Yanga SC vs Simba SC (-)Yanga SC vs Simba SC (-)
  • Yanga SC vs Simba SC wanakutana uso kwa uso katika Fainali ya Muungano Cup 2026, itakayopigwa 29/4/2026.
  • Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar saa 2:15 usiku.
  • Mchezo huu wa Dabi ya Kariakoo, unasubiriwa kwa hamu na ushindani mkubwa, hasa baada ya matokeo ya Yanga SC 0-0 Simba SC walipokutana mara ya mwisho.
  • Fainali hii imekuja baada ya matokeo ya Yanga SC 2-1 Azam FC, na  Mlandege FC 0-3 Simba SC katika hatua ya Nusu Fainali.

Hatimaye ni Yanga SC vs Simba SC wanaokutana uso kwa uso katika Fainali ya Muungano Cup 2026, itakayopigwa 29/4/2026. Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Mchezo huu ambao unajulikana kama Kariakoo dabi, unasubiriwa kwa hamu na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Wananchi watangulia Fainali kwa matokeo ya Yanga SC 2-1 Azam FC, Huku Mnyama akiwafuata kwa kuwachapa Mlandege FC 0-3 Simba SC katika hatua ya Nusu Fainali.

Endelea kufuatilia mwenendo ya mashindano ya Muungano Cup 2026 na mashindano mengine, na uweke ubashiri wako kupitia mechi za Odds kubwa kwa kubonyeza wino huu wa bluu SportPesa.

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.
Aviator: Paisha Kindege cha SportPesa ushinde zaidi ya 800,000,000

Kuhusu fainali ya Muungano Cup 2026, Yanga SC vs Simba SC  

Goli la Mwalimu vs Mlandege
Goli la Mwalimu vs Mlandege

Yanga SC vs Simba hii ni mechi ya kihistoria ya Dabi ya Kariakoo, katika mashindano ya Kombe la Muungano Cup. Mechi hii itakayopigwa Jumatano ya 29/4/2026 itachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, kuanzia majira ya saa 2:15 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Yanga SC wanaingia katika mchezo huu kama mabingwa watetezi, huku watani zao Simba SC Wakisaka kuivua ubingwa Yanga SC.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League: Nassoro Mwinchui mwamuzi wa kati, utabiri

Njia ya Yanga SC kufika Fainali Muungano Cup 2026

Yanga SC vs Simba SC
Dube na Maxi

Yanga SC imekuwa timu ya kwanza kutinga Fainali ya Muungano Cup 2026, ambapo safari yao katika mashindano hayo ilianza kwa matokeo ya Yanga SC 4-0 Muembe Makumbi City.  Matokeo hayo yaliwapeleka Yanga SC kutinga Nusu Fainali ambapo walivaana na Azam FC, ambapo matokeo yalikuwa Yanga SC 2-1 Azam FC. Yanga SC wameingia fainali kwa mara ya 2 mfululizo, ambapo wana kazi kubwa ya kutetea ubingwa wao mbele ya Mnyama.

Njia ya Simba SC kufika Fainali Muungano Cup 2026

Mbegu vs Mlandege FC
Mbegu vs Mlandege FC

Safari ya Simba SC katika mashindano ya Muungano Cup 2026, ilianza kwa matokeo ya ushindi ya Simba SC 1-0 Mafunzo SC. Katika hatua ya Nusu Fainali Simba SC walivaana Mlandege FC, mpaka dakika 90 zinakamilika ubao ulisoma Mlandege FC 0-3 Simba SC. Mara baada ya kujitoa kwenye mashindano hayo kutokana na ratiba nyingine, msimu huu Simba SC wanaonekana kupania kushinda taji hilo.

SOMA HII ZAIDI: Yanga SC 0-0 Simba SC: Semaji Ahmed, Ali Kamwe watoa matamko mazito kumhusu Refa wa Kariakoo dabi, matokeo, msimamo

Dabi za Kariakoo 2 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar 2026

Yanga SC vs Simba SC
Yanga SC vs Simba SC

Fainali hii ya Muungano Cup 2026, inathibitisha rekodi ya kufanyika kwa mechi 2 za Dabi ya Kariakoo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar mwaka 2026. Dabi ya Kariakoo ya kwanza ilikuwa ni ya Ligi Kuu ya NBC Premier League iliyopigwa Machi 1, 2026. Katika mchezo huo ambao Wananchi walikuwa nyumbani, matokeo yalikuwa Yanga SC 0-0 Simba SC.

Yanga SC vs Simba SC, H2H

Majedwali haya hapa chini yanaeleza takwimu za mechi 7 zilizopita za Yanga SC vs Simba SC;

KipengeleSimba SCYoung Africans SC (Yanga)
Jumla ya Mikutano ya karibuni77
Sare11
Mechi 6 za MwishoUshindi 0Ushindi 6
Nafasi ya Sasa Ligi Kuu NBCNafasi ya 2Nafasi ya 1
TareheMashindanoMatokeo
1 Machi 2026Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 0–0 Simba
16 Septemba 2025Kombe la ShirikishoYanga 1–0 Simba
25 Juni 2025Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 2–0 Simba
19 Oktoba 2024Ligi Kuu Tanzania BaraSimba 0–1 Yanga
8 Agosti 2024Kombe la ShirikishoYanga 1–0 Simba
20 Aprili 2024Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 2–1 Simba
5 Novemba 2023Ligi Kuu Tanzania BaraSimba 1–5 Yanga

Yanga SC vs Simba SC Fainali Muungano Cup 2026 mshindi kuzoa Tsh. 150 Milioni

Waziri Mhe- Hamza
Waziri Mhe- Hamza

Mshindi wa fainali ya Muungano Cup 2026 kati ya Yanga SC vs Simba SC ataondoka na zawadi ya Tsh. milioni 150, pia mshindi wa pili atapata Sh milioni 100, jambo linaloongeza presha na ushindani mkubwa katika mchezo huo. Lakini kwa timu hizi kushinda mchezo kuna maana kubwa ya heshima na rekodi.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC kazini leo NBC | Ratiba NBC Premier League na msimamo hii hapa

Hitimisho

Yanga SC vs Simba SC ni zaidi ya mchezo wa Fainali, hii ni vita ya heshima baada ya majigambo ya muda mrefu ya pande zote mbili. Fainali ya Muungano Cup 2026 inatarajiwa kuwa sura nyingine ya kusisimua katika historia ndefu ya upinzani kati ya vigogo wakubwa wa soka la Tanzania. Inatarajiwa Mashabiki wengi ndani na nje ya nchi, watakuwa wakifuatilia kwa karibu kuona nani atatawala tena Kariakoo Derby.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya NBC Premier League 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.