Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SCMuungano Cup
  • Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC kwa kuifunga Yanga SC goli 1-0 hatua ya fainali.
  • Goli la ushindi lilifungwa na Seleman Mwalimu kwa mkwaju wa penati iliyosababishwa na Edmund John
  • Dabi ya Kariakoo Zanzibar ushindi kwa mnyama, Clatous Chama alichezewa faulo dakika za jioni.

Rekodi imeandikwa Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC mbele ya Pedro Goncalves wa Yanga SC. Aprili 29, 2026 ubao wa New Amaan Complex ulisoma Yanga SC 0-1 Simba SC goli likifungwa na Seleman Mwalimu kwa mkwaju wa penati. Muungano Cup 2026 mshindi rasmi ni mnyama ambaye amesharejea nalo Dar akitokea Zanzibar.

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SOMA HII: Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026 | Highlights, goal | Seleman Mwalimu na Clatous Chama wazamisha jahazi

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC mbele ya Pedro Goncalves wa Yanga SC

Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC
Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC akikabidhiwa tuzo na Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi.

Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC baada ya kupokea mikoba ya Dimitar Pantev. Raia huyu wa Afrika Kusini amekuwa na mwendelezo mzuri kwenye mechi za ushindani. Katika mechi tatu za Muungano Cup 2026 zote timu ilipata ushindi.

Hili linakuwa ni taji la kwanza kwa Simba SC 2025/26. Mara baada ya mashindano kukamilika kocha wa Simba SC alitwaa tuzo ya kocha bora. Hii inatokana na matokeo mazuri ambayo alipata kwenye mechi zote.

Edmund John nyota wa Yanga SC alimchezea faulo Clatous Chama dakika ya 118. Zilikuwa zimesalia dakika 2 mchezo huo kukamilika kwa kuwa dakika 90 ilikuwa 0-0. Mwalimu alimfunga Djigui Diarra kipa namba moja wa Yanga SC.

Mnyama kwenye mechi tatu alifunga jumla ya magoli 4. Kinara wa ufungaji ni Seleman Mwalimu akiwa nayo matatu. Goli moja lilifungwa na Neo Maema hatua ya nusu fainali dakika ya 89.

SOMA HII: Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC | Matokeo, takwimu | SportPesa Blog

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Matokeo ya mechi za Steve Barker Muungano Cup 2026

Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC
Seleman Mwalimu mshambuliaji wa Simba SC.
TareheHatua ya MashindanoMechiMatokeo
Aprili 23, 2026Robo fainaliSimba SC vs Mafunzo SC1-0
Aprili 26, 2026Nusu fainaliMlandege FC vs Simba SC0-3
Aprili 29, 2026FainaliYanga SC vs Simba SC0-1

Tuzo kwa Simba SC Muungano Cup 2026

TuzoMshindiTimuTakwimu
Mfungaji BoraSeleman MwalimuSimba SCMagoli 3
Kipa BoraHussen MwalimuSimba SCClean sheet 2
Kocha BoraSteve BarkerSimba SCUshindi mechi 3
Mchezaji Bora ChipukiziHussein MbeguSimba SCAmeanza kikosi cha kwanza mechi 2

SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo

Hitimisho

Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC mbele ya Pedro Goncalves wa Yanga SC. Kocha huyu ameongeza ari ya ushindani kwenye kikosi hicho. Je rekodi yake itaendelea kwenye mataji mengine ikiwemo CRDB Federaton Cup na NBC Premier League? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa.

Share this: