- Arsenal vs Atletico Madrid ni mechi ya kufa na kupona itakayopigwa kesho Jumanne, kwenye Uwanja wa Emirates.
- Huu ni mchezo wa mkondo wa pili ya UEFA Champions League.
- Mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Wanda Metropolitano, uliisha kwa matokeo ya Atletico Madrid 1-1 Arsenal.
- Mshindi wa jumla wa mechi hii atafuzu fainali ya mashindano hayo, ambapo atavaana na mshindi wa mechi ya Bayern Munich vs Paris Saint-Germain.
Arsenal vs Atletico Madrid mechi ya kufa na kupona itakayopigwa kesho Jumanne, kwenye Uwanja wa Emirates. Ni mechi ya mkondo wa pili ya UEFA Champions League. Ikumbukwe mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Wanda Metropolitano uliisha kwa matokeo ya Atletico Madrid 1-1 Arsenal. Mshindi wa jumla wa mechi hii atafuzu fainali ya mashindano hayo, ambapo atavaana na mshindi wa mechi ya Bayern Munich vs Paris Saint-Germain.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya UEFA Champions League 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Arsenal vs Atletico Madrid h2h

Bado hakuna mbabe kati ya wapinzani hawa, Arsenal na Atletico Madrid wamecheza jumla ya mechi 4 katika historia ya soka la ushindani. Kila timu imeshinda mechi 1, huku mechi 2 zikiisha kwa matokeo ya sare. Mara ya mwisho kukutana mechi iliisha kwa sare ya bao 1-1.
SOMA HII PIA: Arsenal Fixtures: Men’s, Women’s and Academy Football in England
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza Arsenal vs Atletico Madrid
Arsenal

Kipa: Raya
Walinzi: White, Saliba, Gabriel, Hincapie
Viungo: Rice, Zubimendi, Saka, Eze, Trossard
Mshambuliaji: Gyokeres
Atletico Madrid

Kipa: Oblak;
Walinzi: Llorente, Pubill, Hancko, Ruggeri
Viungo: Simeone, Koke, Cardoso, Lookman
Washambuliaji: Alvarez, Griezmann
SOMA HII ZAIDI: Atletico Madrid vs Arsenal UEFA Champions League Semi-final: Livescore, h2h, lineups, prediction, na taarifa za timu
Habari za timu
Mchezo wa kwanza baina ya timu hizi wiki iliyopita ulikuwa na penalti 2, ambapo uliisha kwa sare ya 1-1 nchini Hispania. Hali hii imewapa faida ndogo kikosi cha Mikel Arteta, kuelekea mchezo wao mkubwa zaidi Ulaya ndani ya miaka 20. Viktor Gyokeres na Julian Alvarez walifunga penalti zao kila mmoja kabla na baada ya mapumziko.
Arsenal bado hawajapoteza mechi yoyote katika Ligi ya Mabingwa msimu huu wa 2025-26, wanaweza kuweka rekodi mpya ya klabu kucheza mechi nyingi bila kupoteza (14). Mechi yao ya mwisho, Arsenal waliifunga Fulham 3-0, ushindi uliowaweka kileleni mwa Ligi Kuu ya England wakiwa na tofauti ya pointi sita dhidi ya Manchester City. Arsenal wamepoteza mechi moja tu, kati ya 15 walizocheza nyumbani dhidi ya timu za Hispania katika mashindano ya UEFA.
Kwa upande wa Atletico Madrid, msimu mwingine bila taji unawanyemelea kama hawatafanya vizuri Emirates. Tayari walishapoteza fainali ya Copa del Rey dhidi ya Real Sociedad, huku kwenye La Liga wakisalia nafasi ya nne wakati Barcelona wakikaribia kutwaa ubingwa. Simeone alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi (wachezaji 11), dhidi ya Valencia kwenye mechi iliyopita ya ushindi wa 2-0.
Taarifa za majeruhi wa vikosi
Arsenal
Bukayo Saka aling’ara dhidi ya Fulham akifunga na kutoa pasi ya bao, lakini alitolewa mapema kama tahadhari kwa ajili ya mechi hii. Arteta pia anasubiri hali za Martin Odegaard (goti) na Kai Havertz (misuli). Jurrien Timber na Mikel Merino wataeendelea kukosekana. Martin Zubimendi anatarajiwa kurejea kikosi cha kwanza baada ya kupumzishwa, pamoja na Piero Hincapie kuchukua nafasi ya beki wa kushoto.
Atletico Madrid

Kwa upande wa Atletico, Julian Alvarez anaonekana yuko sawa licha ya kupata maumivu mechi ya kwanza na anatarajiwa kuanza. Alvarez aliweka rekodi mpya kwa kuwa Muargentina wa haraka zaidi kufikisha mabao 25 katika Ligi ya Mabingwa (mechi 41), akivunja rekodi ya Lionel Messi. Wachezaji wengine kama, Giuliano Simeone, Alexander Sorloth na Jose Gimenez wako kwenye kikosi, huku Pablo Barrios na Nico Gonzalez ndio wachezaji pekee watakaokosekana.
SOMA HII PIA: Arsenal FC muhtasari, ratiba, matokeo, habari za usajili, msimamo wa ligi na takwimu
Utabiri na hitimisho
Arsenal vs Atletico Madrid ni mchezo mgumu sana kutokana na umuhimu wa matokeo mazuri kwa kila timu, na mizania yao. Arsenal watakuwa nyumbani, hivyo wanatabiriwa kuwa nafasi kubwa ya kufanya vizuri. Arsenal hawakuwa na nafasi ya kupumzisha kikosi chao kama Atletico, lakini huenda hilo likawa faida kwao kwani wachezaji wao muhimu wako kwenye kiwango kizuri.

