
USIKU wa tuzo unatarajiwa kuwa leo Agosti Mosi 2024 ambapo ulimwengu wa mpira utakwenda kushudia nani atakuwa nani baada ya zoezi hilokufika tamati.Gumzo kubwa ni ushindani wa nyota wawili ambao walitimiza majukumu kwa ukamilifu ndani ya timu zao kwenye kusaka pointi tatu hivyo tu basi.
Ikumbukwe kwamba Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) imefanya uteuzi kwenye vipengele mbalimbali kuelekea kwenye tuzo hizo ambazo zilikuwa zinasubiriwa kwa shauku kubwa. Ligi Kuu Tanzania Bara ipo njiani kurejea hivyo zile burudani ambazo zilikuwa zimesimama kwa muda nazo zinarudi upya.
Agosti 16 2024 msimu mpya unatarajiwa kuanza huku Ngao ya Jamii ikitarajiwa kuanza Agosti 8 2024 na hii itaanzia kwenye hatua ya nusu fainali. Kariakoo Dabi itakuwa uwanja wa Mkapa kati ya waliotwaa taji hilo Simba dhidi ya Yanga walipokutana kwenye fainali mwanzo wa msimu wa 2023/24 pale Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Azam FC na Coastal Union watakuwa Uwanja wa New Amaan Complex kwenye nusu fainali atatinga hatua ya fainali kusaka mshindi wa taji la Ngao ya Jamii ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa 2024/25 unaoatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Mabingwa kwa msimu wa 2023/24 ni Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya SportPesa. Ni Toyota Cup Yanga ilitwaa ilipokuwa Afrika Kusini kwenye maandalizi ya msimu mpya kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
USIKU WA TUZO KWENYE MAFUNGU HAYA
- Tuzo za Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB. Ikumbukwe kwamba bingwa wa kombe hili ni Yanga.
- Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake, bingwa ni Simba Queens.
- Tuzo za Ligi Kuu ya NBC, bingwa ni Yanga.
- Tuzo za utawala.
- Tuzo za ligi nyingine.
REKODI ZA NYOTA WANAOWANIA TUZO
REKODI KOMBE LA CRDB

Clement Mzize wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuwa ndani ya kikosi hicho.Mzize naye bado yupo ndani ya kikosi cha Yanga kuelekea msimu wa 2024/25.
Edward Songo wa JKT Tanzania hawa wote walifunga mabao matano kila mmoja akiwa na timu yake ndani ya CRDB Federation Cup ambalo lilitwaliwa na Yanga katika fainali iliyochezwa dhidi ya Ihefu.
KIPA BORA
Djigui Diarra wa Yanga ni yeye alikuwa kwenye fainali alianza kikosi cha kwanza na kukomba dakika zote 120 kwa kuwa dakika 90 ngoma ilikuwa nzito zikaongezwa dakika 30.
Khomein Abubakar wa Ihefu. Ilikuwa ni chaguo la kwanza alifungwa bao moja kwenye mchezo wa fainali na mtupiaji alikuwa ni Aziz Ki.
Mohamed Mustapha wa Azam FC anaingia kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya kipa bora ndani ya CRDB Federation yeye ni kipa namba moja wa Azam FC.
USIKU KWA WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA NA REKODI

- Stephane Aziz Ki wa Yanga huyu alifunga mabao 21 kwenye ligi.
- Feisal Salum wa Azam FC alitupia mabao 19 ndani ya ligi.
Kipre Jr wa Azam FC alitoa jumla ya pasi 9 za mabao na alitupia mabao 10.
4. Djigui Diarra wa Yanga kipa namba moja wa Yanga alicheza mechi 23 alikomba dakika 1,935 cleen sheet 14 alifungwa mabao 10.
5. Ley Matampi wa Coastal Union kinara wa cleen sheet 15 baada ya kucheza mechi 24 za ligi.
6. Yao Kouassi wa Yanga mechi 22 za ligi alicheza akikomba dakika 1,826 alitupia bao moja.
7. Ibrahim Bacca wa Yanga mechi 21 dakika 1,788.
8. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr wa Simba mechi 27 dakika 2,322 pasi za mabao 6.
ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA KIPA BORA NBC
- Ayoub Lakred wa Simba.
2. Djigui Diarra wa Yanga
3. Ley Matampi wa Coastal Union
ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA BEKI BORA

- Yao Kouassi wa Yanga
2. Ibrahim Bacca wa Yanga
3. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr.’ wa Simba
ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA KIUNGO BORA
1. Stephane Aziz Ki wa Yanga
2. Feisal Salum wa Azam FC
3. Kipre Junior wa Azam FC
ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA KOCHA BORA
- David Ouma wa Coastal Union timu yake iligotea nafasi nne kwenye msimamo.
2. Bruno Ferry wa Azam FC timu yake iligota nafasi ya pili kwenye msimamo.
3. Miguel Gamondi wa Yanga timu yake iligotea nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

