- Ni Uruguay vs Spain FIFA Kombe la Dunia 2026 mchezo wa mwisho hatua ya makundi kwa Kundi H.
- Spain wamefuzu hatua ya 32 bora wanakutana na Uruguay inayotakiwa kushinda mchezo huo kufuzu hatua ya 32 bora
- SportPesa Blog tumekuletea uchambuzi wa mchezo, wachezaji muhimu na taarifa kuhusu mechi hiyo Juni 27, 2026.
Uruguay vs Spain FIFA Kombe la Dunia 2026 ni mchezo wa mwisho hatua ya makundi. Utachezwa Juni 27, saa 9:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Uwanja wa Estadio Akron.Uruguay wanatakiwa kushinda mchezo huo siku ya Jumamosi ikiwa wanataka kufuzu hatua ya mtoano. Mabingwa hao mara mbili wa Kombe la Dunia wanashika nafasi ya pili katika Kundi H wakiwa na pointi mbili baada ya kutoka sare katika michezo yao miwili ya mwanzo. Mchezo wao wa mwisho uliisha kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Cape Verde, ambao wanashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza.
Ijue ratiba ya FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mecchi za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Uruguay vs Spain angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa uwajibikaji.

Taarifa za mechi
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | FIFA Kombe la Dunia 2026 |
| Kundi | Kundi H – Mchezo wa 3 |
| Tarehe | Jumamosi, Juni 27, 2026 |
| Muda wa kuanza | Saa 9:00 usiku (EAT) |
| Mechi | Spain vs Uruguay |
| Uwanja | Estadio Akron |
| Jukwaa la kubashiria | SportPesa |
Msimamo Kundi H
| Nafasi | Timu | Pointi | Hali |
|---|---|---|---|
| 1 | Spain | 4 | Imefuzu |
| 2 | Uruguay | 2 | Bado inapigania kufuzu |
| 3 | Cape Verde | 2 | Bado inafursa |
| 4 | Saudi Arabia | 1 | Imeshuka nafasi |
Taarifa kuhusu timu

