- Vinara wa asisti NBC Premier League 2025/26 ni miongoni mwa mijadala mikubwa kwa sasa.
- Mpaka sasa Nyota, Allan Okello, Elie Mpanzu na Feisal wameiteka shoo na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda tuzo hiyo.
- Clatous Chama naye gari limewaka na anakuja kwa kasi, akiitaka tuzo hiyo.
- Zikisalia mechi 6 tu, kwa kila timu msimu huu ligi kumalizika, Je nani ataibuka kinara wa asisti?
Vita inazidi kuwa kali ndani ya Ligi Kuu Bara yaani (NBC Premier League 2025/26), wakati huu zikiwa zimebaki mechi 6 tu. Wapo wanaopambania ubingwa, wapo wanapambania kutoshuka daraja, lakini wapo wachezaji wanaosaka tuzo binafsi. Makala hii inakuletea takwimu za vinara wa asisti NBC Premier League, ambapo hawa ni wachezaji waliotoa pasi nyingi za mabao. Orodha hii ni kabla ya kuanza kwa mzunguko wa 24.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu ya NBC 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Hawa hapa vinara wa asisti NBC Premier League 2025/26

Jedwali lifuatalo linakuletea orodha ya wachezaji 100 walio kwenye orodha ya wafungaji bora NBC Premier League 2025/26.
| Nafasi | Mchezaji | Klabu | Nafasi Anayocheza | Asisti |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Feisal Salum | Azam FC | Kiungo | 8 |
| 2 | Allan Okello | Young Africans SC | Mshambuliaji | 7 |
| 3 | Elie Mpanzu | Simba SC | Kiungo | 7 |
| 4 | Duke Abuya | Young Africans SC | Kiungo | 6 |
| 5 | Maxi Nzengeli | Young Africans SC | Kiungo | 5 |
| 6 | Ibrahim Imoro | Mtibwa Sugar FC | Beki | 4 |
| 7 | Pacome Zouzoua | Young Africans SC | Kiungo | 4 |
| 8 | Lamin Jarjou | Singida Black Stars | Kiungo | 4 |
| 9 | Clatous Chama | Singida Black Stars | Kiungo | 4 |
| 10 | Israel Mwenda | Young Africans SC | Beki | 4 |
| Nafasi | Mchezaji | Klabu | Nafasi Anayocheza | Asisti |
|---|---|---|---|---|
| 11 | Neo Maema | Simba SC | Kiungo | 4 |
| 12 | Anuar Kilemile | JKT Tanzania | Beki | 3 |
| 13 | Ismail Aziz | Fountain Gate FC | Kiungo | 3 |
| 14 | Iddy Selemani | Azam FC | Kiungo | 3 |
| 15 | Rashid Chambo | KMC FC | Mshambuliaji | 3 |
| 16 | Ande Koffi | Singida Black Stars | Beki | 3 |
| 17 | Andrew Raymond Chamungu | Namungo FC | Mshambuliaji | 3 |
| 18 | Khleffin Hamdoun | Dodoma Jiji FC | Kiungo | 3 |
| 19 | Prince Dube | Young Africans SC | Mshambuliaji | 3 |
| 20 | Baraka Filemon | Mbeya City FC | Beki | 3 |
| Nafasi | Mchezaji | Klabu | Nafasi Anayocheza | Asisti |
|---|---|---|---|---|
| 21 | Andrew William | Coastal Union FC | Beki | 2 |
| 22 | Castor Mwangabo | KMC FC | Beki | 2 |
| 23 | Andy Bikoko | Dodoma Jiji FC | Beki / Kiungo | 2 |
| 24 | Lusajo Mwaikenda | Azam FC | Beki | 2 |
| 25 | Kante Alasane | Simba SC | Kiungo | 2 |
| 26 | Mathew Tegisi | Pamba Jiji FC | Mshambuliaji | 2 |
| 27 | David Byrson | JKT Tanzania | Beki | 2 |
| 28 | Shomari Kapombe | Simba SC | Beki | 2 |
| 29 | Datius Peter | Mtibwa Sugar FC | Beki | 2 |
| 30 | Salum Kimenya | Tanzania Prisons | Beki | 2 |
| Nafasi | Mchezaji | Klabu | Nafasi Anayocheza | Asisti |
|---|---|---|---|---|
| 31 | Mwana Kibuta David | Dodoma Jiji FC | Kiungo | 2 |
| 32 | Ammy Mapaka | TRA United | Mshambuliaji | 2 |
| 33 | Anicet Oura | Simba SC | Kiungo | 2 |
| 34 | John Lazarus | TRA United | Beki | 2 |
Hitimisho

Huku ligi ikielekea ukingoni, vita ya takwimu nayo inapamba moto. Ni wazi orodha ya Wakali wa asisti NBC Premier League, ni miongoni mwa takwimu muhimu ambazo huweza kumsaidia mchezaji kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu MVP. Kwa sasa majina ya Allan Okello, Elie Mpanzu na Feisal yamejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda tuzo hiyo, lakini Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama naye anakuja kwa kasi, tusubiri na kuona.

