- Mashindano ya Muungano Cup 2026 yanaendelea tena leo Alhamisi, huko visiwani Zanzibar, mechi 2 kali za Robo Fainali zinapigwa.
- Huku matokeo ya Mlandege FC 2-1 Singida BS yakishtua wengi, matokeo hayo yanamaanisha Mlandege FC wamefuzu moja kwa moja Nusu Fainali.
- Mchezo unaofuata sasa ni Simba SC vs Mafunzo SC, Mnyama akisaka tiketi ya Nusu Fainali.
- Huku Simba SC ikianza kampeni yake; Libasse Gueye, Anicet Oura na Elie Mpanzu watabiriwa makubwa kwenye michuano hiyo, hizi hapa takwimu zao.
Muungano Cup 2026 inaendelea tena leo Alhamisi, huko visiwani Zanzibar. Mechi 2 kali za Robo Fainali zinapigwa, ambapo mchezo wa kwanza umeshuhudia Mabingwa Ligi Kuu Zanzibar, Mlandege FC wakiichapa Singida BS 2-1. Mchezo wa pili ni Simba SC vs Mafunzo SC, Mnyama akisaka tiketi ya Nusu Fainali. Baada ya kuuwasha moto kwenye NBC Mastaa wa Simba SC; Libasse Gueye, Anicet Oura na Elie Mpanzu wanatajwa kuwa mastaa wa kuchungwa zaidi kwenye michuano hiyo. Makala hii inachambua ubora wa Nyota hao.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Muungano Cup 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Elie Mpanzu

Huyu ni nyota wa kimataifa wa Simba SC raia wa DR Congo, akiwa na umri wa miaka 24 tu, amekuwa kipenzi kikubwa cha Wanasimba. Huu ni msimu wake wa 2 akiwa na Simba SC aliyojiunga nayo msimu wa 2024/2025 na kufanya makubwa kwenye msimu wa kwanza. Hali ilianza tofauti msimu huu, ni baada ya staa huyo kuanza vibaya msimu jambo ambalo linatajwa kuchangiwa zaidi na changamoto za kifamilia.
Mpanzu anayetumia miguu yote miwili anamudu kucheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni ‘Winger’. Licha ya kuwa na msimu mgumu, lakini Mpanzu ni miongoni mwa wachezaji walio na takwimu bora zaidi ndani ya Simba SC mpaka sasa. Mpanzu amehusika kwenye mabao 8 akifunga mabao 3 na kuasisti mara 5. Anaonekana kurejea kwenye kai yake na anatarajiwa kufanya makubwa Muungano Cup 2026, akiwa ni mmoja wa mastaa waliotua Zanzibar.
SOMA HII PIA: Muungano Cup 2026 | Ratiba, Simba SC, Yanga SC kukiwasha Robo Fainali
Anicet Oura

Huyu ni Nyota wa kimataifa wa Ivory Coast, ambaye alikamilisha usajili wake ndani ya Simba SC 26/1/2026. Licha ya usajili wake kubezwa na wengi, Oura mwenye umri wa miaka 26 amekuwa na kiwango bora akitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi kwa sasa. Kwenye Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), Oura ameifungia Simba mabao 3, lakini akiwa na wastani wa jumla wa kuichangia Simba zaidi ya mabao 5. Nyota huyo anatabiriwa kuwa miongoni mwa wale watakaoshindania kiatu cha ufungaji bora.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC | Dabi ya Kariakoo hatihati kupigwa Fainali Muungano Cup 2026, Ratiba, matokeo, kuwagonganisha
Libasse Gueye

Huyu ni Nyota wa kimataifa wa Senegal, ambaye alizaliwa katika mji wa Guinguineo tarehe 05/07/2003. Akiwa na umri wa miaka 22 tu, tayari amefanikiwa kuandika jina lake katika historia ya Ligi ya Tanzania Bara (NBC), Premier League. Hii ni mara baada ya kuonyesha kiwango bora tangu aliposajiliwa dirisha dogo la mwezi Januari mwaka huu. Gueye mwenye urefu wa mita Futi 5.68 anamudu kwa usahihi kucheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni ‘Winger’.
Gueye alijiunga na Simba rasmi Januari 17, 2026 na kusaini mkataba wa miaka 2 na Simba SC akitokea Teungueth FC. Silaha yake kubwa ni kasi, na matumizi sahihi ya mguu wake wa kushoto wenye maajabu ya chenga. Tangu ajiunge na Simba SC ameifungia mabao 4 ikiwemo bao kali vs Namungo FC, uwezo wake katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo vs Yanga SC Machi 1, 2026 itabaki kuwa ya kukumbukwa.
Libasse ni miongoni mwa mastaa wa Simba SC ambao wamesafiri na kikosi, na kuwasili Zanzibar. Ni kwa ajili ya mashindano ya Muungano Cup 2026, ambapo anatabiriwa kufanya makubwa.
Endelea kubashiri mechi za mashindano mbalimbali zenye odds kubwa kwa kubonyeza wino huu wa bluu SportPesa
Hitimisho
Mapinduzi Cup 2026 imezidi kupamba moto, tayari timu za Yanga SC, Mlandege FC na Azam FC zimetinga Nusu Fainali. Simba kuanza kibarua chake kwa kuvaana na Mafunzo SC, ambapo kikosi hiko kinajivunia ukubwa wa kikosi chake. Baada ya kufanya makubwa kwenye NBC Premier League, je Nyota hao wataonyesha ubabe Zanzibar.

