- Je, Waamuzi Simba SC vs Yanga SC wanatoka Morocco? Ni swali gumu ambalo mashabiki wanajiuliza kuelekea mchezo mkali wa Simba SC vs Yanga SC
- Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), utapigwa Jumapili tarehe 3/5/2026, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
- Hii itakuwa mara ya 2 timu hizi kukutana ndani ya wiki hii, ambapo jana Jumatano walivaana katika Fainali ya Muungano Cup 2026 na Simba SC kuibuka bingwa kwa matokeo ya Yanga SC 0-1 Simba.
- Kamati ya Waamuzi yatoa tamko zito kuhusu kuleta waamuzi kutoka Morocco.
Taarifa ya Waamuzi Simba SC vs Yanga SC kutoka Morocco kuamua mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Jumapili 3/5/2026, imezidi kuwa gumzo. Hii ni kuelekea mchezo huo mkali wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), ambapo Simba SC wataikaribisha Yanga SC. Mchezo huu ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam utatoa taswira ya ubingwa msimu huu. Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana wiki hii, mara baada ya jana Jumatano Simba SC kuibuka mabingwa wa Muungano Cup 2026 kwa matokeo ya Yanga 0-1 Simba SC.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu Waamuzi Simba SC vs Yanga SC kutoka Morocco kusimamia mechi

Taarifa ambayo imekuwa gumzo, ambayo inasubiri uthibitisho wa Bodi ya Ligi Tanzania ni uamuzi wa kuwaleta waamuzi wa Morocco kusimamia mchezo huu mkubwa. Tetesi za taarifa hiyo zimeeleza kuwa, uamuzi huo umefikiwa ili kuhakikisha kunakuwa na uendeshaji bora wa mchezo huo. Katika hatua nyingine, baadhi ya majina ya waamuzi wa Morocco yanayotajwa kupewa mchezo huo ni; Mwamuzi Hamza El Faruq, Mwamuzi Lahsene Azkawi, Mwamuzi Hamza El Nasri, na Mwamuzi Mostafa Kchaaf.
SOMA HII PIA: Mwamuzi Yanga SC vs Simba SC balaa! kuna kadi nyekundu leo?
Kamati ya Waamuzi wa Ligi Kuu ya NBC watoa tamko

Wakati tetesi hizo zikizidi kupamba moto, Kamati ya Waamuzi kupitia kwa Mwenyekiti wake, Soud Abdi akizungumza na Chombo kimoja cha Habari amesema: “Uamuzi wa kuwatumia waamuzi wa kigeni unalenga kuongeza uwazi, na kuondoa malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kwenye michezo mikubwa ya ndani. Kwa uzoefu wao, waamuzi wa kigeni wanaopewa mechi hizi, wanatarajiwa kuhakikisha mchezo unaendeshwa kwa haki na kufuata sheria zote za soka.
“Kwa hali hiyo, matarajio ya wengi ni kuona dabi yenye ushindani mkali lakini yenye uamuzi wa haki. Pia hii inalenga ubora wa timu uwanjani, kuamua matokeo. Hali hii hisababisha kupungua kwa malalamiko na mijadala baada ya mchezo kuisha.
“Mpaka sasa bado hatujatoa taarifa rasmi ya Waamuzi ambao watasimamia mechi hii, na wakati utakapofika basi tutaweka wazi. Kanuni za ligi yetu zinaturuhusu kutumia Waamuzi wowote, ambao watatoa matokeo bora ya uamuzi wa mchezo. Na waamuzi wa kigeni waliosimamia mechi kadhaa, wameonekana kupunguza sana malalamiko, lakini kama Taifa pia tuna Waamuzi wengi bora ambao wanaweza kusimamia mechi hizi kubwa.”
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC taarifa muhimu kuhusu waamuzi wa mchezo Juni 15 2025 viingilio kutolewa
Simba SC vs Yanga SC, historia ya h2h

Katika miaka ya karibuni timu hizi zimekutana katika michezo 23 ya mashindano yote, Simba SC imeshinda mechi 4 tu, Yanga SC wao wameshinda mechi 8 ikiwemo mechi 6 mfululizo. Mechi 11 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare. Jumla ya mabao 45 yamefungwa katika mechi hizo kama jedwali hapa chini linavyoonyesha;
| Kipengele | Simba SC | Young Africans (Yanga) |
|---|---|---|
| Mikutano 23 ya Mashindano | ushindi 4 | ushindi 8 |
| Sare | 11 | 11 |
| Jumla ya Mabao ya Kufunga | 18 | 27 |
| Tarehe | Mashindano | Matokeo |
|---|---|---|
| 29 Aprili 2026 | Kombe la Muungano (Fainali) | Simba 1–0 Yanga |
| 1 Machi 2026 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Yanga 0–0 Simba |
| 25 Juni 2025 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Yanga 2–0 Simba |
| 19 Oktoba 2024 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Simba 0–1 Yanga |
| 8 Agosti 2024 | Ngao ya Jamii (Community Shield) | Yanga 1–0 Simba |
| 20 Aprili 2024 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Yanga 2–1 Simba |
| 5 Novemba 2023 | Ligi Kuu Tanzania Bara | Simba 1–5 Yanga |
Hitimisho

Tetesi za Waamuzi wa Morocco kusimamia mechi ya Simba SC vs Yanga SC zinazidi kupamba moto, hii ni kuelekea mchezo huu mkubwa utakaopigwa Jumapili 3/5/2026. Tetesi hizi zimezidi, baada ya kushuhudia mechi ya Fainali ya Muungano Cup 2026 ikisimamiwa na mwamuzi wa Kenya, Dickes Mimisa. Mechi hiyo iliisha kwa Simba SC kuibuka na ubingwa huku kukiwa na maoni tofauti, juu ya mwamuzi huyo. Muda utatoa majibu y ani nani Pilato wa Jumapili.

