Ratiba ya Ligi Kuu EngladRatiba ya Ligi Kuu Englad
  • Ratiba ya Ligi Kuu England 2026/27 rasmi imetolewa, huku mechi nyingi zikionekana ni za moto.
  • Mabingwa watetezi Arsenal wataanza kampeni ya kutetea ubingwa dhidi ya Coventry City, Agosti 21, 2026 katika Uwanja wa Emirates.
  • Manchester United wao wataanza msimu kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Hull City siku ya Jumamosi, Agosti 22, 2026. Man City itawakaribisha Bournemouth kwenye Uwanja wa Etihad.
  • Makala hii inakuchambulia kwa ufupi mambo muhimu kuhusu ratiba hiyo

Ratiba ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2026/27 imetangazwa rasmi, huku mabingwa watetezi Arsenal wakianza kampeni yao nyumbani dhidi ya Coventry City, Agosti 21, 2026 katika Uwanja wa Emirates. Manchester United wao wataanza msimu kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Hull City siku ya Jumamosi, Agosti 22, 2026. Majirani zao Manchester City itawakaribisha Bournemouth kwenye Uwanja wa Etihad. Mechi nyingine ni Liverpool vs Newcastle United, na Chelsea ikihitimisha raundi ya kwanza kwa derby ya London dhidi ya Fulham siku ya Jumatatu, Agosti 24.

Ratiba ya Ligi Kuu England 2026/27: Arsenal yaanza kutetea ubingwa, Man United vs Hull City

EPL Ratiba ya Ligi Kuu England 2026/27
EPL Ratiba ya Ligi Kuu England

Arsenal, mabingwa wa Ligi Kuu England, wataanza rasmi harakati za kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Coventry City, timu iliyorejea EPL baada ya kupanda daraja. Katika ratiba iliyotolewa, Coventry itacheza mechi hiyo ya kwanza ya ligi kuu baada ya miaka 25 dhidi ya Arsenal. Ikumbukwe The gunners walitwaa ubingwa wao wa kwanza wa Premier League, tangu mwaka 2004 chini ya kocha Mikel Arteta.

Manchester United, ambayo sasa ipo chini ya kocha Michael Carrick kwa msimu mzima, itakuwa na matumaini ya kuwania ubingwa baada ya kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita. Safari yao itaanza kwa mchezo dhidi ya Hull City katika Uwanja wa MKM. Wakati huu timu hiyo inaendelea na mechi zake za kabla ya msimu.

Kujua msimamo wa msimu uliopita soma hii; Premier League Table & Standings 2025-2026 Season

Manchester City, Liverpool zaongoza timu zenye makocha wapya

Manchester City itaanza maisha bila Pep Guardiola, kwa kuikaribisha Bournemouth tarehe 23 Agosti. Bournemouth pia inaanza msimu ikiwa na kocha mpya, Marco Rose. Liverpool nayo itaanza enzi mpya chini ya kocha Andoni Iraola, aliyechukua nafasi ya Arne Slot, kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Newcastle United. Chelsea pia inaanza kipindi kipya chini ya kocha Xabi Alonso, ambaye ataanza kazi yake kwa derby ya London Magharibi dhidi ya Fulham.

Wakati huo huo mechi nyingine ni pamoja na:

Brentford vs Tottenham Hotspur.

Everton vs Crystal Palace.

Nottingham Forest vs Leeds United

Brighton vs Aston Villa, mabingwa wa Europa League.

Maswali muhimu kutoka kwenye ratiba ya EPL 2026/27

Derby ya kwanza ya Manchester itachezwa lini?

Manchester Derby
Manchester Derby

Derby ya kwanza ya Manchester United vs Manchester City baada ya kuondoka kwa Pep Guardiola itachezwa mwishoni mwa wiki ya Septemba 13, huku Manchester United ikiwa mwenyeji katika Uwanja wa Old Trafford. Carrick atakuwa akitafuta ushindi muhimu dhidi ya wapinzani wao wa jadi, kabla ya safari kubwa ya kwenda Anfield kuikabili Liverpool tarehe Novemba 21. Msimu uliopita, Manchester United iliifunga Manchester City mabao 2-1 katika Uwanja wa Etihad kwa mabao ya dakika za mwisho kutoka kwa Bruno Fernandes na Amad Diallo kabla ya timu hizo kutoka sare tasa katika mchezo wa marudiano Old Trafford.

Derby ya Kaskazini mwa London itachezwa lini?

Derby ya kwanza ya Tottenham Hotspur vs Arsenal itachezwa tarehe 5 Desemba 2026 katika Uwanja wa Tottenham Hotspur. Tottenham itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na hamu ya kujibu, baada ya kunusurika kushuka daraja msimu uliopita. Arsenal ndiyo iliyo na rekodi bora baada ya kushinda mechi zote mbili za ligi dhidi ya Spurs msimu uliopita kwa mabao 4-1 nyumbani na ugenini. Katika ushindi wa Emirates, Eberechi Eze alifunga hat-trick, huku Viktor Gyokeres akiwa nyota wa mchezo wa marudiano, mechi ya marudiano ya msimu mpya itachezwa Emirates tarehe Mei 1, 2027.

