- Mjue Albert Kangwanda mchezaji mpya wa Yanga SC Julai 24,2025 alitambulishwa rasmi kuwa njano na kijani.
- Ni MVP wa Zambia alifunga mabao 17 na asisti 9 ana miaka 27.
- SportPesa Blog tumekuletea takwimu za mchezaji na timu ambazo alicheza raia huyu wa Zambia.
Anaitwa Albert Kangwanda mchezaji mpya wa Yanga SC ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji, winga wa kushoto. Ana umri wa miaka 27 ni raia wa Zambia.Ni moja ya usajili ambao umetikisa kutokana na takwimu za mchezaji huyo ambaye anatajwa kuwa na nguvu akiwa uwanjani.
Usajili mpya Yanga SC: Usajili mpya Yanga SC 2026/27 wachezaji wafanyiwa vipimo |SportPesa Blog
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Mjue Albert Kangwanda mchezaji mpya wa Yanga SC 2026/27

Mjue kocha mpya Yanga SC: Kocha mpya Yanga SC 2026/27 CV yake hii hapa kazi inaanza upya | SportPesa Blog
Mabingwa watetezi wamemtambulisha Albert Kangwanda mchezaji mpya wa Yanga SC. Huyu ni MVP wa Zambia atakuwa ndani ya ardhi ya Tanzania. Msimu uliopita 2025/26alifunga mabao 17 na asisti 9 amesaini dili la miaka miwili. Miogoni mwa timu ambazo amecheza ni Al Hilal Omdurman ya Sudan, CSF Spartanii (Moldava), HNK Gorica, (Croatia) na Red Arrows ya Zambia. Julai 24 2026 alitambulishwa
| Msimu | Klabu | Maelezo |
|---|---|---|
| Kabla ya 2017 | Young Nkwazi | Akademi/maendeleo ya soka |
| 2017/2018 | Red Arrows (Zambia) | Alianza soka la kulipwa |
| 2019/2020 | Kafue Celtic (Zambia) | Uhamisho wa kudumu |
| 2020/2021 | Zanaco FC (Zambia) | Uhamisho wa kudumu |
| 2021/2022 | Kafue Celtic (Zambia) | Alirejea klabuni |
| 2022/2023 | HNK Gorica (Croatia) | Alisajiliwa lakini hakupata nafasi nyingi |
| 2022 | Hrvatski Dragovoljac (Croatia) | Alicheza kwa mkopo |
| 2023 | Red Arrows (Zambia) | Alirejea nchini Zambia |
| 2023–2025 | Al Hilal Omdurman (Sudan) | Uhamisho wa kudumu |
| 2024 | Red Arrows (Zambia) | Kwa mkopo kutoka Al Hilal |
| 2024/2025 | Spartanii Sportul (Moldova) | Kwa mkopo |
| 2025 | Red Arrows (Zambia) | Alirejea tena |
| 2026 | Yanga SC (Tanzania) | Amejiunga na Yanga SC |
Mazoezi yameanza wachezaji wa Yanga SC
Tayari Yanga SC wachezaji wameanza mazoezi ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2026/27. Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni Albert Kangwanda. Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mwasiliano Yanga SC amesema kila kitu kipo kwenye mipango makini.
“Tayari wachezaji wameanza mazoezi ikiwa ni maalumu kuelekea msimu mpya wa 2026/27. Program ambazo zinaendelea ni mazoezi ya viwanjani na mpango kazi kupitia video. Hii yote ni kuhakikisha kwamba tunakuwa imara kwa mwanzo wa msimu.
“Ushindani ni mkubwa hilo tunalitambua na tumefanya usajili mzuri. Kuna kiungo mpya anakuja huyu ni namba 6 ambaye atakuwa katika kikosi chetu. Mashabiki wake tayari kumpokea na kushuhudia ubora katika mechi za ushindani ambazo tutakuwa nazo,”.
MVP kuanza na Kariakoo Dabi
Mchezo wa ufunguzi kwa msimu wa 2026/27 ni Ngao ya Jamii ambao ni Kariakoo Dabi. Yanga SC ambao ni mabingwa wa NBC Premier League watavaana na mabingwa wa CRDB Federation Cup ambao ni Simba SC. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Agosti 12,2026.
Mwanzo wa mchezo huu ni ishara ya ufunguzi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Raia huyu wa Zambia anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi. Hivyo ataanza na mchezo mkubwa ambao unawakutanisha wababe hawa wawili katika ardhi ya Tanzania.
Albert atakuwa chini ya Kocha Mkuu Manqoba Mngqith ni raia wa Afrika Kusini ambaye tayari ameanza kuwapa mbinu za ushindi. Kocha naye ni mpya alitambulishwa mwanzo wa msimu kuwa Jangwani.
Hitimisho
Albert Kangwanda mchezaji mpya wa Yanga SC anatarajiwa kuwa miongoni mwa wale ambao watafanya makubwa msimu ujao. Huyu ni mrithi wa mikoba ya Prince Dube ambaye amerejea Zimbabwe. Julai 25,2026 aliwasili kwa mara ya kwanza katika mazoezi ya watoto wa Jangwani.

