Ufaransa vs Iraq Kombe la Dunia 2026, Kundi I: Prediction, lineups, odds, h2h

ByLunyamadizo Mlyuka

June 20, 2026
Ufaransa vs Iraq Kombe la Dunia 2026Ufaransa vs IraqUfaransa vs Iraq
  • Ni Ufaransa vs Iraq Kombe la Dunia 2026, Kundi I mechi ya pili Juni 23, Jumatatu
  • Uwanja wa Lincoln Financial Filed utachezwa mchezo huo saa 6:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
  • SportPesa Blog tumekuletea uchambuzi wa kina kuhusu mchezo, wachezaji muhimu na hali ya timu zote kwa sasa


Ufaransa vs Iraq Kombe la Dunia 2026 ni mchezo mkali wa maamuzi kutoka Kundi I. Ushindi kwa Ufaransa utawapa tiketi kufuzu hatua ya mtoano rasmi katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Lincoln Financial Field, Philadelphia, Jumatatu. Ni Juni 23, 2026 saa 6:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki mchezo utachezwa. Ufaransa walishinda Senegal mabao 3-1, huku Iraq wakipoteza 4-1 dhidi ya Norway.

Hii hapa ratiba ya mechi zote FFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Unaweza kubashiri mechi hii ya Ufaransa vs Iraq na kupata odds kubwa zilizoboreshwa kwa kugusa hapa chini. Tafadhali bashiri kwa uwajibikaji.

France
France vs Iraq

Taarifa za Mechi

KipengeleMaelezo
MashindanoKombe la Dunia 2026 Kundi I, Mechi ya Pili
Tarehe na muda wa kuanzaJumatatu, 23 Juni 2026 saa 06:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)
UwanjaLincoln Financial Field, Philadelphia, Pennsylvania, Marekani
Msimamo wa Kundi IBaada ya mechi za kwanza: Norway pointi 3, Ufaransa pointi 3, Senegal pointi 0, Iraq pointi 0
Kilicho hatariniUfaransa wakishinda watafuzu rasmi hatua ya 32 bora. Iraq wakipoteza, nafasi yao ya kusonga mbele itakuwa ndogo sana na kuondolewa kutakaribia kuthibitishwa.
Jukwaa la kubashiriSportPesa

Ufaransa vs Iraq safari kuwania kufuzu 32 bora

Ufaransa vs Iraq Kombe la Dunia 2026
Mbappe nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Ufaransa walianza kampeni ya Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal. Kylian Mbappé alifunga mabao mawili na Bradley Barcola, alifunga moja chini ya kocha Didier Deschamps na kuthibitisha ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.Ufaransa ni mabingwa wa Kombe la Dunia wa 2018.

Wanaingia jijini Philadelphia kusaka ushindi vs Iraq kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya 32 bora bado na mechi moja mkononi. Michael Olise alikuwa katika kiwango cha juu kwenye mchezo wa ufunguzi anatarajiwa kuendelea kuanza upande wa kulia wa ushambuliaji. Aurélien Tchouéméni na Adrien Rabiot wanatarajiwa kuendelea kuongoza eneo la kiungo. Bradley Barcola naye anaendelea kushinikiza kupewa nafasi ya kuanza kikosini baada ya mchango wake mkubwa alipotokea benchi. Habari njema kwa Ufaransa ni kwamba hawana majeruhi wala wachezaji wenye matatizo ya utimamu wa mwili.

Kwa upande wa Iraq, kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Norway kilikuwa cha kuumiza, lakini hakikukosa dalili za ubora. Aymen Hussein aliisawazishia Iraq muda mfupi kabla ya mapumziko na kuwapa matumaini mashabiki wa “Simba wa Mesopotamia”. Hata hivyo, makosa ya kujihami yaliwaadhibu katika kipindi cha pili, huku Norway wakifunga mabao matatu zaidi kupitia Leo Østigård pamoja na bao la kujifunga.

 Kocha Graham Arnold sasa anakabiliwa na jukumu gumu la kuimarisha safu ya ulinzi, ambayo ilionekana kushindwa kukabiliana na kasi na presha ya wapinzani wao.Ubunifu wa Iraq unatarajiwa kutegemea uwezo wa Amir Al-Ammari katikati ya uwanja, huku kasi na mashambulizi ya moja kwa moja ya Ali Jasim yakitarajiwa kuwa silaha muhimu pembeni mwa uwanja. Mabeki Zaid Tahseen na Ali Hashim watalazimika kuwa makini zaidi na wenye nidhamu kubwa kuliko walivyokuwa dhidi ya Norway ikiwa wanataka kuizuia safu kali ya ushambuliaji ya Ufaransa.

