Namungo FC 1-0 Polisi Tanzania FC: NBC Premier League, Matokeo, Highlights, magoli, Lukindo awapa pointi 3 wauaji wa kusini
- Dakika 90 zimetamatika katika dimba la Majaliwa mkoani Lindi, huku matokeo yakiwa Namungo FC 1-0 Polisi Tanzania.
- Ni Nyota wa Namungo, Herbert Lukindo ndiye aliyewahakikishia wenyeji ushindi huo muhimu.
- Ushindi huo unawafanya Namungo kukwea mpaka nafasi ya 6 ya msimamo na pointi zao 15, walizokusanya katika michezo 10, huku Polisi Tanzania wakishuka hadi nafasi ya 10 na pointi zao 12.
- Makala hii inachambua baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu kwa picha za mchezo huu.
Kutoka Uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa, dakika 90 zimetamatika katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, huku matokeo yakiwa Namungo FC 1-0 Polisi Tanzania. Nyota wa Namungo, Herbert Lukindo ndiye aliyewahakikishia wenyeji ushindi huo muhimu kwa bao lake la dakika ya 30. Ushindi huo unawafanya Namungo kukwea mpaka nafasi ya 6 ya msimamo na pointi zao 15, walizokusanya katika michezo 10, huku Polisi Tanzania wakishuka hadi nafasi ya 10 na pointi zao 12. Makala hii inachambua baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu kwa picha za mchezo huu.
SOMA HII PIA: Namungo FC 2-1 Coastal Union: NBC Premier League | Highlights | Msimamo
Unaweza kubashiri mechi hii kwa odds kubwa za SportPesa, gusa hapa chini
Shinda mpaka Milioni 800, cheza kindege ‘aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini

Kipindi cha kwanza Namungo FC 1-0 Polisi Tanzania

Mchezo huu ulianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikisaka bao la mapema ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuvuna pointi 3 muhimu. Licha ya mashambulizi hayo lakini ndani ya dakika 29 hakukuwa na bao kway imu yoyote. Namungo walipata penalti ambayo ilishindwa kuwekwa kimiani na Herbert Lukindo. Hatimaye dakika ya 30 mpira mrefu uliopigwa na kiungo Nassoro Kapama uliambaa langoni mwa Polisi kabla ya kufungwa kwa Kichwa na Lukindo na bao hilo kudumu hadi dakika 45 kuisha.
Kipindi cha pili

Kipindi cha pili timu zote ziliuanza mchezo kwa kasi. Namungo wakisaka bao la kuongeza ili kujihakikishia ushindi, na Polisi Tanzania wakisaka bao la kufutia machozi. Licha ya piga nikupige za hapa na pale, bado matokeo ya mchezo huo yalisalia kuwa kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza.
Hitimisho
Ushindi huo unaifanya Namungo kukwea mpaka nafasi ya 6 na pointi zao 15, hii ni baada ya kucheza mechi 10. Polisi Tanzania wanashuka hadi nafasi ya 10 wakiwa na pointi zao 12 tu, katika mechi 10 walizocheza. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa mpya zaidi

