Iran vs New Zealand FIFA Kombe la Dunia 2026Iran
  • Mchezo mkali kati ya Iran vs New Zealand FIFA Kombe la Dunia 2026 unatarajiwa kuchezwa Juni 15, 2026.
  • Huu ni mchezo wa Kundi G, saa 1:00 usiku itakuwa kwa saa za Afrika Mashariki
  • SportPesa Blog tumekuletea takwimu za mchezo, H2H za wababe hawa na taarifa kuhusu vikosi

Timu ya taifa ya Iran vs New Zealand FIFA Kombe la Dunia 2026 zinatarajiwa kuanza kampeni kutafuta tiketi ya kutwaa taji hilo kubwa. Iran imeshiriki fainali za Kombe la Dunia mara 6, haijawahi kufuzu hatua ya mtoano. Mchezo huu wa Kundi G unatarajiwa kuchezwa Juni 15, 2026, Uwanja wa Los Angeles saa 1:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Ijue ratiba na muda wa mechi za FIFA Kombe la Dunia kwa kusoma hapa: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Iran vs New Zealand, angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa wajibu.

Iran
Iran vs New Zealand, FIFA Kombe la Dunia Odds zimeimarishwa

Taarifa muhimu ya Iran vs New Zealand FIFA Kombe la Dunia 2026

Kuelekea mchezo mkali wa Iran vs New Zealand FIFA Kombe la Dunia 2026 wachezaji wenye uzoefu wanapewa nafasi kuanza kikosi cha kwanza. Amir Ghalenoei Kocha Mkuu wa Iran ameijenga timu hiyo kwenye hali ya nidhamu na tahadhari zaidi. Mshambuliaji tegemeo ni Mehdi Taremi anayekipiga katika klabu ya Olympiacos aliyefunga magoli 5 katika mechi za hivi karibuni.

New Zealand, chini ya kocha M. Mayne, wanarejea kwenye Kombe la Dunia baada ya kusubiri kwa miaka 16. Ingawa wanaonekana kuwa wageni wasiokuwa na nafasi kubwa kwa mujibu wa wengi, hawakosi mpango wa kupambana. 2010 bado walimaliza hatua ya makundi bila kupoteza hata mchezo mmoja baada ya kutoka sare katika mechi zote tatu.

Utabiri

Iran wana uzoefu mkubwa na ubora wa wachezaji binafsi. Hata hivyo, New Zealand wameonyesha mara kadhaa kuwa wana uwezo wa kuwavuruga vigogo wanapocheza kwa nidhamu na kujituma. Kwenye kushinda Iran 2-0 New Zealand. Haya ni maoni matokeo rasmi yatajulikana baada ya mchezo,

Matokeo ya mechi 5 za mwisho za Iran

TareheMashindanoMpinzaniMatokeo
Machi 2026Mechi ya KirafikiCosta Rica🇮🇷 Iran 5-0 Costa Rica
Machi 2026Mechi ya KirafikiNigeria🇮🇷 Iran 1-2 Nigeria
Novemba 2025Kombe la Kimataifa la Al AinUzbekistan🇮🇷 Iran 0-0 Uzbekistan
Novemba 2025Kombe la Kimataifa la Al AinCape Verde🇮🇷 Iran 0-0 Cape Verde
Oktoba 2025Mechi ya KirafikiTanzania🇮🇷 Iran 2-0 Tanzania
 Iran vs New Zealand FIFA Kombe la Dunia 2026
Nyota wa New Zealand.

Itambue ratiba ya mechi za Argentina hapa: Ratiba ya Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mabingwa watetezi kikosi | Takwimu | SportPesa Blog

Matokeo ya mechi tano za mwisho za New Zealand

TareheMashindanoMpinzaniMatokeo
Machi 2026FIFA SeriesChile🇳🇿 New Zealand 4-1 Chile
Machi 2026FIFA SeriesFinland🇳🇿 New Zealand 0-2 Finland
Novemba 2025Mechi ya KirafikiEcuador🇳🇿 New Zealand 0-2 Ecuador
Novemba 2025Mechi ya KirafikiColombia🇳🇿 New Zealand 1-2 Colombia
Oktoba 2025Mechi ya KirafikiNorway🇳🇴 Norway 1-1 New Zealand 🇳🇿

Rekodi ya Iran dhidi ya New Zealand

Iran na New Zealand wamekutana mara mbili pekee katika historia yao. Hakuna hata mmoja kati ya michezo hiyo uliokuwa wa mashindano makubwa. Iran alipata ushindi mara moja na mchezo mwingine sare.

TareheMechiMatokeo
2003Iran vs New ZealandIran 3-0 New Zealand
1973Iran vs New ZealandIran 0-0 New Zealand

Habari za Kikosi cha Iran

Maandalizi ya Iran kuelekea Kombe la Dunia 2026 yameathiriwa na changamoto kubwa nje ya uwanja. Ligi kuu ya Iran ilisimamishwa kuanzia Machi 2026 kutokana na mzozo wa kikanda, hali iliyosababisha baadhi ya wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani kufika kambini bila kuwa katika kiwango bora cha ushindani.

Wachezaji hao wanatoka katika klabu kubwa za nchini humo kama Persepolis, Tractor na Esteghlal, huku klabu hizo zikitoa idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi cha taifa. Kutokuwa na mechi za ushindani kwa muda mrefu kunaweza kuathiri utimamu wa mchezo wa baadhi yao, ingawa bado haijulikani kwa kiwango gani hali hiyo itaonekana ndani ya dakika 90 za pambano.

Langoni, kipa mkongwe Alireza Beiranvand anatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza. Akiwa na uzoefu wa mechi 86 za kimataifa, Beiranvand atakuwa mmoja wa nguzo muhimu zaidi za Iran katika mchezo huu.

Habari za Kikosi cha New Zealand

Kwa upande wa New Zealand, macho mengi yataelekezwa kwa mshambuliaji wao nyota Chris Wood. Nahodha huyo alirejea uwanjani mwaka 2026 baada ya kupona tatizo la goti lililoathiri sehemu kubwa ya msimu wake akiwa na klabu ya Nottingham Forest. Ingawa anatarajiwa kuwa fiti kuanza mchezo huu, bado kuna maswali kuhusu kiwango chake cha utimamu wa mchezo na kama ataweza kucheza kwa kiwango chake bora mara moja.

Habari njema kwa New Zealand ni kwamba wachezaji wengine wote muhimu wanapatikana kwa ajili ya pambano hili. Wachezaji kama Liberato Cacace, Marko Stamenić na Elijah Just wanatarajiwa kuwa sehemu ya mhimili wa kikosi hicho chenye mchanganyiko wa uzoefu na ari ya kupambana.

Share this: