Kazi inaendelea huku usajili wa Azam FC 2026/27 ukizidi kupamba moto kwa matajiri wa Dar. Haya yote ni maandalizi kuelekea msimu mpya unaotarajia kuanza Agosti 12,2026 kwa mchezo wa ufunguzi Ngao ya Jamii. Azam FC tayari wachezaji wamerejea kambini na kuna maingizo mapya akiwemo Caleb Ilese,Taiwo Abdulrafiu, kutoka Rivers United raia wa Nigeria.
Mafanikio ya Azam FC: Azam FC 2025: Mwongozo Kamili Kuhusu Kikosi, Benchi la Ufundi, na Urithi wa Klabu

Huu hapa usajili wa Azam FC 2026/27 wapya na walioongeza mkataba

Kuna usajili mpya wa Azam FC 2026/27 mara baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.Timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani haijapoa imerejea kambini. Hapa tunakuletea orodha ya wachezaji waliosajiliwa, kuongeza mkataba na Thank You namna hii:-
Sopu
Abdul Sopu bado yupoyupo ndani ya kikosi cha Azam FC. Kiungo huyu mshambuliaji alisajiliwa na matajiri hao akitokea Coastal Union ya Tanga. Aliongeza kandarasi kuendelea kuwa ndani ya kikosi cha Azam FC, Julai 24,2026.
Ilese
Caleb Ilese alitambulishwa ndani ya kikosi cha Azam FC rasmi Julai 24,2026. Huyu alikuwa akilelewa kwenye kituo cha Azam FC Academy ni raia wa DR Congo. Mchezaji huyu amepandishwa katika timu ya wakubwa.
Taiwo
Beki wa kushoto raia wa Nigeria, Taiwo Abdulrafiu ni mali ya Azam FC. Alikuwa anaitumikia Klabu ya Rivers United. Alitambulishwa Julai 23, 2026 ndani ya viunga vya Azam Complex.
Donovan Makoma
Huyu anaitwa Donovan Makoma ingizo jipya Azam FC. Ni raia wa Ufaransa ametambulishwa kuwa katika kikosi cha matajiri wa Dar kuelekea msimu mpya wa 2026/27. Kiungo huyu amesajiliwa akitokea Klabu ya Birkirkara ya Ligi Kuu Malta.
Mano
John Mano raia wa Sudan ni familia ya Azam FC. Alitambulishwa Julai 21,2026 akitokea Klabu ya Al Akhdar ya Libya. Ni dili la miaka miwili anatajwa kusaini.
Mubiru
Hassan Mubiru raia wa Uganda alitambulishwa katika kikosi cha matajiri wa Dar. Huyu ni ingizo jipya inatajwa amesaini dili la miaka miwili.Julai 20,2026 alitambulishwa.
Molia
Julai 18,2026, Henoc Molia alitabulishwa. Huyu ni winga kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo. Atakuwa kwenye changamoto mpya.
Lupini
Julai 17,2026, beki wa kati, Lupini Dieumerci, amejiunga na familia ya Azam FC akitokea AS Maniema.
Stanic
Julai 16,2026, Henri Stanic huyu ni beki wa kati. Mchezaji huyu alikuwa Klabu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini. Msimu mpya atakuwa viunga vya Azam Complex.
Kipre Jr
Ni Julai 15,2026, Kipre Jr alitambulishwa rasmi. Anaingia kwenye orodha kuwa nyota wa kwanza kutambulishwa kwa matajiri wa Dar. Alinunuliwa kutoka MC Alger ya Algeria anarejea kwa mara nyingine Azam FC.
Orodha ya wachezaji waliopewa Thank You

Mtasigwa
Adolf Mtasigwa alipewa Thank You rasmi Julai 25,2026. Huyu amepata changamoto mpya Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Chilambo
Nyota Nathaniel Chilambo beki wa kulia alikutana na Thank You rasmi Julai 25. Kwa sasa yupo kwenye changamoto mpya Simba SC.
Yoro Diaby
Alikutana na Thank You rasmi Julai 25. Yupo huru kujiunga na timu nyingine ambayo itahitaji huduma yake.
Muhsin Malima
Nyota huyu alikutana na Thank You Julai 25.Hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2025/26. Yupo huru kwa changamoto mpya nje ya Azam FC.
James Akamiko
Kiungo huyu mkabaji alikutana na Thank You Julai 25. Miongoni mwa viungo wakabaji waliokuwa katika ubora. Alikuwa anatajwa kupigiwa hesabu na Yanga SC.
Abel Abah
Nyota huyu Abel Abah alikutana na Thank You Julai 25,2026. Yupo huru kwa changamoto mpya msimu ujao.
Jean Ngita
Nyota huyu alikutana na Thank You Julai 26,2026.Moja ya wachezaji ambao hakuwa na nafasi mara kwa mara kikosi cha kwanza.
Jephte Kitambala
Alikutana na Thank You rasmi Julai 26,2026. Ana miaka 27 ni raia wa DR Congo. Huyu ni mshambuliaji ambaye hatakuwa katika viunga vya Azam FC.
Tepsi Evance
Kiungo mshambuliaji mwenye ujuzi mkubwa hatakuwa ndani ya kikosi cha Azam FC. Huyu ni mzawa ambaye.
Hitimisho
Usajili wa Azam FC 2026/27 ni mwanzo wa maandalizi ya msimu mpya. Timu hiyo tayari imerejea kambini katika viunga vya Azam Complex. Inatarajia kuelekea Rwanda, Kigali kwa kambi kabla ya kurejea Tanzania kwa mechi za ligi.

