- Namba hazidanganyi je, nani kuibuka na Tuzo ya mchezaji bora Ligi Kuu NBC 2025/26 yaani MVP?
- Ubishi ni mkubwa kwenye vijiwe, kila mtu akitamba kuwa Nyota wake anayeamini anastahili kubeba tuzo hiyo.
- Kati ya wachezaji wote ni majina 3 yanaonekana kuteka mijala hiyo ambayo ni; Allan Okello, Clatous Chama na Feisal Salum.
- Makala hii inachambua takwimu za wachezaji hao, na kufichua kwanini wanatajwa sana?
Nani anastahili kuibuka na tuzo ya mchezaji bora Ligi Kuu NBC 2025/26? Mjadala ni mkubwa vijiweni na mitandaoni, huku majina matatu yakitajwa kwa ukubwa. Ni Feisal Salum, Allan Okello na Clatous Chama ambao wameonekana kuwa na moto wa hatari. Namba hazidanganyi na Makala hii inakuchambulia takwimu zao kuonyesha ni kwanini wanaimbwa?
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu ya NBC 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Aviator: High-flying wins up to 800,000,000.
Nani kubeba tuzo ya mchezaji bora Ligi Kuu NBC 2025/26?
Feisal Salum
Kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Azam FC, Feisal Salum amekuwa moto wa kuotea mbali. Feisal Salum kwa misimu kadhaa sasa ameendelea kuonesha kuwa, yeye ndiye injini inayozungusha timu yake. Msimu huu Feisal ndiye mchezaji mwenye takwimu bora zaidi kuliko wote, ambapo amehusika katika mabao 22. Anatawala listi ya wafungaji, akiwa kileleni na mabao yake 14, huku pia akiwa ameasisti mabao 8. Yote haya ameyafanya kwenye dakika 1963 tu katika mechi 24 alizocheza.
SOMA HII PIA: Pacome Zouzoua kutwaa tuzo ya mchezaji bora NBC Premier League 2024/25? Zijue rekodi zake, timu alizozifunga
Allan Okello
Huyu ndiye Nyota anayeimbwa zaidi kwa sasa, unaweza kumuita ‘star boy’ au balaa jipya. Licha ya kujiunga na Yanga SC kwenye dirisha dogo, lakini moto wa Okello unatisha. Amecheza kwa dakika 1405 tu za mechi 19, lakini amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 18 mpaka sasa. Nyota huyo wa kimataifa wa Uganda amefunga mabao 11 na kuasisti mabao 7. Allan Okello ana kasi, utulivu wa kupenya safu yoyote ya ulinzi.
SOMA HII ZAIDI: Vinara wa asisti NBC Premier League 2025/26 | Okello, Mpanzu, Feisal waiteka shoo
Clatous Chama
Waswahili wanasema “Kijiji bila wazee, hakiendi” ndicho alichothibitisha Chama ndani ya Simba SC. Amejiunga na Simba SC katika dirisha dogo la mwezi Januari, kipindi timu hiyo ikiwa inapitia kipindi kigumu. Katika muda mfupi tu, amefanikiwa kuibadilisha timu hiyo kuwa ya kutisha, baada ya kurejea makali yake. Chama ambaye anahudumu ndani ya kikosi cha Simba SC kwa mara ya pili, ni kama amezaliwa upya, hivi karibuni aliweka rekodi ya kubeba tuzo ya mchezaji bora wa mechi mara 4 mfululizo na anatajwa huenda anastahili kuwa MVP. Katika dakika 2035 za mechi 25 alizocheza amehusika kwenye mabao 14, akifunga mabao 8 na kuasisti mabao 6.
SOMA HII PIA: USIKU WA TUZO AGOSTI MOSI 2024, ZIJUE REKODI ZA WANAOWANIA
Hitimisho
Usiku wa tuzo za Ligi Kuu NBC 2025/26 unatajwa kuwa huenda utakuwa usiku wa moto, kutokana na ugumu wa maamuzi unaoweza kuamua baadhi ya vipengele. Kipengele cha Tuzo ya mchezaji bora Ligi Kuu NBC 2025/26 Vita ya Tuzo ya kipa bora NBC Premier League 2025/26 kimeanza kuzua mijadala ya mapema sana. Mechi 5 zimesalia kutoa majibu ya nani mchezaji bora msimu huu.




