Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SCSeleman Mwalimu (-)
  • Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026, Uwanja wa New Amaan Complex
  • Seleman Mwalimu Gomez afunga goli la ushindi kwa mkwaju wa penati dakika za jioni
  • Matokeo ya Yanga SC vs Simba SC, Aprili 29 Kombe la Muungano
  • Kituo kinachofuata Mei 3, 2026, Simba SC vs Yanga SC, NBC Premier League

Mwisho wa yote Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026 ni matokeo rasmi mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex. Goli pekee la ushindi limefungwa na Seleman Mwalimu Gomez dakika ya 120+4 kwa mkwaju wa penati. Msababishaji ni Clatous Chama alichezewa faulo na Edmund John dakika ya 118.

SOMA HII: Matokeo ya Muungano Cup 2026 |Wafungaji vinara | Man of The Match

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026

Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026
Diara mlinda mlango wa Yanga SC mchezo wa fainali.

Hatimaye Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026 mchezo ukichezwa dakika 120. Dakika 90 za mwanzo ngoma ilikuwa 0-0. Ni Dicksen Mimisa mwamuzi kutoka Kenya aliamuru ipigwe penalty dakika za jioni.

Simba SC inawavua ubingwa Yanga SC waliokuwa wanatetea taji hilo baada ya kutwaa 2025. Dabi ya Kariakoo haijaisha wanatarajiwa kukutana tena Mei 3, 2026. Huu utakuwa mchezo wa NBC Premier League Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.

Man of The Match ni De Reuck beki wa Simba SC. Ibrahim Bacca beki wa Yanga SC amechaguliwa kuwa mchezaji aliyeonyesha mchezo wa kiungwana. Wababe hawa wamemaliza kazi Zanzibar watakutana Bara.

Matokeo Muungano Cup 2026

TimuTareheMechiHatuaMatokeo
Yanga SCAprili 21, 2026Yanga SC vs Muembe MakumbiRobo fainaliYanga SC 4-0 Muembe Makumbi
Aprili 25, 2026Yanga SC vs Azam FCNusu fainaliYanga SC 2-1 Azam FC
Aprili 29, 2026Yanga SC vs Simba SCFainaliYanga SC 0-1 Simba SC
Azam FCAprili 22, 2026KVZ vs Azam FCRobo fainaliKVZ 0-2 Azam FC
Aprili 25, 2026Yanga SC vs Azam FCNusu fainaliYanga SC 2-1 Azam FC
Simba SCAprili 23, 2026Simba SC vs Mafunzo SCRobo fainaliSimba SC 1-0 Mafunzo SC
Aprili 26, 2026Mlandege FC vs Simba SCNusu fainaliMlandege FC 0-3 Simba SC
Aprili 29, 2026Yanga SC vs Simba SCFainaliYanga SC 0-1 Simba SC
Mlandege FCAprili 23, 2026Mlandege FC vs Singida Black StarsRobo fainaliMlandege FC 2-1 Singida Black Stars
Aprili 26, 2026Mlandege FC vs Simba SCNusu fainaliMlandege FC 0-3 Simba SC

SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Ratiba, Simba SC, Yanga SC kukiwasha Robo Fainali

image

Takwimu za magoli

Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026
Dube Prince mshambuliaji wa Yanga SC.
TimuMechi zilizochezwaMagoli yaliyofungwaMagoli yaliyofungwa dhidi yao
Yanga SC261
Azam FC232
Simba SC250
Mlandege FC224

SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo

Hitimisho

Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026 baada ya jasho kuvuja. Mwisho wa ubishi mnyama ametwaa taji la kwanza msimu wa 2025/26. Kazi haijaisha Kariakoo Dabi nyingine ni Jumapili, Mei 3, 2026. Je kisasi kitalipwa ndani ya NBC Premier League?

Share this: