- Simba SC kikosi cha ushindi 2025/26 NBC Premier League umeongezewa nguvu na wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo
- Clatous Chama amekuwa mhimili eneo la kiungo anashikilia rekodi ya kutwaa tuzo ya Man of the Match mara 5 mfululizo
- Mlinda mlango Mahamadou Kassali ni namba mbili kwa makipa wenye hati safi nyingi ndani ya ligi
Simba SC kikosi cha ushindi 2025/26 NBC Premier League kinajumuisha wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo. Mnyama mzunguko wa pili amekuwa kwenye mwendo bora katika mechi za ushindani. Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo ni Clatous Chama, Nickson Kibabage, Libase Gueye na Anicent Oura. Mchezo uliopita walipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex.
SOMA HII: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa
Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

Simba SC kikosi cha ushindi 2025/26 usajili wa dirisha dogo umeongeza nguvu

SOMA HII:Ratiba ya Simba SC 2025/26 Machi dakika 450 za kazi | Msimamo, matokeo

Mnyama Simba SC kikosi cha ushindi 2025/26 NBC Premier League wachezaji waliotambulishwa dirisha dogo wameonyesha ubora. Langoni Mahamadou Kassali amekuwa na uhakika kikosi cha kwanza. Huyu naye ni usajili wa dirisha dogo akichukua mikoba ya Moussa Camara ambaye atakuwa nje ya uwanja msimu mzima kutokana na kutokuwa fiti.
Kassali anashikilia nafasi ya pili kwa makipa wenye hati safi nyingi akiwa nazo 12. Mshindani wake mkubwa ni Djigui Diarra mlinda mlango wa Yanga SC ambaye anazo 13. Je nani atakuwa kipa bora kwa wababe hawa wote wamebakiwa na mechi 5?
Matokeo ya mechi 5 zilizopita kwa Simba SC NBC Premier League
Mei 6, 2026 Simba SC 1-0 JKT Tanzania
Mei 10, 2026, Simba SC 4-0 Tanzania Prisons
Mei 14, 2026, Mashujaa FC 0-3 Simba SC
Mei 21, 2026, Coastal Union 1-2 Simba SC
Mei 24, 2026, Simba SC 1-0 Dodoma Jiji FC
Chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Steve Barker
Langoni
Mahamadou Kassali
Mabeki
Shomari Kapombe
Nickson Kibabage
Ismail Traore
De Reuck
Viungo
Yusuph Kagoma
Libasse Gueye
Neo Maema
Ellie Mpanzu
Inno Loemba
Clatous Chama
Kwenye kikosi cha kwanza Kassali amekuwa na uhakika kwenye mechi nyingi. Kwa upande wa mabeki Kibabage naye anaingia kwenye orodha. Eneo la kiungo Chama amekuwa mhilimili katika ushindi naye ni ingizo jipya dirisha dogo akitokea Singida Black Stars.
Rekodi za Simba SC katika mechi 5 mfululizo

SOMA HII: Usajili Simba SC umeanza mapema | Orodha na rekodi za wachezaji walioongeza kandarasi unyamani
Mlinda mlango Kassali hati safi 4 akifungwa goli 1.
Clatous Chama Man of the Match mara 4.
Ellie Mpanzu Man of the Match mara 1.
Safu ya ushambuliaji imefunga magoli 10.
Safu ya ulinzi imeruhusu goli 1.
Katika orodha ya wafungaji wenye magoli mengi jina la Chama ambaye ni ingizo jipya dirisha dogo lipo kwenye orodha. Kiungo huyo amefunga magoli 8. Bado mechi 5 kukamilisha msimu wa 2025/26.
Mchezo ujao kwa Simba SC
Kituo kinachofuata katika ratiba ni Juni 14 itakuwa Simba SC vs Pamba Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex. Mchezo wa mzunguko wa kwanza walitoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1. Nani ataibuka mshindi mchezajo ujao? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa.
Pamba Jiji FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 7 baada ya mechi 25. Inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 58. Wababe hawa wawili utakuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili 2025/26.
Hitimisho
Simba SC kikosi cha ushindi 2025/26 NBC Premier League chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker kinatumia mshambuliaji mmoja. Seleman Mwalimu ni mshambuliaji pekee wa asilia ambaye amekuwa akianzia benchi. Kwenye ligi amefunga jumla ya magoli 8 sawa na Clatous Chama.

