- FT: Azam FC 0-2 Simba SC matokeo ya hivi punde NBC Premier League 2026/27, Uwanja wa Azam Complex.
- Clatous Chama mwamba wa Lusaka amefunga bao la pili dakika ya 68 na lile la uongozi ni Fasika Idumba alijifunga
- Feisal Salum alianza kikosi cha kwanza akiongoza safu ya kiungo na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 42 kwa kumchezea faulo Nathaniel Chilambo.
Mchezo mkali umekamilika ubao ukisoma Azam FC 0-2 Simba SC Mzizima Dabi, Septemba 16, 2026. Mabao ya Simba SC yamefungwa na Fasika Idumba ambaye alijifunga dakika ya 58 na bao la pili limefungwa na Clatous Chama dakika ya 68. Unakuwa mchezo wa kwanza matajiri wa Dar wanapoteza msimu wa 2026/27.
Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha kindenge
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

Takwimu muhimu Azam FC 0-2 Simba SC Mzizima Dabi

Azam FC vs Simba SC H2H: Azam FC vs Simba SC NBC Premier League | H2H | Livescores | SportPesa Blog
| Kipengele | Maelezo |
| Matokeo | Azam FC 0-2 Simba SC |
| Wafungaji | Fasika Idumba (OG)58 na Clatous Chama dakika ya 68 |
| Simba SC Clean Sheet | 1 |
| Kadi nyekundu | 0 |
| Mabao | 2 |
| Uwanja | Azam Complex |
Unbeaten ya Azam FC yavunjwa mapema
Ushindi wa Simba SC umevunja rekodi ya matajiri wa Dar, Azam FC kucheza mechi 5 bila kufungwa. Huu ni mchezo wa kwanza timu hiyo kupoteza. Simba SC inafikisha jumla ya pointi 18 kibindoni sawa na Yanga SC tofauti kwenye mabao yakufunga na kufungwa.
Hitimisho
Azam FC 0-2 Simba SC ulikuwa ni mchezo wenye presha kubwa. Wachezaji wa timu zote walikuwa wanatumia nguvu na akili kusaka ushindi. Miongoni mwa wachezaji walioonyeshwa kadi za njano ni Himid Mao wa Azam FC aliyemchezea faulo Libase Gueye. Toure wa Simba SC anaingia kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC walioonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Elly Sasi.