Ufaransa vs Iraq Prediction

Kwa mujibu wa takwimu Ufaransa ina nafasi kushinda mchezo huu. Utabiri wetu matokeo itakuwa Ufaransa 4-1 Iraq. Hii inatokana na kasi ya safu ya ushambuliaji ya Ufaransa ikiongozwa na Mbappe.

Hii hapa ratiba ya Afrika Kusini FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba ya Afrika Kusini FIFA Kombe la Dunia 2026 | Uwanja | Tarehe| Kikosi | Kundi A | SportPesa Blog

Wachezaji wa Kufuatilia

MchuanoMuktadha
Kylian Mbappé vs Zaid TahseenMbappé alifunga mabao mawili dhidi ya Senegal. Tahseen anakabiliwa na kazi ngumu ya kumdhibiti mmoja wa washambuliaji hatari zaidi duniani.
Michael Olise vs Merchas DoskiOlise aliwasumbua sana wapinzani katika mechi ya kwanza ya Ufaransa. Doski atalazimika kuwa makini na mwenye nidhamu kubwa katika maeneo ya pembeni.

Habari za Timu na vikosi vinavyotarajiwa

Ufaransa hakuna majeruhi walioripotiwa. Didier Deschamps anatarajiwa kuendelea na kikosi kilekile kilichoshinda vs Senegal. Mbappé ataongoza safu ya ushambuliaji, Olise ataendelea upande wa kulia, huku Barcola akiwa na nafasi ya kuanza. Tchouéméni na Rabiot wanatarajiwa kuongoza eneo la kiungo.

Graham Arnold anatarajiwa kusisitiza maboresho ya kiulinzi katika kikosi cha Iraq baada ya makosa yaliyoigharimu timu dhidi ya Norway. Aymen Hussein na Mohanad Ali Al-Hamadi wanatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji, huku Amir Al-Ammari akiwa mhimili wa ubunifu kutoka katikati ya uwanja.

Vikosi vinavyotarajiwa

Hivi sio vikosi rasmi kwenye mchezo wa Ufaransa vs Iraq, vikosi vinatarajiwa kutolewa saa moja kabla ya mchezo

Ufaransa (4-3-3)Iraq (4-4-2)
Maignan (Kipa)Jalal Hasan (Kipa)
Koundé (Beki wa kulia)H. Ali (Beki wa kulia)
Konaté (Beki wa kati)Z. Tahseen (Beki wa kati)
Saliba (Beki wa kati)A. Hashim (Beki wa kati)
Hernandez (Beki wa kushoto)Doski (Beki wa kushoto)
Tchouaméni (Kiungo mkabaji)I. Bayesh (Kiungo wa kulia)
Rabiot (Kiungo)Al-Ammari (Kiungo wa kati)
Camavinga (Kiungo)O. Rashid (Kiungo wa kati)
Olise (Winga wa kulia)A. Jasim (Kiungo wa kushoto)
Mbappé (Mshambuliaji)Al-Hamadi (Mshambuliaji)
Barcola (Winga wa kushoto)A. Hussein (Mshambuliaji)

Takwimu Muhimu

  • Ufaransa waliifunga Senegal mabao 3-1 katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi I. Kylian Mbappé alifunga mabao mawili (dakika ya 66 na 90+), huku Bradley Barcola akiongeza bao la tatu.
  • Ufaransa ni mabingwa wa Kombe la Dunia wa mwaka 2018 na wanashika nafasi ya 2 kwenye viwango vya FIFA duniani.
  • Mwenendo wa Ufaransa katika mechi zao tano zilizopita ni: Ushindi, Ushindi, Kipigo, Ushindi, Ushindi (W W L W W). Kabla ya Kombe la Dunia waliwafunga Brazil 2-1, Colombia 3-1 na Ireland Kaskazini 3-1.
  • Kylian Mbappé, nahodha wa timu, alifunga mabao mawili dhidi ya Senegal na ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Ufaransa.
  • Michael Olise alikuwa mchezaji aliyeonyesha kiwango bora katika mechi ya kwanza na anatarajiwa kuanza tena.
  • Bradley Barcola alifunga bao akiwa ametokea benchi dhidi ya Senegal na anaweza kupewa nafasi ya kuanza.
  • Iraq walipoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya Norway katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi I. Aymen Hussein ndiye aliyefunga bao lao pekee.
  • Iraq wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40, mara yao ya mwisho ikiwa mwaka 1986.
  • Mwenendo wa Iraq katika mechi zao tano zilizopita ni: Kipigo, Kipigo, Sare, Ushindi, Ushindi (L L D W W). Kabla ya Kombe la Dunia walitoa sare ya 1-1 dhidi ya Hispania katika mechi ya kirafiki na kuifunga Bolivia 2-1 katika mechi ya kufuzu.
  • Aymen Hussein ndiye tishio kubwa zaidi la ushambuliaji kwa Iraq baada ya kufunga dhidi ya Norway.
  • Amir Al-Ammari ndiye tegemeo lao la ubunifu katikati ya uwanja.

