- Simba SC 0-0 Jamus SC, Kagame Cup hali ni tete mechi mbili mfululizo hakuna ushindi wala kufunga bao
- Matokeo ya mechi ya hivi karibuni kwa Simba SC ilitoshana nguvu dhidi ya Mogadishu City
- Simba SC vs Singida Black Stars imeshikilia hatma ya timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali
- Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amewapa kazi Kelvin Nashon, Bakari Msimu, Ibrahim Doumbia
Huko Rwanda, Simba SC 0-0 Jamus SC ni matokeo rasmi ya mchezo wa hatua ya makundi katika kusaka hatua ya nusu fainali. Mnyama hali ni tete kutokana na matokeo tasa aliyopata mechi mbili mfululizo. Ni pointi mbili imevuna Simba SC katika hatua ya makundi ikilazimisha sare mechi ilizoshuka uwanjani. Ilifungua pazia kwa ubao kusoma Simba SC 0-0 Mogadishu City ya Somalia.
Huu hapa usajilimpya Simba SC: Mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 | Kelvin Nashon, Chilambo na Bakari Msimu kazi imeanza | SportPesa Blog
Bado hujashinda? Cheza na ushinde mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Ni Simba SC 0-0 Jamus SC Kagame Cup nchini Rwanda

Ubao umesoma Simba SC 0-0 Jamus SC Kagame Cup nchini Rwanda ikiwa ni mechi za kusaka tiketi kutinga hatua ya nusu fainali. Mchezo wa kwanza kwa kundi B ilitoshana nguvu na Mogadishu City. Ili Simba SC ifufue matumaini kutinga hatua ya nusu fainali inatakiwa kupata ushindi mchezo ujao dhidi ya Singida Black Stars.
Hata ikipata ushindi dhidi ya Singida Black Stars bado haitakuwa tiketi kamili kwa mnyama kutinga hatua ya nusu fainali. Hii inatokana na kundi B kuwa na pointi ambazo zinafanana. Jamus SC inaongoza kundi ikiwa na pointi 4 inafuatiwa na Singida Blac Stars yenye pointi 3 huku Simba SC ikiwa nafasi ya 3 na pointi 2, Mogadishu City inaburuza mkia ikiwa nafasi ya 4.
Ushindi pekee dhidi ya Singida Black Stars hauipi nafasi ya jumla kutinga hatua ya makundi kulingana na pointi ilizonazo. Italazimika kusubiri matokeo ya Jamus SC vs Mogadishu City. Hata hivyo bado matumaini yatakuwa hayajafikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na kundi kuwa gumu.
Huu ni wakati mgumu kwa Simba SC kwa sababu ikitokea imepata ushindi dhidi ya Singida Black Stars basi inabidi iombe Jamus SC ipate ushindi dhidi ya Mogadishu City. Bado matumaini yatakuwa kwa kuwa watakuwa wanasaka nafasi kufuzu kupitia timu iliyomaliza nafasi ya pili. Hesabu za hapa zinategemea matokeo ya Kundi A namna litakavyokuwa.
Ukitazama kundi A, Vipers wanaongoza kundi wakiwa na pointi 6, APR FC na Tusker FC hizi zinapambana kusaka nafasi ya kufuzu. Simba SC kwenye eneo la ushambuliaji haijawa imara ikicheza mechi mbili bila kufunga. Katika eneo la ulinzi imekuwa bora kwa kuwa haijaruhusu kufungwa.
Lineup ya Simba SC Kagame Cup
Simba SC 0-0 Mogadishu City, Julai 25,2026
Langoni
Hussen Abel
Mabeki
Duchu
Nathaniel Chilambo
Anthony Mligo
Vedastus
Viungo
Semfuko
Bakari Msimu
Kelvin Nashon
Inno Loemba
Cooper
Morice Abraham
Simba SC 0-0 Jamus SC, Julai 28,2026
Langoni
Hussen Abel
Mabeki
Duchu
Anthony Mligo
Vedastus
Shomari Kapombe
Viungo
Semfuko
Morice Abraham
Cooper
Inno
Clatous Chama
Oura.
Steve Barker katika mpango kazi

Soma kuhusu Simba SC kurejea kambini: Kikosi cha Simba SC kimerejea kambini rasmi | NBC Premier League na CRDB Federation Cup | SportPesa Blog
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker amekuwa akifanya mabadiliko ya mara kwa mara katika kikosi cha kwanza. Mchezo wa pili dhidi ya Jamus SC aliwaingiza wachezaji sita akiwemo Kalesto Makgalwa ambaye ni ingizo jipya. Ibrahim Doumbia huyu ni mshambuliaji mpya, Yusuph Kagoma ambaye ni kiungo mkabaji na Rushine ambaye ni beki.
Beki Nickson Kibabage na Libasse Gueye ni miongoni mwa wachezaji waliopata nafasi kwenye mchezo wa pili. Licha ya mabadiliko hayo bado hakukuwa na matokeo ya ushindi kwa timu hiyo. Ni mchezo mmoja umebaki kwa mnyama kukamilisha mechi za makundi itavaana na bingwa mtetezi Singida Black Stars iliyopata ushindi wa mabao 4-1 Mogadishu City, Julai 28,2026.
Hitimisho
Simba SC 0-0 Jamus SC matokeo ya mechi ya pili iliyokuwa imebeba matumaini kwa timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali. Mnyama yupo kazini ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2026/27. Wachezaji wapya waliosajiliwa wanaendelea na mazoezi makali huku kocha akiwapa nafasi kwenye mechi hizo za ushindani.

