- Saudi Arabia vs Uruguay Kombe la Dunia 2026 inaashiria kuanza rasmi kwa ratiba ya mechi za Kundi H la mashindano hayo.
- Mchezo huu utapigwa saa 7 usiku wa kuamkia Jumanne kwa saa za Afrika Mashariki.
- Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Miami Garden.
- Makala hii inauchambua mchezo huo kiufundi ikiwemo; h2h, vikosi, habari za timu na Utabiri wa matokeo.
Mechi za Kundi H Kombe la Dunia 2026 zinatarajiwa kuanza kesho Jumatatu. Timu za Uruguay na Saudi Arabia zitashuka Uwanjani kusaka pointi 3 za kwanza. Mechi hii itapigwa saa 7 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Uwanja wa Miami Garden ndio unatarajiwa kutumika.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa.
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Saudi Arabia vs Uruguay kwa kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kistaarabu.

Kuhusu Utabiri na uchambuzi wa mechi ya Saudi Arabia vs Uruguay

Saudi Arabia walikuwa na mashindano bora ya Kombe la Dunia 2022, hii ni baada ya kuishtua Dunia kwa ushindi wao wa mchezo wa kwanza dhidi ya Argentina. Uruguay wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu, kutokana na uzito na historia yao kwenye mashindano haya. Uwanja wa Miami Garden utakuwa mwenyeji wa pambano hili muhimu.
Timu hizi mbili zinashiriki Kundi H pamoja na timu za Hispania na Cape Verde, kundi linaloonekana kuwa na ushindani mkubwa. Saudi Arabia imekuwa mshiriki wa mara kwa mara wa Kombe la Dunia tangu mwaka 1994, ikikosa kufuzu tu katika michuano ya 2010 na 2014. Katika mashindano mawili yaliyopita ya Kombe la Dunia, Saudi Arabia ilitolewa katika hatua ya makundi. Hispania ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kumaliza kileleni mwa Kundi H, lakini nafasi ya pili inaonekana kuwa wazi.
SOMA HII PIA: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Saudi Arabia vs Uruguay rekodi ya timu hizi zilipokutana / H2H
Saudi Arabia imekutana na Uruguay mara tatu zilizopita, katika mashindano ya hivi karibuni. Kila imeshinda mechi moja, huku mchezo mmoja ukiisha kwa matokeo ya sare. Mara ya mwisho kukutana ilikuwa mwaka 2018 katika mashindano ya Kombe la Dunia, ambapo Uruguay walishinda bao 1-0. Hivyo matokeo yoyote ya mchezo huu, yanakwenda kuandika historia mpya yamakutano yao.
Fomu ya Saudi Arabia na Uruguay katika michezo 6 iliyopita
Saudi Arabia: LLLLWD
Katika michezo 6 iliyopita Saudi Arabia hawana rekodi nzuri wameshinda mechi moja pekee, wamepoteza mechi 4 na kutoa sare mchezo mmoja.
Uruguay WWDLDD
Kama ilivyo kwa wapinzani wao, Uruguay pia hawana rekodi bora ambapo wameshinda mechi 2 tu, Wametoa sare mechi 3 na kupoteza mechi 1.
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza
Hivi ni vikosi vinavyotarajiwa kuanza kulingana na fomu ya wachezaji, taarifa za awali za timu na mwenendo wa mechi zilizopita. Vikosi rasmi vitathibitishwa karibu na muda wa mchezo.
Saudi Arabia

Kipa: Al-Owais
Walinzi: Abdulhamid, Al Tambakti, Lajami, Bu
Viungo: Kanno, Al-Khaibari, N Al-Dawsari, Al-Juwayr, S Al-Dawsari
Mshambuliaji: Al-Buraikan.
Uruguay
Kipa: Muslera
Walinzi: Varela, Caceres, Bueno, Olivera
Viungo: Valverde, Ugarte, Bentancur, M Araujo, Vinas,
Mshambuliaji: Nunez
SOMA HII ZAIDI: France vs Senegal utabiri Kombe la Dunia 2026 | Kundi I
Habari za timu na majeruhi
Taarifa hizi ni zile zilizothibitishwa na timu za madaktari na mabenchi ya ufundi, lakini huweza kubadilika kutokana na maendeleo ya majeruhi. Hivyo, taarifa sahihi zaidi zitatolewa saa chache kuelekea mchezo huu. Kama ilivyo kawaida hii inatarajiwa kufanywa na timu za madaktari, kwa kushirikiana na mabenchi ya ufundi.
Saudi Arabia
Hawa wanatarajiwa kumkosa mchezaji wao, Nawaf Al Aqidi kutokana na majeraha ya misuli, lakini wachezaji wengine wote wako katika hali nzuri. Salem Al-Dawsari ndiye nahodha wa timu na mfungaji bora wa kikosi hicho akiwa na mabao 34, na Saudi Arabia watategemea ubunifu na uzoefu wake. Safu ya ushambuliaji itamtegemea, Firas Al-Buraikan, ambaye ana mabao 16 katika mechi 72 alizoichezea nchi yake.
Uruguay

Kuna Kundi kubwa la majeruhui ndani ya kikosi chao wakiwemo; Jose Gimenez (kifundo cha mguu), Ronald Araujo (misuli ya mguu), Giorgian de Arrascaeta (misuli ya mguu), Matias Vina (misuli). Sebastian Caceres amepata (jeraha la kichwani) na huenda akakosekana. Kati ya wachezaji hao, Caceres ndiye mwenye nafasi kubwa ya kucheza, na anaweza kuanza pamoja na Santiago Bueno.
Federico Valverde ndiye tegemeo kubwa la Uruguay na anatarajiwa kuanza eneo la kiungo. Manuel Ugarte, Rodrigo Bentancur na Darwin Nunez wakitarajiwa pia kuanza mchezo huo. Mastaa wengine wakianzia benchi.
SOMA HII PIA: Sweden vs Tunisia FIFA Kombe la Dunia 2026: Utabiri, H2H, muda, Kundi F | SportPesa Blog
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Saudi Arabia vs Uruguay Kombe la Dunia 2026 (Utabiri wetu: Saudi Arabia 1-2 Uruguay
Huu ni mchezo mgumu kutabiri kwani timu zote zina uwezo wa kushinda. Ubora na uzoefu wa Uruguay unabaki kuwa tofauti pekee, ambayo inaweza kuamua matokeo. Kwa mizania ya fomu, ubora wa vikosi na umuhimu wa mchezo, tunatarajia mchezo mgumu lakini tunaipa Uruguay nafasi ya kushinda 2-1.
Hitimisho:
Saudi Arabia vs Uruguay mechi ya Kundi H la Kombe la Dunia inaangaziwa kwa jicho la tofauti. Kwa uchambuzi wetu, tunatarajia mchezo mgumu na ushindi wa mabao 2-1 kwa Uruguay. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Saudi Arabia vs Uruguay, kwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.
Maswali muhimu yanayoulizwa kuhusu mchezo huu

Mechi ya Saudi Arabia vs Uruguay itachezwa lini?
Mechi hii itapigwa saa 7 usiku kuamkia Jumanne kwa saa za Afrika Mashariki.
Saudi Arabia vs Uruguay wapo kundi gani?
Huu ni mchezo wa Kundi H kwenye Kombe la Dunia 2026.
Saudi Arabia vs Uruguay zimewahi kukutana?
Timu hizi zina historia ya kukutana mara 3, ambapo kila timu imeshinda mara 1.
Utabiri wa Saudi Arabia vs Uruguay ni upi?
Utabiri wetu wa kiuhariri ni Saudi Arabia 1-2 Uruguay.
Saudi Arabia vs Uruguay itachezwa uwanja gani?
Mechi hii itachezwa Uwanja wa Miami Garden