Takwimu za Norway vs Ufaransa: Norway vs Ufaransa FIFA Kombe la Dunia 2026: Prediction, h2h, lineups, odds
Spain, wanaongoza Kundi H wakiwa na pointi nne baada ya kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Saudi Arabia katika mchezo wao wa mwisho. Mabingwa wa Kombe la Dunia wa mwaka 2010 wanahitaji kuepuka kupoteza ili kumaliza kileleni mwa kundi hilo.Spain bado hawajaruhusu bao lolote katika mashindano haya na wanaonekana kuimarika kadri michezo inavyoendelea. Lamine Yamal alifunga bao lake la kwanza kabisa katika Kombe la Dunia kwenye ushindi dhidi ya Saudi Arabia.
Mara ya mwisho Uruguay walishindwa kuvuka hatua ya makundi ya Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 2002, na sasa taifa zima lina matumaini makubwa kwamba watafanikiwa kufuzu hatua ya mtoano.Huu ni mchezo muhimu kwao kusaka tiketi kufuzu 32 bora.
Uruguay vs Spain taarifa kuhusu timu
Viungo washambuliaji Maximiliano Araújo na Agustín Canobbio walifunga mabao katika mchezo wao uliopita na wanatarajiwa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza. Katika safu ya kiungo, Federico Valverde na Rodrigo Bentancur wamekuwa nguzo muhimu kwa timu hiyo, na wanatarajiwa kuanza tena katika mchezo huu muhimu.
Mbele, Federico Viñas anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji huku Uruguay wakisaka ushindi utakaowapa nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia 2026.Hakuna mabadiliko yanayotarajiwa kwenye kikosi cha Uruguay, huku kipa mkongwe Fernando Muslera akitarajiwa kuanza langoni tena.
Kwa upande wa Spain, kuna mabadiliko machache yanayotarajiwa kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya Saudi Arabia.Lamine Yamal anatarajiwa kupata nafasi yake ya pili ya kuanza katika mashindano haya, huku Ferran Torres akitarajiwa kuanza kwa mara ya kwanza katika kampeni hii.
Mikel Oyarzabal, aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Saudi Arabia, ataendelea kuanza katika kikosi cha kwanza. Hata hivyo, Dani Olmo na Yeremy Pino wanatarajiwa kuanzia benchi katika mchezo huu.
Uruguay vs Spain: Rekodi ya makabiliano na fomu ya sasa
Uruguay wako katika hali ya shinikizo kubwa wakihitaji ushindi, baada ya kutoka sare katika mechi nne mfululizo kabla ya mchezo huu. Kwa ujumla, Uruguay sasa hawajashinda mechi katika michezo sita mfululizo, huku ushindi wao wa mwisho ukiwa ni ushindi wa kirafiki wa 2-1 dhidi ya Uzbekistan mwezi Oktoba 2025.
Kwa upande mwingine, Spain wapo katika msururu wa kutofungwa katika mechi 12 mfululizo, jambo linaloonyesha uimara wao mkubwa.Hata hivyo, ingawa Spain bado hawajapoteza mechi, wamefanikiwa kushinda mechi mbili pekee kati ya tano za mwisho, hali inayoonyesha kuwa bado si wababe kamili katika kila mchezo.
Uruguay vs Spain h2h
Uruguay na Spain zimekutana mara 5 katika historia, huku Spain wakiwa na ubabe zaidi katika mechi hizi.
- Spain wameshinda: mara 4
- Sare: mara 1
- Uruguay: hawajashinda katika mechi hizi za karibuni zilizotajwa
| Tarehe | Matokeo |
| Juni 17, 2013 | Spain 2-1 Uruguay |
| Februari 6, 2013 | Spain 3-1 Uruguay |
| Agosti 17, 2005 | Spain 2-0 Uruguay |
| Januari 18, 1995 | Spain 2-2 Uruguay |
| Septemba 4, 1991 | Spain 2-1 Uruguay |
Fomu ya sasa
- Uruguay – DDD D L
(Sare, Sare, Sare, Sare, Kipigo) - Spain – W D W D D
(Ushindi, Sare, Ushindi, Sare, Sare)
Prediction Uruguay vs Spain
Kwa mujibu wa Opta Analyst mchezo huu mshindi atakuwa ni Spain. Uruguay wamepwa asilimia 15.8 kupata ushindi huku Spain akipewa asilimia 62.8. Spain wana safu ngumu ya ulinzi hivyo Uruguay watakuwa na kazi kubwa kupenya. Mbali na hilo safu ya ushambuliaji ya Uruguay imefunga mabao 3 huku ile ya Spain ikiwa imefunga mabao 4.
Utabiri wa matokeo kwa maoni ya mhariri ni Uruguay 1-2 Spain. Haya sio matokeo rasmi ni maoni.

Rekodi za Senegal vs Iraq hizi hapa: Prediction Senegal vs Iraq FIFA Kombe la Dunia 2026: Kundi I, h2h, team news, odds
Jinsi ya Kubashiri na SportPesa
Fungua ukurasa wa mechi ya Uruguay vs Spain kwenye SportPesa (link above).
Chagua aina ya masoko unayotaka kuweka dau lako – Single Bet (SB), Multi-Bet (MB), au Live Bet (LB)
Weka kiasi cha dau lako na uthibitishe.
Wapi kwa kutazama (How to watch) Uruguay vs Spain Kombe la Dunia 2026
Mashabiki wanaweza kufuatilia mechi ya Uruguay vs Spain kupitia watangazaji rasmi wa FIFA World Cup 2026 katika nchi zao. Kwa Tanzania, angalia ratiba ya matangazo ya washirika rasmi wa FIFA, na fuatilia SportPesa Blog kwa live score, matokeo, highlights na taarifa za mchezo.

