
JKT Tanzania ni moja ya timu yenye wachezaji bora wazawa wanaojituma kwenye mechi zote za ushindani. Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji muhimu akiwemo Bajana,mlinda mlango Ramadhan Chalamanda na mshambuliaji Paulo Peter. Matokeo ya mchezo wa hivi punde hayakuwa ni yenye furaha kwao. Ubao ulisoma Coastal Union 2-1 JKT Tanzania ilikuwa Septemba 12, 2026.Sera yao kubwa wanasema ‘Kichapo cha Kizalendo’.
Kuhusu ratiba na matokeo ya JKT Tanzania soma hii:JKT Tanzania: Ratiba, Matokeo na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa
Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.
Matokeo ya JKT Tanzania
Chini ya Kocha Mkuu Hamad Ally, JKT Tanzania imecheza mechi 6. Ushindi ni katika mechi 2, sare 1 na imepoteza mechi 3. Timu hiyo imekusanya pointi 7 ipo nafasi ya 10 inatumia Uwanja wa Meja Jen. Isamuhyo kwa mechi za nyumbani.
| Tarehe | Matokeo |
| Agosti 16, 2026 | JKT Tanzania 1-1 TRA United |
| Agosti 20, 2026 | Polisi Tanzania 2-0 JKT Tanzania |
| Agosti 24, 2026 | Yanga SC 4-0 JKT Tanzania |
| Agosti 29, 2026 | JKT Tanzania 2-0 Namungo FC |
| Septemba 5, 2026 | JKT Tanzania 3-0 Pamba FC |
| Septemba 12, 2026 | Coastal Union 2-1 JKT Tanzania |
Msimamo wa NBC Premier League
JKT Tanzania msimu wa 2026/27 kwenye msimamo ipo nafasi ya 10. Vinara wa ligi ni Yanga SC wenye pointi 18. Pamba Jiji FC inaburuza mkia ndani ya msimu ikiwa na pointi 1.

Matarajio ya jkt Tanzania kwa msimu wa 2026/27
Msemaji wa JKT Tanzania, Masau Bwire amesema kuwa malengo ya timu hiyo ni kuleta ushindani katika mechi zote. Msemaji huyo ametamba licha ya kutokuwa na matokeo mazuri watarejea kwenye ubora. Aliongeza kuwa kila mechi kwao ni fainali.
“Kila mchezo kwetu ni fainali kutokana na ushindani uliopo. Mashabiki waendelea kuwa nasi kuhakikisha kwamba tunapata matokeo. Ushindani ni mkali nasi tunaendelea kufanya maandalizi mazuri kwa mechi zijazo,”.
Hitimisho
JKT Tanzania inaendelea kuwa timu muhimu katika Ligi Kuu Bara, ikileta ushindani na burudani kwa mashabiki wa soka. Kwa ratiba iliyo mbele yao, matokeo ya hivi karibuni, na msimamo wa ligi, ni wazi kuwa safari yao bado ina changamoto nyingi. Tunawatakia kila la heri katika mechi zao zijazo na tunatumai watafanikiwa kufikia malengo yao ya msimu.