H2H Ufaransa vs Iraq

Ufaransa na Iraq rekodi zinaonyesha kwamba hawajahi kukutana katika mechi za ushindani. Hivyo mchezo huu wa hatua ya makundi utakuwa ni mara ya kwanza.

TareheMchezo
Juni 23, 2026Ufaransa vs Iraq, Hatua ya Makundi, Kundi I

Mchanganuo wa Kundi I

  • Ufaransa wakishinda, watafikisha pointi sita na kufuzu rasmi hatua ya 32 bora. Matokeo ya mchezo wa Norway dhidi ya Senegal yatabainisha kama wataongoza kundi peke yao au watakuwa sawa kwa pointi na Norway.
  • Iraq wakishinda, kundi litafunguka upya, kwani watafikisha pointi tatu sawa na Ufaransa.
  • Sare itaiweka Ufaransa katika nafasi nzuri kuelekea mechi yao ya mwisho dhidi ya Norway, huku Iraq wakilazimika kuifunga Senegal katika mchezo wao wa mwisho ili kubaki na matumaini ya kusonga mbele.

Mwenendo wa karibuni

TimuMechi 5 za Mwisho (ikiwemo mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia)
UfaransaUshindi, Ushindi, Kipigo, Ushindi, Ushindi
IraqKipigo, Kipigo, Sare, Ushindi, Ushindi

Jinsi ya Kuweka dau kupitia SportPesa

  1. Fungua ukurasa wa mechi ya Ufaransa dhidi ya Iraq kwenye SportPesa (kupitia kiungo kilichotolewa hapo juu).
  2. Chagua soko la dau unalopendelea, iwe ni Single Bet (SB), Multi-Bet (MB) au Live Bet (LB) mara baada ya mchezo kuanza.
  3. Weka kiasi cha fedha unachotaka kucheza, kisha thibitisha na kukamilisha dau lako.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQ)

Mechi ya Ufaransa dhidi ya Iraq itaanza saa ngapi?

Mchezo huu utaanza saa 06:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) siku ya Jumatatu, tarehe 23 Juni 2026, katika Uwanja wa Lincoln Financial Field, uliopo Philadelphia, Pennsylvania, Marekani.

Nini kilitokea katika mechi ya kwanza ya Ufaransa kwenye Kombe la Dunia 2026?

Ufaransa iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi I. Kylian Mbappé alifunga mabao mawili, dakika ya 66 na lingine mwishoni mwa muda wa nyongeza, huku Bradley Barcola akiongeza bao la tatu. Mabingwa hao wa dunia wa mwaka 2018 walionyesha ubora mkubwa kipindi cha pili.

Nini kilitokea katika mechi ya kwanza ya Iraq kwenye Kombe la Dunia 2026?

Iraq ilipoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya Norway katika mechi yao ya ufunguzi. Aymen Hussein aliisawazishia Iraq na kufanya matokeo kuwa 1-1 kabla ya mapumziko, lakini makosa ya safu ya ulinzi katika kipindi cha pili yaliigharimu timu hiyo baada ya Norway kufunga mabao matatu zaidi na kuondoka na ushindi mnono.

Ufaransa na Iraq wapo kundi gani katika Kombe la Dunia 2026?

Timu zote mbili zinashiriki Kundi I, pamoja na Norway na Senegal. Baada ya michezo ya kwanza, Norway na Ufaransa zina pointi tatu kila moja, huku Senegal na Iraq zikiwa bado hazijapata pointi.

Je, Ufaransa inaweza kufuzu hatua inayofuata katika mechi hii ya pili?

Ndiyo. Endapo Ufaransa itaishinda Iraq, itafikisha pointi sita na kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 32 bora ikiwa bado imebakiza mechi moja ya makundi, bila kujali matokeo ya mchezo kati ya Norway na Senegal.

Ni wachezaji gani muhimu wa Ufaransa katika Kombe la Dunia 2026?

Kylian Mbappé ndiye nahodha wa timu na tegemeo kubwa katika safu ya ushambuliaji. Michael Olise alikuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia zaidi katika mchezo wa kwanza, huku Bradley Barcola, aliyefunga akitokea benchi, akitajwa kuwa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza. Aurélien Tchouaméni ndiye nguzo muhimu katika eneo la kiungo.

France
France

Mabingwa watetezi utabiri mechi yao ijayo huu hapa: Argentina vs Austria Kombe la Dunia 2026: prediction, Live score, lineups, vikosi, h2h, live score, odds

Share this: