Usajili mpya Yanga SC balaa: Ali Kamwe atangaza mashine mbili mpya, namba 6 yatikisa, je ni Feisal?

ByJoel Thomas

July 29, 2026
Usajili mpya Yanga SCUsajili mpya Yanga SCUsajili mpya Yanga SC
  • Usajili mpya Yanga SC umeendelea kuwa mjadala mkubwa wa medani ya soka ndani na nje ya Tanzania.
  • Mpaka sasa Yanga SC imesajili mastaa wapya 10 ambao ni; Juma Abushiri, Hussein Mihambo, Abdulnasir Muhamed, Mohamed Mussa, Erick Mwijage, Suleiman Mbarouk, Ibrahima Toure, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, na Peter Shalulile.
  • Baada ya kukamilisha sajili hizo, kama ulidhani Yanga SC wamemaliza basi hapana, uongozi wa timu hiyo kupitia kwa semaji, Ali Kamwe umesema utawatangaza mastaa wapya 2.
  • Taarifa zinaihusisha Yanga SC kwa ukaribu na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’. Makala hii inachambua kwa ufupi usajili mpya wa Yanga SC 2026/27.

Zimebaki siku 15 tu, kuelekea kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27, ambapo timu mbalimbali zinapambana kufanya usajili mzito. Miongoni mwa timu ambazo zimefanya usajili mkubwa ni mabingwa watetezi Yanga SC. Mpaka sasa timu hiyo imekamilisha usajili wa wachezaji 10 ambao ni; Juma Abushiri, Hussein Mihambo, Abdulnasir Muhamed, Mohamed Mussa, Erick Mwijage, Suleiman Mbarouk, Ibrahima Toure, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, na Peter Shalulile. Uongozi wat imu hiyo kupitia kwa msemaji wake, Ali Kamwe umeweka wazi mashine nyingine 2 kutua huku tetesi zikimtaja Feisal Salum ‘Feitoto’.

Muhtasari Kuhusu usajili mpya Yanga SC 2026/27, Bilioni 15!

Peter Shalulile
Peter Shalulile

Akizungumzia usajili wao msimu huu, Ali Kamwe amesema: “Bajeti ya usajili msimu huu Rais wetu Eng. Hersi alimuita mfadhili wetu GSM kumuuliza msimu huu tunafanyaje kusajili wachezaji GSM akamjibu kuwa tafuta wachezaji pesa nitatoa.

“Ghalib Said Mohamed ameweka bajeti ya Bilioni 15 kusajili tu wachezaji na kuna mchezaji mmoja juzi alizungumza na GSM alimtaka, ila alirukaruka lakini tulitaka kumleta Yanga SC kwa jeuri ya hela aliyoweka mfadhili wetu.”

KUSOMA KUHUSU USAJILI MPYA WA YANGA SC, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC 2026/27 wachezaji wafanyiwa vipimo |SportPesa Blog

Kuhusu Kundi kubwa la washambuliaji

Erick Mwijage
Erick Mwijage

Akielezea kwanini timu yao ina Kundi kuwa la washambuliaji, Ali Kmawe amesema: “Msimu huu kuna mechi itafika tutaweka Mzize, Shalulile, Mwijage, Toure, Okello na tunashinda vizuri sana maana watu wanauliza Yanga Sc imesajili washambuliaji watachezaje? Sisi tumedhamiria kushinda tu, msimu huu na kuna siku mtanikumbuka maneno yangu.

KUMFAHAMU STRAIKA MPYA WA YANGA SC, TOURE SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC 2026/27: Cheikh Ibrahima Toure Straika mpya, rekodi zake balaa afunga mabao 105 mechi 243

Mashine 2 mpya kutua, je kuna Feisal Salum ‘Feitoto’

Usajili mpya Yanga SC
Usajili wa Namba –

Akizungumzia nyota ambao wanatarajiwa kutambulishwa Ali Kamwe amesema: “Usajili wa namba sita ndiyo usajili mkubwa tulioufanya msimu huu, tayari tumekamilisha kila kitu, kilichobaki ni siku ya utambulisho. Wanaomtaja Morice Chukwu nawaomba waondoe hofu siye tunayemzungumzia. Usajili wetu tayari umekamilika. Usajili tuliofanya msimu huu unaonyesha kiwango tulichojiwekea.

“Tumekusudia kufanya jambo kubwa na msimu huu hatukuja kutania. Feisal Salum ni mchezaji mzuri sana, lakini Yanga SC tumeshafunga usajili wetu wa ndani. Hakuna mazungumzo yoyote kati ya Yanga na Fei au Azam. Mashine mbili zilizobaki zote ni za kimataifa.”

Hitimisho

Toure akisaini Yanga SC
Toure akisaini Yanga SC

Usajili mpya Yanga SC unazidi kutikisa majukwaa ya Habari na vijiwe vya soka hapa nchini. Huku wakiwa wamekamilisha usajili wa nyota 10 wapya, ni wazi inaonyesha kuwa uongozi wat imu hiyo umepania kufanya makubwa kwa msimu mpya wa 2026/27. Ili kupata uwiano wa ushindani msimu ujao, ni wazi kuwa timu wapinzani wa Yanga wana kazi kubwa ya kufanya. Endelea kufuatilia SportPesa blog kwa taarifa mbalimbali za usajili.

KUFAHAMU WASIFU WA WINGA MPYA WA YANGA KANGWANDA, SOMA HII: Albert Kangwanda mchezaji mpya wa Yanga SC, takwimu na timu ambazo amecheza | SportPesa Blog

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.