Vozinha (-)Vozinha (-)
  • Cape Verde vs Saudi Arabia Kombe la Dunia 2026, mechi ya mzunguko wa 3 wa Kundi H kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya 32 bora.
  • Cape Verde baada ya kuishangaza dunia kwa kutoa sare dhidi ya Hispania na Uruguay, watavaana na Saudi Arabia Uwanja wa NRG, Houston, Jumamosi tarehe 27 Juni 2026
  • Mchezo huo utapigwa saa 9 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Cape Verde na Saudi Arabia wanahitaji ushindi ili kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu.
  • Makala hii inakuchambulia Live score, h2h, odds na habari za timu kuelekea mchezo huu.

Cape Verde, ambao wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza wameishangaza Dunia. Hii ni baada ya kukusanya mechi pointi 2 wakitoa sare dhidi ya Hispania na Uruguay, watakutana na Saudi Arabia katika mchezo muhimu na wa mwisho wa Kundi H utakaochezwa Uwanja wa NRG, Houston. Mchezo huu utapigwa Jumamosi tarehe 27 Juni 2026, saa tisa usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Saudi Arabia na Cape Verde wote wanahitaji pointi 3, ili kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu.

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Cape Verde vs Saudi Arabia

Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeborwesha na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Cape Verde vs Saudi Arabia
Cape Verde vs Saudi Arabia

Maelezo ya Mechi

Cape Verde vs Saudi Arabia Kombe la Dunia 2026
Saudi Arabia
KipengeleMaelezo
MashindanoMchezo wa tatu wa Kundi H katika fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Tarehe na MudaPambano hili litachezwa Jumamosi, tarehe 27 Juni 2026, kuanzia saa 03:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
UwanjaNRG Stadium, uliopo Houston, Texas nchini Marekani, utakuwa mwenyeji wa mechi hii.
Hali ya Kundi HHispania wanaongoza kundi kwa pointi 4 na tayari wamefuzu, huku Cape Verde na Uruguay wakifuatia kwa pointi 2 kila mmoja. Saudi Arabia wanashika nafasi ya mwisho kwa pointi 1.
Umuhimu wa MchezoSaudi Arabia wanahitaji ushindi ili kuendeleza matumaini yao ya kufuzu hatua inayofuata. Kwa upande wa Cape Verde, pointi tatu zinaweza kuwahakikishia nafasi nzuri zaidi kwenye kundi na hata kuwapa fursa ya kumaliza katika nafasi mbili za juu kutegemea matokeo mengine.
Mchezo Mwingine wa KundiWakati huohuo, Hispania na Uruguay watakuwa wakimenyana katika mechi nyingine muhimu ya Kundi H.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104 MPAKA FAINALI, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Wapi kwa kutazama (How to watch) Cape Verde vs Saudi Arabia Kombe la Dunia 2026

Mashabiki wanaweza kufuatilia mechi ya Cape Verde vs SaudiArabia kupitia watangazaji rasmi wa FIFA World Cup 2026 katika nchi zao. Kwa Tanzania, angalia ratiba ya matangazo ya washirika rasmi wa FIFA, na fuatilia SportPesa Blog kwa live score, matokeo, highlights na taarifa za mchezo.

Muhtasari wa Cape Verde vs Saudi Arabia

Cape Verde
Cape Verde

Cape Verde wamekuwa na mashindano ya aina yake, wakishiriki kwa mara ya kwanza hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa. Katika mchezo wao wa kwanza walitoka sare tasa dhidi ya Hispania, mabingwa wa dunia wa mwaka 2010, matokeo yaliyoshangaza wengi. Baadaye walionyesha moyo wa kupambana kwa kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Uruguay baada ya kurejea mara mbili kwenye mchezo.

Kipa mkongwe Vozinha amekuwa nguzo muhimu ya mafanikio hayo, huku mabeki Logan Costa na Roberto Lopes wakiongoza safu ya ulinzi kwa ustadi mkubwa chini ya kocha Rui Águas. Habari njema kwa Cape Verde ni kurejea kwa Jovane Cabral, ambaye alikuwa na tatizo la majeraha dhidi ya Uruguay. Sasa yuko fiti na anatarajiwa kuanza mchezo, akiongeza kasi na ubunifu kwenye safu ya ushambuliaji. Kevin Piña na Hélio Varela pia wamekuwa muhimu, huku Dailon Livramento na Gilson Benchimol wakiongoza mashambulizi.

Kwa upande wa Saudi Arabia, shinikizo ni kubwa. Baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Uruguay katika mchezo wa kwanza, walipokea kichapo cha mabao 4-0 kutoka Hispania katika mchezo wa pili. Matokeo hayo yalifichua mapungufu makubwa ya safu yao ya ulinzi. Kocha Hervé Renard anajua kuwa ushindi pekee, ndiyo njia ya kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu. Nahodha Salem Al-Dawsari bado ni tishio kubwa kwa Saudi Arabia, huku Firas Al-Buraikan akiongoza safu ya ushambuliaji.

