Matokeo | Liverpool 4-0 Manchester United | EPL 2026/27 highlights, livescore, Ratiba, matokeo na taarifa za mechi

Liverpool --- Manchester UnitedLiverpool --- Manchester UnitedLiverpool --- Manchester United

Matokeo | Liverpool 4-0 Manchester United | EPL 2026/27 highlights, livescore, Ratiba, matokeo na taarifa za mechi

  • Mchezo mkubwa wa mashindano ya Ligi Kuu England EPL leo Jumapili, umetamatika huku matokeo ya Uwanja wa Anfield ukionyesha Liverpool 4-0 Manchester United.
  • Mechi hii ilikuwa ya kwanza kwa kocha, Mauricio Pochettino ndani ya kikosi cha Manchester United tangu alipotangazwa kuwa kocha mkuu mpya.
  • Matokeo haya yameipandisha Liverpool mpaka kwenye 4 bora huku Manchester United wakisalia eneo la kushuka daraja.
  • Makala hii inachambua kwea ufupi ‘highlights’ za mechi hii.

‘Big match’ ya Ligi Kuu England, EPL leo Jumapili, imetamatika huku matokeo ya Uwanja wa Anfield yakisomeka Liverpool 4-0 Manchester United. Mechi hii ilikuwa ya kwanza kwa kocha, Mauricio Pochettino ndani ya kikosi cha Manchester United tangu alipotangazwa kuwa kocha mkuu mpya. Matokeo haya yameipandisha Liverpool mpaka kwenye 4 bora, huku Manchester United wakisalia eneo la kushuka daraja.

SOMA HII PIA: Liverpool vs Manchester United: Saa ya Mechi, H2H, Vikosi na Takwimu

Kuhusu matokeo ya Liverpool 4-0 Manchester United

Matokeo kipindi cha -
Matokeo kipindi cha 2

Liverpool imeendeleza ubabe wake dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Manchester United, baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa dimba la Anfield, Jumapili, Novemba 22, 2026. Matokeo hayo yamekuwa pigo kubwa kwa Manchester United, ambayo ilikuwa ikicheza mchezo wake wa kwanza chini ya kocha mpya Mauricio Pochettino. Ni wazi Pochettino ameanza na mtihani mgumu wa kuiongoza klabu hiyo.

Shinda mpaka Milioni 800, cheza Kindege ‘Aviator’ sasa gusa hapa chini 

Tottenham Hotspur

Kipindi cha kwanza

Matokeo kipindi cha kwanza
Matokeo kipindi cha kwanza

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku Liverpool ikionyesha dhamira ya kutafuta ushindi mapema, dakika ya nane ndiyo iliyobadilisha kabisa mwelekeo wa pambano hilo. Hii ni baada ya beki wa Manchester United, Leny Yoro, kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Alexander Isak akiwa kama mchezaji wa mwisho kuzuia nafasi ya wazi ya kufunga bao. Liverpool ilitumia vyema faida ya kuwa na mchezaji mmoja zaidi uwanjani na kupata bao la kwanza dakika ya 10 kupitia Dominik Szoboszlai, aliyefumua shuti kali la mpira wa adhabu na kuuweka wavuni.

Dakika tatu baadaye, Florian Wirtz aliandika bao la pili kwa Liverpool kwa kumalizia kwa ustadi mkubwa krosi ya Rio Ngumoha. Hata hivyo, licha ya Manchester United kufanya jitihada za kujilinda na kuzuia mashambulizi ya Liverpool, wenyeji waliendelea kutawala mchezo na kutengeneza nafasi mbalimbali za kuongeza mabao lakini walishindwa kuzitumia.

Kipindi cha 2

Liverpool --- Manchester United
Liverpool  vs Manchester United

Kipindi cha pili kilianza kwa Liverpool kuendelea kushambulia huku mlinda mlango wa Manchester United, Senne Lammens, akifanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi ya wenyeji. Dakika ya 66, Rio Ngumoha aliandika bao la tatu baada ya kumalizia krosi ya Bradley Barcola, ambaye alifanya kazi nzuri upande wa kulia kabla ya kumpelekea mchezaji mwenzake mpira uliomuwezesha kufunga kwa mara nyingine. Bao la nne na la mwisho lilifungwa dakika ya 82 na mchezaji wa akiba Victor Munoz, aliyepokea pasi nzuri kutoka kwa Florian Wirtz.

Athari ya matokeo haya kwenye msimamo

Liverpool 4-0 Manchester United
Liverpool wakishangilia bao la Rio

Ushindi huo umeiwezesha Liverpool kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na tofauti ya pointi moja dhidi ya Manchester City iliyo nafasi ya tatuna nyuma ya vinara Arsenal kwa pointi saba. Kwa upande wa Manchester United, kipigo hicho kimeiacha klabu hiyo ikiendelea kukaa katika eneo la kushuka daraja. United iko na tofauti ya pointi moja pekee dhidi ya timu inayoshika nafasi ya mwisho.

Hitimisho

Matokeo ya Liverpool 4-0 Manchester United yanasalia kuwa mwanzo mbaya kwa kocha Pochettino. Kocha huyo amepewa jukumu kubwa la kurejesha ushindani na heshima ya Manchester United baada ya kipigo hicho kizito kutoka kwa mahasimu wao wakubwa.Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi za michezo na burudani.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.