- Kazi imeanza usajili mpya Yanga SC 2026/27 huu hapa, wachezaji wafanyiwa vipimo kurejea kambini
- Watotot wa Jangwani wametambulisha nyota wapya akiwemo Mohamed Mussa, Chuga Boy, Mihambo
- Benchi la ufundi limefanyiwa maboresho mtaalamu wa mapigo huru Kagisho Dikgacoi raia wa Afrika Kusini mchezaji wa zamani wa Fulham
Ni usajili mpya Yanga SC 2026/27 ikiwa ni maandalizi kwa mabingwa watetezi kurejea NBC Premier League, CAF Champions League. Tayari imetambulisha wachezaji wapya watatu ikiwa chini ya Kocha Mkuu Manqoba Mngqithi raia wa Afrika Kusini. Mrithi huyu wa mikoba ya Pedro Goncalves alitambulishwa Julai 10,2026.
Ijue ratiba ya Yanga SC: Ratiba ya Yanga SC NBC Premier League 2026/27 mechi 10 zamoto / Kariakoo Dabi Oktoba 10,2026
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Usajili mpya Yanga SC 2026/27, wachezaji wafanyiwa vipimo
Kumekucha usajili mpya Yanga SC 2026/27 baada ya dirisha la usajili kufunguliwa. Tayari wachezaji wamefanyiwa vipimo kamili kurejea kambini. Miongoni mwa wachezaji waliofanyiwa vipimo ni mlinda mlango Aboutwalib Mshery, Chuga Boy, Juma Abushir.
Mohamed Mussa
Nyota huyu ni mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC ambaye msimu uliopita alikuwa Kigoma. Alitambulishwa Jangwani rasmi Julai 21 anaitwa Mohamed Mussa ni beki alikuwa Mashujaa FC.
Juma Issa Abushir
Mchezaji wa kwanza kutambulishwa mitaa ya Jangwani ni beki chipukizi ambaye ni mzawa. Julai 18,2026 alitambulishwa Juma Issa Abushir huyu ni beki kutoka Fountain Gate maarufu kwa jina la Chuga Boy. Alianza maisha ya soka kwenye kituo cha Future Stars kilichopo Arusha akiwa na miaka 6 tu.
Mihambo
Mali nyingine mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC ni mshambuliaji wa kazi. Anaitwa Hussen Mihambo aliyekuwa akicheza Mashujaa FC. Ni Julai 20,2026 alitambulishwa Jangwani kuwa ingizo jipya.
Abdulnasir Muhamed
Beki wa kulia Abdulnasir Muhamed aliyekuwa Mashujaa FC naye ni kijani na njano. Alitambulishwa Julai 20,2026 kuwa mtaa wa Kariakoo.Ni kandarasi ya miaka miwili inaelezwa kuwa amesaini.
Benchi la ufundi
Wasifu wa kocha mpya Yanga SC: Kocha mpya Yanga SC 2026/27 CV yake hii hapa kazi inaanza upya | SportPesa Blog
Mbali na Yanga SC kufanya maboresho kwenye eneo la wachezaji wamefanya maboresho katika benchi la ufundi. Ni Manqoba Mngqithi raia wa Afrika Kusini amepewa majukumu kuwa kocha mkuu. Wamemtambulisha kocha msaidizi na mchambuzi wa mechi.
Simo Dladla
Ni kocha msaidizi alitambulishwa Julai 21, 2026 Simo Dladla raia wa Afrika Kusini. Kocha huyu ana uzoefu kwenye masuala ya ufundi ambapo 2020/21 alikuwa Kocha Mkuu Richard Bay, 2021/22 alikuwa kocha msaidizi Maroka Swallows, 2022/23alikuwa Kocha Mkuu Uthonghath FC, 2023/25 alikuwa Kocha Mkuu, Maritzburg Utd na 2025/26 alikuwa kocha msaidizi Golden Arrows.
Kagisho Dikgacoi
Eneo jingine ambalo wamefanyia maboresho ni sehemu ya mapigo huru. Yanga SC wamemtambulisha mtaalamu wa set piece anaitwa Kagisho Dikgacoi. Kocha huyu alitambulishwa Julai 21,2026. Huyu ni mchezaji wa zamani wa Fulham FC 2008/11, Crystal Palace 2012/14 na Cardiff City 20214/16. Raia huyu wa Afrika Kusini alicheza Kombe la Dunia 2010. AFCON 2008/13 na Europa League Final 2010 akiwa na Fulham.
Yardaan Valodia
Mchambuzi wa mbinu Yardaan Valodia alitambulishwa Julai 21,2026 Yanga SC alifanya kazi na Memolodi Sundown, Moroka Swallow, Golden Arrows. Mtaalamu huyu amepata mafunzo FC Barcelona na leseni ya CAF.
Greg Etafia
Kocha wa makipa Greg Etafia huyu ni kocha wa makipa ametambulishwa Julai 21,2026. Amefanikiwa kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria, Nigeria (Sydney Olympics 2000), AFCON 2004 nafasi ya 3 akiwa na timu ya taifa ya Nigeria.
Hitimisho
Tayari usajili mpya Yanga SC 2026/27 umeanza huku mashine mpya zikitambulishwa. Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano kutoka Jangwani amebainisha watafanya maboresho makubwa. Timu hiyo ina kibarua cha kutetea ubingwa 2026/27.