Manchester United dhidi ya Liverpool itachezwa lini?

Baada ya kucheza dhidi ya Manchester City mwezi Oktoba na Arsenal mwishoni mwa mwezi huo, Manchester United itasafiri kwenda Anfield kuikabili Liverpool Jumamosi, Novemba 21, 2026. United itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kujiamini, baada ya kuifunga Liverpool mara mbili msimu uliopita. Walishinda 2-1 Anfield kabla ya kupata ushindi mwingine wa kusisimua wa mabao 3-2 Old Trafford, ambapo Kobbie Mainoo alifunga bao la ushindi dakika ya 77. Liverpool itarejea Old Trafford kwa mchezo wa marudiano, tarehe Januari 23.

Arsenal dhidi ya Chelsea itachezwa lini?

Chelsea vs Arsenal
Chelsea vs Arsenal-Credit fabrizio Romano

Mchezo mkubwa wa kwanza wa kuwania ubingwa utachezwa tarehe Septemba 5, 2026, Arsenal itakapowakaribisha Chelsea katika dimba la Emirates. Arsenal ina faida ya kisaikolojia baada ya kukusanya pointi nne dhidi ya Chelsea msimu uliopita, ikiwemo ushindi wa mabao 2-1 ulioshuhudia Pedro Neto akipewa kadi nyekundu. Chelsea itakuwa na nafasi nzuri ya kuonyesha kuwa, inaweza kushindana kwa ubingwa chini ya kocha mpya Xabi Alonso.

Kujua taarifa mbalimbali za Chelsea, Soma hii: Chelsea FC: Habari za Hivi Karibuni, Ratiba, Taarifa ya Kikosi na Maarifa ya Kubashiri

Mechi Nyingine Kubwa za Msimu

Septemba 19, 2026: Manchester City vs Arsenal – pambano la mapema la kuwania ubingwa.

Siku hiyo hiyo Everton itaikaribisha Liverpool katika derby ya kwanza ya Merseyside kwenye Uwanja mpya wa Hill Dickinson.

Oktoba 24, 2026: Chelsea vs Tottenham Hotspur katika Stamford Bridge.

Ratiba ya Msimu

Kutokana na Kombe la Dunia la FIFA 2026 lililopanuliwa kuwa na timu 48, msimu wa Premier League utaanza wiki moja baadaye kuliko kawaida.

Msimu wa 2026/27 utakuwa na:

  • Wikiendi 33 za mechi.
  • Raundi tano za mechi za katikati ya wiki.
  • Ratiba imepangwa ili kuepuka migongano na mashindano ya UEFA kadri inavyowezekana.
  • Katika kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya, kila klabu itapata angalau saa 60 za mapumziko kati ya mechi mbili.
  • Kutakuwa pia na idadi kubwa ya mechi siku ya Boxing Day kuliko ilivyokuwa misimu iliyopita.
  • Msimu utamalizika tarehe 30 Mei 2027, ambapo:

Arsenal itacheza nyumbani dhidi ya Brighton.

Manchester City itakuwa ugenini dhidi ya Sunderland.

Liverpool itaikaribisha Bournemouth.

Chelsea itawakaribisha Brentford.

Manchester United itamaliza msimu nyumbani dhidi ya Fulham.

Ratiba ya Raundi ya Kwanza (Agosti 21–24, 2026)

Ijumaa, Agosti 21, 2026

Arsenal vs Coventry City – Emirates Stadium – Saa 4:00 Usiku (EAT)

Jumamosi, Agosti 22, 2026

Hull City vs Manchester United – MKM Stadium – Saa 8:30 Mchana (EAT)

Ipswich Town vs Sunderland – Portman Road – Saa 11:00 Jioni (EAT)

Everton vs Crystal Palace – Goodison Park – Saa 11:00 Jioni (EAT)

Nottingham Forest vs Leeds United – City Ground – Saa 11:00 Jioni (EAT)

Brentford vs Tottenham Hotspur – Gtech Community Stadium – Saa 1:30 Usiku (EAT)

Jumapili, Agosti 23, 2026

Brighton vs Aston Villa – Amex Stadium – Saa 10:00 Jioni (EAT)

Manchester City vs Bournemouth – Etihad Stadium – Saa 10:00 Jioni (EAT)

Newcastle United vs Liverpool – St James’ Park – Saa 12:30 Usiku (EAT)

Jumatatu, Agosti 24, 2026

Fulham vs Chelsea – Craven Cottage – Saa 4:00 Usiku (EAT)

Hitimisho

Ratiba ya Ligi Kuu Englad
Ratiba ya Ligi Kuu Englad

Ratiba ya Ligi Kuu England 2026 inatoa taswira ya msimu utakaokuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya michezo mikubwa ya mapema. Arsenal wana kibarua kizito cha kutunza furaha ya mashabiki wao, kwa kupambana kutetea ubingwa. Lakini timu nyingi kubwa zinatarajiwa kuwa makocha wapya na swali ni je, wataanza na matokeo gani? Fuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

KUJUA TAARIFA MBALIMBALI ZA ARSENAL SOMA HI: Arsenal FC muhtasari, ratiba, matokeo, habari za usajili, msimamo wa ligi na takwimu

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.