Hispania vs Cape Verde FIFA Kombe la Dunia 2026, utabiri, h2h, taarifa ya timu | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

June 13, 2026
Hispania vs Cape Verde FIFA Kombe la Dunia 2026Spain vs Cape VerdeSpain vs Cape Verde

Timu ya taifa ya Hispania vs Cape Verde FIFA Kombe la Dunia 2026 mchezo unatarajiwa kuchezwa Juni 15, 2026. Miongoni mwa timu ambayo inapewa nafasi kutwaa taji hilo kubwa ni hizi Hispania. Hii ni kampeni inaanza kwenye mchezo dhidi ya Cape Verde, usiku wa Jumatatu, Uwanja wa Mercedes-Benz Stadium.

SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Hispania vs Cape Verde, angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa wajibu.

Spain
Hispania vs Cape Verde

Taarifa muhimu kuhusu Hispania vs Cape Verde FIFA Kombe la Dunia 2026

Hispania walitwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 2010. Hili ni taji lao pekee ambalo wanalo kwa sasa. Wanatarajiwa kuongoza Kundi H linaloundwa pia na Uruguay kutoka Amerika Kusini na Saudi Arabia ikiwa watapata ushindi.

Kwa mujibu wa viwango vya ubora vya FIFA, Hispania wanashika nafasi ya pili duniani, Cape Verde wapo nafasi ya 67. Mataifa hayo mawili yatakutana jijini Atlanta, wakati Saudi Arabia watacheza dhidi ya Uruguay saa 1:00 usiku jijini Miami.

Ni wazi safari ya Hispania awamu 3 zilizopita Kombe la Dunia hazikuwa bora. Walishindwa kuvuka hatua ya 16 bora katika awamu mbili za mashindano hayo. Aidha, kikosi kinachonolewa na kocha Luis de la Fuente kimefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee kati ya mechi 6 za mwisho walizocheza Kombe la Dunia.

Licha ya changamoto hizo katika michuano ya Kombe la Dunia, Hispania bado ni mabingwa watetezi wa Ulaya baada ya kutwaa ubingwa wa Euro. Ikumbukwe pia walimaliza washindi wa pili nyuma ya Ureno michuano ya UEFA Nations League 2025.

 Hispania vs Cape Verde FIFA Kombe la Dunia 2026
Yamal nyota wa Hispania.

SOMA HII: FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil | Mechi zote | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika | Je, Neymar Jr yuko tayari?

Cape Verde watatoboa mbele ya Hispania?

Cape Verde wanakibarua kikubwa kutoboa mbele ya Hispania katika mchezo huu, hasa ikizingatiwa kuwa wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao. Taifa hili kutoka Afrika lenye idadi ya watu inayokadiriwa kufikia laki sita linatumaini kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu hatua ya mtoano katika ushiriki wake wa kwanza tangu Ghana walipofanya hivyo mwaka 2006.

Cape Verde waliingia katika mashindano haya wakiwa katika kiwango kizuri baada ya kushinda mechi sita kati ya saba za mwisho za kufuzu. Hata hivyo, watalazimika kucheza kwa ubora wa hali ya juu ikiwa wanataka kuanza kwa matokeo mazuri jijini Atlanta.Ikiwa Cape Verde watashinda itakuwa ni rekodi ya kushtua dunia katika Kombe la Dunia 2026.

Utabiri wa Matokeo

Hispania wana ubora mkubwa wa kikosi, uzoefu wa mashindano makubwa na wachezaji wenye viwango vya juu. Cape Verde wanaweza kutoa upinzani mkali kutokana na morali yao na hamasa ya kushiriki kwa mara ya kwanza, lakini inaonekana vigumu kuizuia Hispania. Matokeo ya ushindi itakuwa Hispania 3-1 Cape Verde. Haya ni maoni na sio matokeo halisi hivyo beti kwa wajibu.

Hispania vs Cape Verde itachezwa muda gani?

Mchezo kati ya Hispania na Cape Verde umepangwa kuanza saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (E.A.T) katika Uwanja wa Mercedes-Benz Stadium jijini Atlanta. Pambano hilo ni sehemu ya michezo ya Kundi H ya Kombe la Dunia 2026.

Taarifa za kikosi cha Hispania

Hispania wanakabiliwa na wasiwasi wa majeraha kwa baadhi ya nyota wao muhimu kuelekea mchezo huu. Winga mahiri Lamine Yamal na Nico Williams walikosa mchezo wao wa mwisho wa maandalizi kabla ya kuanza kwa fainali hizo kutokana na changamoto za kiafya. Hata hivyo, wawili hao wanatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Saudi Arabia. Víctor Muñoz amerejea mazoezini hivi karibuni, lakini huenda akaanza mchezo huu akiwa benchi.

Katika safu ya ushambuliaji, Mikel Oyarzabal na Pedri walifunga mabao katika ushindi dhidi ya Peru wiki iliyopita na wanatarajiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza, wakimsaidia Ferran Torres, ambaye anatarajiwa kuongoza mashambulizi kama mshambuliaji pekee.

Golikipa David Raya anatarajiwa kupewa nafasi ya kuanza langoni, huku Unai Simón akianza kutoka benchi. Katika safu ya ulinzi, Pau Cubarsí pamoja na Aymeric Laporte wanatarajiwa kuwa nguzo muhimu za nyuma za La Roja.

Habari za kikosi cha Cape Verde

Kwa upande wa Cape Verde, mshambuliaji wa klabu ya Omonia Nicosia, Willy Semedo, anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji baada ya kufunga bao katika mchezo wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Bermuda. Wachezaji wengine wa Cape Verde wanatarajiwa kubaki wale wale walioanza katika kikosi kilichoifunga Bermuda wiki moja iliyopita.

Hispania vs Cape Verde: Rekodi za mikutano, fomu za sasa

Timu ya taifa ya Hispania, maarufu kama La Roja, inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na rekodi ya kutopoteza mechi 10 mfululizo katika mashindano yote. Hata hivyo, licha ya kutofungwa, Hispania imefanikiwa kushinda michezo miwili pekee kati ya mechi zao tano zilizopita, huku ikitoka sare mara tatu. Katika mchezo wao wa mwisho wa maandalizi kabla ya Kombe la Dunia 2026, Hispania waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Peru, matokeo yaliyowaongezea morali kuelekea pambano hili la ufunguzi.

Kwa upande mwingine, Cape Verde wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na hamasa kubwa baada ya kutafuta ushindi wa nne mfululizo. Kabla ya kuanza kwa fainali hizo, waliifunga Finland na Serbia, kabla ya kuhitimisha maandalizi yao kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Bermuda.

SOMA HII: Germany vs Curacao utabiri Kombe la Dunia 2026 | Kundi E

Fomu za Sasa

  • Hispania: W – D – D – W – D
    (Ushindi, Sare, Sare, Ushindi, Sare)
  • Cape Verde: W – W – W – L – L
    (Ushindi, Ushindi, Ushindi, Kichapo, Kichapo)

Rekodi ya Mikutano ya uso kwa uso

Mchezo huu utaweka historia kwa kuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Hispania na Cape Verde kukutana katika ngazi ya kimataifa. Kutokuwepo kwa rekodi ya awali kunafanya pambano hili kuwa gumu kutabiri kwa kuzingatia historia, huku kila timu ikitegemea kiwango chake cha sasa na maandalizi kuelekea mashindano haya.

Share this: