Liverpool vs Manchester United: Mtihani wa kwanza wa Kocha Mauricio Pochettino EPL

Liverpool vs Manchester UnitedLiverpool vs Manchester UnitedLiverpool vs Manchester United

Liverpool vs Manchester United: Mtihani wa kwanza wa Kocha Mauricio Pochettino EPL

  • Ligi Kuu England yaani EPL inaendelea tena leo Jumapili 22/11/2026, huku mchezo mkubwa ukiwa ni Liverpool vs Manchester United.
  • Manchester United inaingia katika mchezo huo ikiwa na kocha mpya, Mauricio Pochettino baada ya kufukuzwa kwa kocha Michael Carrick.
  • Katika mechi 5 zilizopita kila timu imeshinda mechi 2 huku mchezo mmoja ukiisha kwa sare. Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa Mei 3, 2026 ambapo matokeo yalikuwa Manchester United 3-2 Liverpool.
  • Unaweza kufuatilia matokeo ya mchezo huu live kupitia SportPesascore.

Ligi Kuu England, EPL inaendelea tena leo Jumapili huku mchezo mkubwa ukiwa ni Liverpool vs Manchester United. Mechi hii inatarajiwa kupigwa Uwanja wa Anfield majira ya saa moja na nusu usiku. Mashetani wekundu wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kocha mpya, Mauricio Pochettino baada ya kufukuzwa kwa kocha Michael Carrick. Makala hii inachambua mambo muhimu kuhusu kocha Pochettino kwenye mchezo huu.

SOMA HII PIA: Liverpool vs Manchester United: Saa ya Mechi, H2H, Vikosi na Takwimu

Weka mkeka wako wa mechi hii ya Liverpool vs Manchester United, ushinde kupitia odds kubwa zilizoboreshwa za SportPesa kwa kugusa hapa chini.

Liverpool vs Manchester United
Liverpool vs Manchester United

Mchezo wa Kwanza Baada ya Kuondoka Marekani (USMNT)

Pochettino X Cunha X De Light
Pochettino X Cunha X De Light

Kocha, Mauricio Pochettino, amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu (hadi 2029), kuchukua nafasi ya Michael Carrick aliyefutwa kazi. Manchester United ililazimika kulipa takribani Pauni milioni 10, kuvunja mkataba wake na jopo lake la makocha kutoka timu ya taifa ya Marekani. Pochettino aliiongoza Marekani kuifunga Haiti Jumanne usiku (Novemba 17), na kusafiri usiku kucha kuwasili Manchester Jumatano, hivyo amekuwa na takriban nusu wiki tu, ya kufanya mazoezi na kikosi chake kipya kabla ya kuvaana na Liverpool.

Presha ya kuinusuru United kutoka eneo la kushuka Daraja

Hali ni mbaya kwa Manchester United kwenye msimamo, ambapo wanaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika nafasi ya hatari ya kushuka nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu. Ikiwa Manchester United watashinda mchezo huu, basi wanaweza kupanda hadi nafasi ya 16 na kupunguza presha. Ni wazi mchezo huu utakuwa mtihani mgumu zaidi kwake kuanza nao.

Unaweza kushinda mpaka Milioni 800 sasa, cheza kindege ‘Aviator’ cha SportPesa sasa gusa hapo chini

image
Win big with Sportpesa Aviator

Falsafa mpya na mbinu za mazoezi

Pochettino mazoezini
Pochettino mazoezini

Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari, Pochettino alisisitiza kuwa klabu hiyo haiwezi kuendelea kukwama kwenye yaliyopita, na kwamba anataka kujenga kitu kipya kuanzia mwanzo kulingana na falsafa yake. United imekuwa na takwimu mbaya zaidi za kukimbia uwanjani msimu huu. Changamoto ni kuwa kocha, Pochettino anajulikana kuhusudu soka la nguvu na utayari wa kimwili.

SOMA HII PIA: Manchester United: Ratiba, kikosi, usajili na matarajio msimu wa 2026/27

Hatima ya Bruno Fernandes

Licha ya, Bruno Fernandes kuwa na kiwango kisichoridhisha na mvutano wa mkataba, Pochettino alithibitisha kuwa kiungo huyo raia wa Ureno ataendelea kuwa nahodha wa timu na kumtaja kama mchezaji muhimu sana. Pochettino alitumia saa tatu siku ya Alhamisi, kuzungumza faraghani ofisini kwake na karibu wachezaji wote ili kuelewa hali zao ndani na nje ya uwanja. Hii ililenga kujaribu kuwajengea ari ya ushindi.

Hitimisho

Mechi zijazo za Pochettino
Mechi zijazo za Pochettino

Baada ya ratiba ya mchezo wa Liverpool vs Manchester United. Mchezo unaofuata United wanataerajiwa kusafiri mpaka Ureno kuvaana na Sporting CP (Novemba 25), kisha Brentford (Novemba 28), Newcastle (Desemba 2), na Coventry City (Desemba 5). Je, Mauricio Pochettino atafanikiwa kuvuna pointi ngapi? Endelea kufuatilia SportPesa blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.