Simba SC vs Yanga SC | Taarifa mpya ya majeruhi; Oura, Kibabage na Kagoma, NBC Premier League, Ratiba, Uwanja, matokeo, msimamo na Takwimu | SportPesa Blog

ByJoel Thomas

May 1, 2026
Simba SC vs Yanga SCSimba SC vs Yanga SCSimba SC vs Yanga SC
  • Simba SC vs Yanga SC imebaki siku 1 tu, kiwake kuelekea mchezo huu mkali na maarufu kama Kariakoo Dabi.
  • Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), unatarajiwa kupigwa Jumapili 3/5/2026 Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
  • Hii ni mara ya 2 timu hizi kukutana wiki hii, mara baada ya Jumatano 29/4/2026 Simba SC kuibuka mabingwa wa Muungano Cup 2026 kwa matokeo ya Yanga 0-1 Simba SC.
  • Uongozi wa Simba hatimaye umetoa taarifa mpya kuhusu wachezaji wao majeruhi wakiwemo Oura, Kibabage na Kagoma.

Imebaki Siku 1 tu, Kuelekeea mchezo mkali wa Simba SC vs Yanga SC maarufu kama Kariakoo Dabi. Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), unatarajiwa kupigwa Jumapili 3/5/2026 Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. Mchezo huu ni wa pili kwa timu hizo kukutana wiki hii, mara baada ya juzi Jumatano Simba SC kuibuka mabingwa wa Muungano Cup 2026 kwa matokeo ya Yanga 0-1 Simba SC. Uongozi wa Simba hatimaye umetoa taarifa mpya kuhusu wachezaji wao majeruhi wakiwemo Oura, Kibabage na Kagoma.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Simba SC vs Yanga SC, Kuhusu taarifa ya majeruhi wa Simba SC

Simba SC vs Yanga SC
Oura akitoka baada ya kuumia

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari, Menej awa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema: “Nipo hapa kuzungumzia mchezo wa Mei 3, 2026 wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans. Mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, uwanja ambao kiasili tunautumia kama uwanja wetu wa nyumbani. Kuhusu hali ya kikosi chetu kina ari kubwa, kuelekea mchezo huu.

“Ikumbukwe baadhi ya wachezaji wetu muhimu walipata majeraha katika mchezo wa Fainali ya Muungano Cup, dhidi ya Yanga SC na kuleta hofu kuelekea mchezo huu. Baadhi ya wachezaji hao ni Anicet Oura, Nickson Kibabage na Yusuph Kagoma. Napenda kuwajulisha kwamba wachezaji hao wote ambao walitolewa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano kwa kuumia, wako tayari kwa mchezo wa Jumapili. Ninapozungumza hapa wachezaji wapo vizuri kabisa, Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kulinda hali zao.”

SOMA HII PIA: Waamuzi wa Morocco washtua Simba SC vs Yanga SC, ‘Dabi ya Kariakoo’ NBC Premier League, Ratiba, matokeo, msimamo na Takwimu | SportPesa Blog

Kuhusu mabadiliko ya Uwanja mechi ya Simba SC vs Yanga SC

Simba SC vs Yanga SC kupigwa Uwanja wa Meja Isamuhyo
Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo

Akifafanua kuhusu mabadiliko ya Uwanja yaliyotokea, Ahmed amesema: “Tunafahamu kwamba Uwanja Mkapa ni uwanja bora, lakini kutokana na marekebisho ambayo yanaendelea tuliamua kuchagua uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Ukitoa Uwanja wa Mkapa, Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, ndio unaongoza kwa eneo zuri la kuchezea. Isichukuliwe kama tumepeleka pale ili kumkomoa mtu, ndio maana tunatangaza kistaarabu tofauti na wenzetu walipopeleka mechi Zanzibar.

“Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo tunatarajia utaingiza mashabiki 10,000 na kama hutapata tiketi, tafadhali baki nyumbani kwako. Niwakumbushe eneo lile lote na uwanja lipo chini ya JKT. Kama huna tiketi kaa mbali, ufuatilie mchezo kupitia luninga.”

SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Yanga SC |Ratiba, matokeo, Takwimu, Hawa hapa wachezaji 10 hatari wakuchungwa Kariakoo Dabi

Kuhusu tiketi Simba SC vs Yanga SC

Akizungumzia viingilio vya mchezo huo, Ahmed amesema: “Hatujataka kuweka viingilio vya kausha damu ili kila Mwanasimba aweze kuingia uwanjani, kwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo tungeweza kuweka viingilio vikubwa. Lakini tumeweka viingilio rafiki, ili watu wanunue tiketi mapema, tumezungumza na N-Card kuangalia namna ya kudhibiti vishoka ili asije kutuharibia mechi yetu.  Kwa uchache wa tiketi, ni wazi kuwa mwenye dhamira ya kwenda uwanjani basi akanunue tiketi yake sasa.”

Hitimisho

Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC
Seleman Mwalimu

Simba SC vs Yanga SC ni zaidi ya mchezo, hii ni vita yav kusaka heshima na rekodi kati ya watani hawa wa jadi. Baada ya matokeo ya Yanga SC 0-1 Simba SC kule Zanzibar, imezidi kuongeza ugumu wa mchezo huu. Dakika 90 za Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo zitatoa majibu.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.