- Simba SC 2-2 Yanga SC ndivyo ubao wa matokeo wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ulivyosomeka, mara baada ya dakika 90 za moto jana Jumapili.
- Ni matokeo ya mchezo mkali wa Dabi ya Kariakoo, mchezo namba 164 wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League.
- Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 5.
- Makala hii inachambua matukio 10 makubwa kuhusu dabi hii.
Simba SC 2-2 Yanga SC ulisomeka ubao wa matokeo wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, mara baada ya dakika 90 nzito jana Jumapili. Haya ni matokeo ya mchezo mkali wa Dabi ya Kariakoo, mchezo wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League. Kwa Yanga SC matokeo hayo yanaifanya kujichimbia kileleni mwa ligi kwa tofauti ya pointi 5. Makala hii inachambua matukio 10 makubwa kuhusu dabi hii.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Haya hapa matukio 6 makubwa yaliyotokea kwenye mechi ya Simba SC 2-2 Yanga SC
1. Kariakoo Dabi 2, ndani ya siku 5 tu

Mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Simba SC vs Yanga SC ndio mchezo mkubwa zaidi katika historia ya soka la Tanzania, hivyo ni mchezo ambao ni nadra kuchezwa. Hivyo mchezo huu unaingia katika historia ya kuwa dabi 2, zilizochezwa ndani ya kipindi kifupi zaidi cha siku 5 tu. Ikumbukwe timu hizi zilikutana Aprili 29, 2026 katika fainali ya Muungano Cup ambapo Simba SC waliibuka mabingwa kwa matokeo ya Simba SC 1-0 Yanga SC.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC uso kwa uso Fainali Muungano Cup 2026 | h2h, Ratiba, Matokeo, Takwimu
2. Simba SC 2-2 Yanga SC, Waamuzi wa Kombe la Dunia

Mechi hii imeingia katika rekodi ya kuchezeshwa na Waamuzi wa viwango vya juu kutoka Morocco, wakiongozwa na Hamza El Fareq. Mwamuzi huyo ni miongoni mwa waliochaguliwa kuchezesha Kombe la Dunia 2026. Kila mtu amekuwa na maoni tofauti kuhusu safu hiyo ya waamuzi, lakini wengi wameonyesha kuridhishwa na sehemu kubwa ya maamuzi. Ikumbukwe dabi nyingi, maamuzi ya waamuzi huwa sehemu ya mjadala mkubwa.
3. Goli la Clatous Chama gumzo kubwa

Kiungo Mzambia wa Simba SC, Clatous Chama jana alifunga moja ya mabao bora kabisa kwenye NBC Premier League. Mjadala umekuwa mkubwa kuhusu bao hilo, ambapo wengi wamelielezea kuwa huenda likawa goli bora la msimu. Katika ufungaji wa bao hilo Chama alipokea pasi ya kunyanyua ya Mpanzu, akiwa ameupa mgongo lango, na kufunga kwa mfumo wa ‘acrobatic’ tiki-taka. Muda utaamua kama litakuwa gori bora zaidi la msimu.
Pamoja na goli hilo Chama pia alisaidia upatikanaji wa bao la kwanza kwa kutoa asisti ya bao la, Libasse Gueye. Takwimu hizo zilimfanya Chama kutangazwa, na kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mechi. Ikumbukwe Chama pia alichangia Penalti ya ushindi vs Yanga SC Zanzibar.
4. Mjadala ubora wa Uwanja wa Isamuhyo

Siku moja kabla ya mchezo na siku ya mchezo huu mjadala mkubwa ulizuka juu ya Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, hii ni baada ya kunyesha mvua kubwa jijini Dar es Salaam. Licha ya kuwa na vipimo vikubwa vya eneo la kuchezea, bado kulikuwa na maswali kuhusu kama unakidhi hadhi ya dabi ya Kariakoo. Malalamiko yalihusu ubora wa sehemu ya kuchezea na miundombinu kwa ujumla. Pamoja na maoni hayo, uwanja ulihimili sehemu kubwa ya mchezo japo ni wazi kulikuwa na changamoto kadhaa.
5. Penalti za Libasse Gueye na Laurindo Depu kukataliwa

Licha ya ubora ambao ulionyeshwa na waamuzi waliochezesha mechi hiyo, bado kumekuwa na baadhi ya maamuzi yaliyoonekana kuwa na mapungufu. Miongoni mwa mapungufu hayo, matukio ya kukataliwa kwa kile kilichoonekana ni Penalti za wazi kwa Depu wa Yanga SC na Gueye wa Simba SC. Hii inaendelea kuchagiza mjadala wa uzito wa mchezo na changamoto za kibinaadamu za waamuzi.
SOMA HII PIA: Muungano Cup 2026 Man of The Match Simba SC vs Yanga SC | Matokeo, takwimu | SportPesa Blog
6. Yanga SC kubadilisha nguo nje ya Uwanja

Miongoni mwa matukio ya kushangaza ni lile la wachezaji wa Yanga SC kugoma kutumia vyumba vya Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kubadili nguo. Kikosi hicho kilitumia nyumba mojawapo iliyopo nje ya uwanja huo, hali iliyozua sintofahamu kubwa. Kwakuwa tukio hilo lilifanyika kinyume na Kanuni za ligi, ni wazi Yanga SC watajikuta kwenye hatari ya kupewa adhabu ya faini.
Hitimisho
Matokeo ya Simba SC 2-2 Yanga SC ya mchezo wa Kariakoo Dabi, yameendelea kuthibitisha ubora na ushindani wa mchezo huu. Ikumbukwe pia timu hizi msimu huu zimekutana mara 4, huku kila timu ikishinda mechi 1 na mechi 2 kuisha kwa sare. Kwa matokeo haya vita ya ubingwa sasa ni wazi inampa Yanga SC nafasi kubwa, wakati ambao wapo kileleni kwa tofauti ya pointi 5.

