Jean Baleke.

BAKARI NONDO

Nahodha wa Yanga, Bakari Nondo alianza kikosi cha kwamba mbele ya JKT Tanzania na aliokoa hatari dakika ya 15 alishuhudia wakisepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo huo.

SURE BOY

Nyota huyu alikomba dakika 90, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 59, aliokoa hatari dakikaya 15, alichezewa faulo dakika ya 37, alicheza faulo dakika ya 53.

ANDAMBWILE AZIZ

Alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 90 alicheza faulo dakikaya 21.

PACOME

Pacome
Pacome, Max, Duke kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Azam Complex. Source: Yanga.

Pacome alikomba dakika 90 alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Alifunga bao lake la kwanza kwenye msimu ndani ya ligi dakika ya 23 akiwa ndani ya 18 na alisababisha faulo iliyoleta bao dakika ya 43.

Alipiga kona dakika ya 45 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 57.

MAXI NZENGELI

Kinara wa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga, Maxi Nzengeli akiwa na mabao manne alianza kikosi cha kwanza na hakukomba dakika zote 90 nafasi yake ilichukuliwa na Mudathir Yahya ilikuwa dakika ya 55.

Maxi alichezewa faulo dakika ya 34 na Muda aliyeingia alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 59, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 63.

KIBABAGE

Nickson Kibabage beki wa kupanda na kushuka alianza kikosi cha kwanza na alichezewa faulo dakika 45.

DICKSON JOB

Beki wa kazikazi alianza kikosi cha kwanza alichezewa faulo dakika ya 50 alikomba dakika 72 nafasi yake ilichukuliwa na Yao Yao.

MZIZE

Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 55 nafasi yake ikachukuliwa na Aziz Ki.

DUKE ABUYA

Duke Abuya alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 86 nafasi yake ilichukuliwa na Dennis Nkane.

HAWA HAPA JKT TANZANIA

DENNIS RICHARD

Kipa namba moja wa JKT Tanzania, Dennis Richard alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 15 alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi Ahmed Arajiga dakika ya 39 kwa kitendo kilichotafsiriwa kuwa alidaka mpira nje ya eneo la 18.

Nafasi yake ilichukuliwa na Gonzo dakika ya 42 alitunguliwa bao moja na Clatous Chama la pigo la faulo dakika ya 43. Aliokoa hatari dakika ya 49, 59, 64.

DAVID BRYSON

Mwamba huyu alikomba dakika 90 alichezewa faulo dakika ya 34.

JOHN BOCCO

Legend John Bocco alikomba dakika 45 za mwanzo nafasi yake ilichukuliwa na Edward Songo. Ikumbukwe kwamba Shiza Kichuya naye alianza kwenye mchezo huo lakini hakukomba dakika 90.

Mudathir v JKT Tanzania
Nyota wa Yanga Mudathir kwenye kazi na staa wa JKT Tanzania. Source: Yanga.

MAKA EDWARD

Alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 52 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

ISMAIL AZIZ

Kiungo huyu alianza kikosi cha kwanza na alichezewa faulo dakika ya 53.

HUYU HAPA GAMONDI

Gamondi amebainisha kuwa kazi kubwa ilifanyika kwa wachezaji kwenye mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania jambo ambalo linapaswa kuwa endelevu kwa kuwa wanahitaji pointi tatu katika mechi wanazocheza.

“Katika mechi ambazo tunacheza kitu cha msingi ni kuona kwamba tunapata pointi tatu hilo ni jambo la msingi hivyo ninawapongeza wachezaji kwa kufanya kazi nzuri kutafuta ushindi.”

Share this: