Simba SC Ligi Kuu Bara 2026/27: Watikisa rekodi ya mabao mipira ya kutenga Table & Stats, Ratiba na matokeo
- Ligi Kuu Bara imerejea baada ya mapumziko ya kupisha ratiba ya mashindano ya kimataifa ya mashindano ya AFCON, na tumeshuhudia vita kali miongoni mwa timu shiriki.
- Mpaka sasa Simba SC ndiyo vinara wa msimamo na pointi zao 33, wakifuatiwa na Yanga SC wenye pointi 28, huku Azam FC wao wakiwa nafasi ya 3 na pointi 23.
- Mnyama anaonekana kuwa katika fomu nzuri, ambapo amrfanikiwa kuandika rekodi kadhaa, ikiwemo kuwa timu hatari kwenye mipira ya kutenga.
- Makala hii inachambua kwa ufupi rekodi ya timu zenye rekodi bora ya ufungaji mabao ya kutenga kwenye Ligi ya NBC 2026/27.
Simba SC Ligi Kuu Bara hawashikiki, baada ya mapumziko mafupi kupisha mechi za kufuzu AFCON wamerudi wamoto. Kwenye msimamo wa ligi Simba SC wanaendelea kukamatia usukani na pointi zao 33, wakifuatiwa na Yanga SC wenye pointi 28, huku Azam FC wao wakisalia na pointi 23. Simba pia ndiyo timu ambayo imeandika rekodia ya kufunga mabao mengi ya mipira ya kutenga kama inavyoelezewa hapa.
SOMA HII PIA: Uchaguzi Mkuu Simba SC: Mangungu achukua tena fomu, kushindana na wengine 6 yupo Kaburu, MO Soloka
Rekodi ya magoli ya mipira iliyokufa Simba SC Ligi Kuu Bara

Uwezo wa kutumia vyema mipira iliyokufa (Set Pieces) unaendelea kuwa moja ya silaha muhimu kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027. Simba SC ikionyesha ubora zaidi katika eneo hilo, kwa kuongoza orodha ya timu zilizofunga mabao mengi kupitia mipira iliyokufa. Kwa mujibu wa takwimu za Ligi Kuu ya NBC, kabla ya mechi za wikiendi iliyopita Simba SC ilikuwa inaongoza kuwa na idadi ya mabao mengi ya mipira ya kutenga wakifunga mabao 8. Hii inathibitisha hatati ya timu hiyo kwenye mipira ya kona, faulo na mipira mingine iliyosimama kupata mabao.
Polisi Tanzania nafasi ya 2

Klabu ya Polisi Tanzania inashika nafasi ya pili ikiwa na mabao sita, ikiendelea kuonyesha kuwa mipira iliyokufa ni sehemu muhimu ya mfumo wao wa ushambuliaji. Sehemu kubwa ya mabao hayo yakifungwa kwa m,ikwaju ya Penalti. Anuary Jabir ndiye kinara wa kucheza mipira hiyo.
SOMA HII PIA: Yanga SC Baada ya Ushindi Dhidi ya Polisi Tanzania: Uchambuzi wa Kikosi na Matarajio
Coastal Union nafasi ya 3, Pamba Jiji ya 4
Coastal Union na Pamba Jiji zinashika nafasi ya tatu na nne kila moja ikiwa imefunga mabao manne kupitia mipira iliyokufa. Hii inaonyesha ufanisi na ukuaji wa ubora wa ligi ya NBC katika misimu ya karibuni. Kwamba hata timu za daraja la kati zinaweza kushindana na timu kubwa na kuwapiku baadhi ya maeneo.
Unaweza kushinda mpaka Milioni 800, cheza kindege ‘Aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini
Yanga SC, Azam FC na Geita Gold mabao 3

Wanao maliza listi ya timu zenye mabao mengi ya kutenga ni timu za Azam, Geita Gold na Young Africans. Timu hizi zimefanikiwa kufunga mabao matatu kila moja. Hii inakamilisha orodha hiyo ya wakali wa mipira ya kutenga.
SOMA HII PIA: Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27: Simba SC, Yanga SC, Azam FC mmh! Table & Stats, Ratiba na matokeo
Hitimisho
Takwimu hizi zinaonyesha umuhimu wa maandalizi maalumu ya mipira iliyokufa katika soka la kisasa. Simba SC Ligi Kuu Bara msimu huu wamekuwa rekodi bora zaidi. Ikumbukwe ufanisi wa mipira ya kutenga unaweza kuzisaidia timu kupata matokeo kupitia mikakati ya kona na faulo, hata pale zinapokutana na ushindani mkali ndani ya mchezo. Endelea kufuatilia SportPesa blog kwa taarifa za rekodi mbalimbali msimu huu wa2026/27.


