- Kombe la Dunia la FIFA 2026, limeacha kumbukumbu nyingi za rekodi kali na matukio ya kihistoria ya kukumbukwa.
- Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na nchi 3 za Mexico, USA na Canada yalishuhudia timu ya Taifa ya Hispania ikiibuka bingwa kwa mara ya pili katika historia yake.
- Hii ni baada ya matokeo ya Spain 1-0 Argentina kwenye fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa MetLife, au Ney York New Jersey, USA.
- Makala hii inagusia baadhi ya rekodi na takwimu za Kombe la Dunia 2026.
Kombe la Dunia la FIFA 2026, litaendelea kukumbukwa kwa muda mrefu kutokana na kuvunja rekodi nyingi na kushuhudia matukio ya kipekee ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya mashindano hayo. Mashindano hayo yalishuhudia timu ya Taifa ya Hispania ikiibuka bingwa wa dunia, kwa mara ya pili katika historia yake. Hii ni baada ya kuichapa Argentina bao 1-0, kwenye fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa MetLife, au Ney York New Jersey, USA. Makala hii inagusia baadhi ya rekodi na takwimu za Kombe la Dunia 2026.
FIFA Kombe la Dunia 2026: Rekodi ya Fedha za zawadi

Kati ya jumla ya dola za Marekani milioni 871 sawa na zaidi ya Bilioni 300 za kitanzania, zilitengwa na FIFA kama Zawadi. Argentina iliyomaliza nafasi ya pili ilijinyakulia zaidi ya Bilioni 89, England iliyomaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Ufaransa, ilipata zaidi ya Bilioni 79. Kwa kuifunga Argentina baada ya muda wa nyongeza, Hispania ilijishindia kitita cha zaidi ya Bilioni 134. Fedha hizo ni Zawadi ya kihistoria kulinganisha na Zawadi za Kombe la Dunia 2022.
KUJUA REKODI YA MAPATO YA KOMBE LA DUNIA 2026, SOMA HII: FIFA Kombe la Dunia 2026 limeweka rekodi mpya ya mapato
Timu 48, mechi 104
Kombe la Dunia la 2026 pia lilikuwa la kwanza katika historia kushirikisha timu 48, ikiwa ni ongezeko la timu 12 kutoka mashindano yaliyopita, hatua iliyolenga kuongeza ushiriki wa mataifa mengi zaidi duniani. Ongezeko hilo la timu pia lilichangia kuwekwa kwa rekodi mpya ya michezo mingi zaidi ambapo mechi 104 zilipigwa. Hii ni hesabu ya michezo ya kuanzia hatua ya makundi hadi fainali iliyopigwa Uwanja wa New York New Jersey.
Mabao na Asisti

Rekodi nyingine kali ni ya kufungwa kwa mabao 308 katika mechi hizo 104. Nahodha wa safu ya ushambuliaji ya Ufaransa, Kylian Mbappe, aliweka rekodi mpya kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kufunga mabao 10 kwenye mashindano ya mwaka 2026. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid sasa ana jumla ya mabao 22 katika Kombe la Dunia, bao moja zaidi ya Lionel Messi. Mchezaji mwenzake Michael Olise pia aliweka rekodi nyingine kwa kutoa asisti saba, idadi kubwa zaidi kuwahi kufikiwa katika Makala moja ya mashindano hayo.
Messi naye alifunga mabao nane katika Kombe la Dunia la 2026, na kuwa mchezaji aliyefanikiwa kupiga chenga nyingi zaidi katika mashindano yote. Akiwa na umri wa miaka 39 na siku 21, Messi aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa zamani zaidi wa nafasi za uwanjani (outfield player), kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia, katika mchezo dhidi ya England. Bao lake dhidi ya Jordan katika hatua ya makundi, lilimfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga katika mechi saba mfululizo za Kombe la Dunia.
Rekodi mbovu ya upinzani ya Fainali

Licha ya kiwango bora cha Lionel Messi kwenye mashindano hayo, Argentina iliweka rekodi mbaya baada ya kushindwa kupiga hata shuti moja lililolenga lango ndani ya dakika 90 za fainali dhidi ya Hispania. Jambo hili halikuwahi kutokea katika historia ya fainali za Kombe la Dunia.
KUHUSU RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Rekodi ya Didier Deschamps
Kwa upande wa benchi la ufundi, kocha wa Ufaransa Didier Deschamps aliendelea kuweka historia. Baada ya kuwa mtu wa kwanza kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na baadaye kocha. Kocha huyo sasa ameweka rekodi mpya ya kuwa kocha mwenye ushindi mwingi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia, akifikisha jumla ya ushindi wa mechi 19.
Vozinha wa Cape Verde asepa na kijiji

Kipa wa Cape Verde, Voizinha, alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuizuia Hispania kufunga katika mechi ya kwanza kabisa ya taifa hilo kwenye Kombe la Dunia. Kufuatia kiwango hicho bora kipa huyo aliyekuwa na wafuasi takribani 50,000 tu kwenye mtandao wa Instagram alipata wafuasi wapya milioni 10 ndani ya masaa 24 tu na mpaka Makala hii inaandikwa alikuwa na wafuasi Milioni 29.6. Kuonyesha kuwa hakubahatisha kipa huyo alionyesha tena kiwango bora kwenye mchezo vs Argentina licha ya kupoteza kwa kichapo cha mabao 3-2. Hata hivyo, kipa wa Paraguay Orlando Gill ndiye aliyeokoa michomo mingi zaidi akifanya hivyo mara 28.
KUHUSU UCHAMBUZI WA MATOKEO YA MECHI YA FAINALI, SOMA HII: Hispania 1-0 Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026| Ferran Torres afunga bao la ushindi
Hitimisho
FIFA Kombe la Dunia 2026 linabaki kuwa miongoni mwa matamasha yaliyoacha rekodi kubwa zisizofutika. Ni miaka 4 ijayo ndiyo panapo majaaliwa ya uhai, huenda tukashuhudia rekodi mpya zikiandikwa. Tuandikie je ni rekodi gani kali ya Kombe la Dunia unaikumbuka? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

