Fountain Gate 0-1 Simba SC: NBC Premier League, Matokeo, Highlights, magoli, Rushine aibeba Simba SC

Bao la RushineBao la RushineBao la Rushine

Fountain Gate 0-1 Simba SC: NBC Premier League, Matokeo, Highlights, magoli, Rushine aibeba Simba SC

  • Ubao wa matokeo wa Tanzanite Kwaraa huko Babati mkoani Manyara umesoma Fountain Gate 0-1 Simba SC.
  • Ni mwendelezo wa ushindi kwa timu hiyo, ambayo inasalia kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wala kutoa sare msimu huu, wakiwa na asilimia 100 ya ushindi.
  • Ni mlinzi Rushine De Reuck ndiye aliyeibeba Simba SC mabegani, baada ya bao lake la mpira wa kichwa dakika ya 33 kusalia kuwa bao pekee la mchezo.
  • Makala hii inachambua baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu kwa picha za mchezo huu.

Fountain Gate 0-1 Simba SC, ndivyo ulivyosoma ubao wa matokeo wa Tanzanite Kwaraa huko Babati mkoani Manyara. Hii ni katika mwendelezo wa ushindi kwa timu hiyo, ambayo inasalia kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wala kutoa sare msimu huu, wakiwa na asilimia 100 ya ushindi. Mlinzi wa Kati wa Simba SC, Rushine De Reuck ndiye aliyeibeba Simba SC mabegani, baada ya bao lake la mpira wa kichwa dakika ya 33 kusalia kuwa bao pekee la mchezo. Makala hii inachambua baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu kwa picha za mchezo huu.

SOMA HII PIA: Simba SC imepangwa Kundi C CAF: RS Berkane, Orlando Pirates na Colombe Sportive

Kipindi cha kwanza Fountain Gate 0-1 Simba SC

Toure (-)
Toure 

Mchezo huu ulianza kwa kasi kubwa huku Simba wakilisakama lango la Fountain Gate ili kusaka bao la mapema, lakini Fountain Gate walikaa imara. Baada ya majaribio kadhaa hatimaye Simba SC, walifanikiwa kupata bao la kuongoza na pekee la mchezo huo kupitia mpira wa kona aliouunga kwa kichwa. Bao hilo awali lilikataliwa na mwamuzi msaidizi wa pembeni, kabla ya kukubaliwa kufuatia marejeo ya mfumo wa FVS.

SOMA HII ZAIDI: Washambuliaji Simba SC ni hatari: Ligi Kuu ya NBC 2026/27, Takwimu, Libase Gueye atikisa

Shinda Milioni 800 muda huu, cheza kindege ‘aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini 

image
Win big with Sportpesa Aviator

Kipindi cha pili

Fountain Gate 0-1 Simba SC
Morice 

Kipindi cha pili timu zote ziliuanza mchezo kwa kasi. Simba SC wakisaka bao la kuongeza ili kujihakikishia ushindi, na Fountain Gate wakisaka bao la kufutia machozi. Licha ya piga nikupige za hapa na pale, bado matokeo ya mchezo huo yalisalia kuwa kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza.

SOMA HII PIA: Simba SC vs 15 de Agosto: Doumbia Day CAF Champions League | Livescore

Hitimisho

Ushindi huo unaifanya Simba SC kufikisha pointi 27 na kuendelea kushika usukani wa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Simba SC wanafuatiwa na Yanga SC ambao wamekusanya pointi 22 baada ya timu zote kucheza mechi 9. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa mpya zaidi

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.