- Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC vita nzito
- FT: Yanga SC 0-1 Simba SC ni matokeo ya Fainali Muungano Cup, Aprili 29, 2026 Uwanja wa New Amaan Complex.
- Steve Barker anashinda taji lake la kwanza akiwa kwenye benchi la ufundi unyamani na kutwaa tuzo
Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC mtifuano mzito. Katika mechi 3 mnyama ametwaa tuzo 3 huku Wananchi wakitwaa tuzo mbili. Kwenye tuzo za jumla, Simba SC kabeba tuzo zote muhimu Aprili 29, 2026 wakiwavua ubingwa Yanga SC kwa ushindi wa goli 1-0. Seleman Mwalimu mfungaji pekee wa goli la ushindi amechaguliwa kuwa mfungaji bora akifunga magoli 3.
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini

Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC

Vita imekwisha Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC huku bingwa akiwa kinara. Wababe hawa wawili Kariakoo Dabi ya Zanzibar imekwisha bado hawajamalizana. Mei 3, 2026 Simba SC vs Yanga SC, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo, NBC Premier League.
Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Steve Berkar wamefanikiwa kutwaa ubingwa mbele ya mabingwa watetezi. Katika mchezo wa fainali ilikuwa lazima mmoja afungwe na mmoja apoteze. Kituo kinachofuata ni Dar kwenye mchezo wa ligi.
SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo

Tuzo ya Man of The Match Muungano Cup 2026
| Hatua | Mechi/Timu husika | Mchezaji aliyechaguliwa |
|---|---|---|
| Robo fainali | Yanga SC vs Muembe Makumbi | Shekhan Khamis (Yanga SC) |
| Nusu fainali | Yanga SC vs Azam FC | Duke Abuya (Yanga SC) |
| Robo fainali | KVZ vs Azam FC | Ngita Jean (Azam FC) |
| Robo fainali | Simba SC vs Mafunzo SC | Semfuko Daud (Simba SC) |
| Nusu fainali | Mlandege FC vs Simba SC | Neo Maema (Simba SC) |
| Robo fainali | Mlandege FC vs Singida Black Stars | Mbappe (Mlandege FC) |
| Fainali | Simba SC vs Yanga SC (Aprili 29, 2026) | De Reuck (Simba SC) |
Simba SC vs Yanga SC kwenye vita ya tuzo ya wachezaji bora kazi ilikuwa nzito. Mnyama ametoa wachezaji watatu kila mchezo alifanikisha malengo hayo. Mwananchi ni wachezaji wawili ilikuwa hatua ya robo fanali na nusu fainali.
Timu ya Singida Black Stars haikufanikisha kutoa hata mchezaji mmoja. Timu hiyo iliishia hatua ya robo fainali. Kwa timu kutoka Tanzania Bara ilikuwa ya kwanza kufungashiwa virago, Azam FC ikafuata hatua ya nusu fainali.
Takwimu za wafungaji magoli

| Mchezaji | Timu | Idadi ya Magoli |
| Prince Dube | Yanga SC | 3 |
| Shekhan Khamis | Yanga SC | 2 |
| Ngita Jean | Azam FC | 2 |
| Seleman Mwalimu | Simba SC | 3 |
Takwimu za waliobeba tuzo za jumla
| Tuzo | Mshindi | Timu | Takwimu |
| Mfungaji Bora | Seleman Mwalimu | Simba SC | Magoli 3 |
| Kipa Bora | Hussen Mwalimu | Simba SC | Clean sheet 2 |
| Kocha Bora | Steve Barker | Simba SC | Ongoza mechi 3 |
| Mchezaji Bora Chipukizi | Hussein Mbegu | Simba SC | Anza kikosi cha kwanza mechi 2 |
Hitimisho
Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC kazi ya kwanza imekwisha. Mara ya mwisho wababe hawa kukutana Uwanja wa New Amaan Complex ilikuwa mchezo wa ligi, Yanga SC 0-0 Simba SC. Taji la kwanza kwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker. Je Yanga SC watakubali kufungwa mara mbili dhidi ya Simba SC ama watalipa kisasi? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa.

