- Usajili mpya Yanga SC 2026/27 unazidi kuteka mijadala ya vijiwe vya soka Tanzania.
- Tayari benchi jipya la ufundi la timu hiyo, chini ya kocha raia wa Afrika Kusini, Manqoba Mngqithi limeanza kazi ya kujiandaa na msimu mpya.
- Miongoni mwa Sajili ambazo zimekamilika na kutangazwa ni ya straika mpya Cheikh Toure mwenye uraia pacha wa Senegal na Ufaransa.
- Straika huyo ameandika rekodi bora ambapo wasifu wake unaonyesha amefunga mabao 105, kati ya mechi 243 alizocheza katika nchi mbalimbali.
Zimebaki siku chache kuelekea kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026/27, ambapo uongozi wa Yanga SC umeendelea kushusha vyuma kufanya maboresho ya kikosi chao. Miongoni mwa Sajili kubwa ambazo zimekamilika na kutangazwa ni ya straika wa kimataifa, Cheikh Ibrahima Toure ambaye ana uraia pacha wa Senegal na Ufaransa. Straika huyo anatajwa kuwa moto wa kuotea mbali, ambapo kupitia takwimu za mtandao wa Transfer market ambao unahifadhi rekodi mbalimbali za michezo. Toure ameweka rekodi kali ya kufunga mabao 105 katika mechi 243, na makala hii inachambua kwa ufupi.
Kuhusu usajili mpya Yanga SC 2026/27 na utambulisho wa Cheikh Toure

Toure amejiunga na Yanga SC, akisajiliwa kutoka kikosi cha timu ya Al-Jabalain FC inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Saudia. Kabla ya kutua Yanga SC Toure amewahi kupita kwenye timu mbalimbali zaidi ya 8 kutoka Ufaransa na Saudia. Nyota huyo ni miongoni mwa Nyota wapya 8 ambao wamekamilisha usajili wao mpaka sasa na kuendelea kutambulishwa.
KUSOMA ZAIDI KUHUSU USAJILI MPYA YANGA SC 2026/27, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC 2026/27 wachezaji wafanyiwa vipimo |SportPesa Blog
Taarifa binafsi za mchezaji
Jina : Cheikh Ibrahima Touré
Kuzaliwa: 22/09/1996 (Miaka 29)
Mahali: Kaolack, Senegal
Urefu: 1,87 m
Uraia: Ufaransa, Senegal
Nafasi: Straika wa Kati
Klabu: Yanga SC
Mguu: Anatumia kwa ufasaha miguu yote
KUMFAHAMU KOCHA MPYA YANGA SC, SOMA HII: Kocha mpya Yanga SC 2026/27 CV yake hii hapa kazi inaanza upya | SportPesa Blog
Source:
Mafanikio binafsi ya Toure na takwimu

Akiwa na jezi ya klabu mbalimbali, Toure ameandika rekodi ya kipekee akifanikiwa kufunga mabao 105 katika mechi 243 alizocheza. Toure pia ana uwezo wa kutengeneza mabao kwa wenzake uwanjani, ambapo rekodi zinaonyesha ametoa asisti 12 katika timu tofauti. Hii inamfanya straika huyo kuwa na uhusika wa jumla ya mabao 117 katika mechi 243.
KUHUSU REKODI ZA USAJILI YANGA SC, SOMA HII: Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajili Ecua afungua Agosti / Walioongeza mikataba/ Usajili
Hitimisho
Usajili mpya wa Yanga SC umekuwa Habari ya mjini katika dirisha hili kubwa la usajili, hasa baada ya kushuhudia wakiwa na namba kubwa ya mastaa waliofeli baada ya kusajiliwa msimu uliopita. Takwimu za Toure zinamtanabaisha kama miongoni mwa Nyota hatari. Jambo kubwa sasa ni swali je, Toure ataweza kuthibitisha uwezo wake akiwa na Yanga SC? Endelea kufuatilia SportPesa blog.