KWA UCHAMBUZI WA MECHI INAYOFUATA YA URUGUAY, SOMA HII: Uruguay vs Spain FIFA Kombe la Dunia 2026: Prediction, Kundi H, match preview, h2h, odds

Habari za Timu na Vikosi Vinavyotarajiwa

Cape Verde

NafasiMchezaji
Kipa (GK)Vozinha
Beki wa Kulia (RB)Moreira
Beki wa Kati (CB)Roberto Lopes
Beki wa Kati (CB)Logan Costa
Beki wa Kushoto (LB)Wagner Pina
Kiungo wa Kulia (RM)Telmo Arcanjo
Kiungo wa Kati (CM)Deroy Duarte
Kiungo wa Kati (CM)Kevin Piña
Kiungo wa Kushoto (LM)Jovane Cabral
Mshambuliaji (ST)Dailon Livramento
Mshambuliaji (ST)Gilson Benchimol

Saudi Arabia

Kikosi cha Saudi Arabia
Kikosi cha Saudi Arabia
NafasiMchezaji
Kipa (GK)Mohammed Al-Owais
Beki wa Kulia (RB)Saud Abdulhamid
Beki wa Kati (CB)Hassan Al-Tambakti
Beki wa Kati (CB)Ali Lajami
Beki wa Kushoto (LB)Boushal
Kiungo wa Ulinzi (DM)Mohammed Kanno
Kiungo wa Kati (CM)Al-Khaibari
Kiungo wa Kati (CM)Musab Al-Juwayr
Winga wa Kulia (RW)Salem Al-Dawsari
Mshambuliaji (ST)Firas Al-Buraikan
Winga wa Kushoto (LW)Al-Shehri

Takwimu Muhimu

  • Cape Verde wamekusanya pointi 2 katika michezo miwili.
  • Walitoka sare ya 0-0 dhidi ya Hispania na sare ya 2-2 dhidi ya Uruguay.
  • Bado hawajapoteza katika mechi zao nne za mwisho za mashindano rasmi.
  • Hii ni mara yao ya kwanza kushiriki Kombe la Dunia.
  • Vozinha amekuwa mmoja wa makipa bora wa mashindano hadi sasa.
  • Jovane Cabral amerejea baada ya kupona majeraha.
  • Saudi Arabia wana pointi 1 pekee katika michezo miwili.
  • Walitoka sare dhidi ya Uruguay kabla ya kufungwa 4-0 na Hispania.
  • Salem Al-Dawsari ndiye mchezaji hatari zaidi wa Saudi Arabia.
  • Firas Al-Buraikan anaiongoza safu ya ushambuliaji.
  • Huu ni mkutano wa kwanza kabisa kati ya Cape Verde na Saudi Arabia.

Rekodi ya Cape Verde vs Saudi Arabia H2H

Cape Verde na Saudi Arabia hawajawahi kukutana katika mechi yoyote ya kimataifa, iwe ya kirafiki au ya mashindano rasmi. Hii itakuwa mara yao ya kwanza kukutana. Hivyo huu, ni mchezo utakaobeba historia mpya.

Utabiri Wetu (zaidi ya bao 1 yaani over 0.5)

Cape Verde vs Saudi Arabia Kombe la Dunia 2026
Kipa wa Cape Verde Vozinha

Cape Verde wameonyesha nidhamu kubwa ya kiufundi, na uwezo wa kupambana dhidi ya timu zenye majina makubwa kama Hispania na Uruguay. Kurejea kwa Jovane Cabral kunawapa nguvu zaidi kwenye safu ya ushambuliaji. Ingawa Saudi Arabia wana wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Salem Al-Dawsari na Firas Al-Buraikan, matatizo yao ya ulinzi yalifichuliwa dhidi ya Hispania. Mchezo huu unatarajiwa kushuhudia zaidi ya bao 1.

kujua ratiba ya mechi za afrika kusini soma hii: Ratiba ya Afrika Kusini FIFA Kombe la Dunia 2026 | Uwanja | Tarehe| Kikosi | Kundi A | SportPesa Blog

Hitimisho

Utabiri wetu wa kiuhariri unayapa nafasi kubwa matokeo ya zaidi ya bao moja kwa kuwa kila timu inalazimika kusaka pointi 3, ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu hatua inayofuata. Mechi hi itaamua nani anakwenda hatua inayofuata ambapo timu zote zinahitaji ushindi kufufua matumaini ya kusonga mbele. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za DR Congo vs Uzbekistan kwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Cape Verde dhidi ya Saudi Arabia itaanza saa ngapi?

Mchezo utaanza saa 03:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) siku ya Jumamosi, tarehe 27 Juni 2026.

Je, Cape Verde wanaweza kufuzu kutoka Kundi H?

Ndiyo. Ushindi katika mechi hii utawahakikishia angalau nafasi ya tatu, na wanaweza hata kumaliza katika nafasi mbili za juu kutegemea matokeo ya Hispania dhidi ya Uruguay.

Je, Jovane Cabral atacheza?

Ndiyo. Amepona majeraha na anatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza.

Vozinha ni nani?

Vozinha ni kipa mkongwe wa Cape Verde ambaye amekuwa na kiwango bora sana, katika kampeni yao ya kwanza ya Kombe la Dunia.

Cape Verde na Saudi Arabia wako kundi gani?

Timu zote mbili zipo Kundi H pamoja na Hispania na Uruguay. Baada ya michezo miwili, Hispania wanaongoza kwa pointi 4, Cape Verde na Uruguay wana pointi 2 kila mmoja, huku Saudi Arabia wakiwa na pointi 1.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.