- Matokeo ya Muungano Cup 2026 na wafungaji vinara
- Mlandege FC 0-3 Simba SC, Yanga SC 2-1 Azam FC ni matokeo hatua ya nusu fainali
- Mashindano yalizinduliwa rasmi Aprili 19 yakihusisha timu 8 ambazo zinawania ubingwa
- Yanga SC vs Simba SC ni mchezo unaofuatia Kariakoo Dabi, Aprili 29, 2026
Matokeo ya Muungano Cup 2026 Zanzibar yamekuwa na maajabu mengi. Singinda Black Stars walifungashiwa virago mapema kwenye michuano hii. Yanga SC vs Simba SC ni mchezo unaofuatia hatua ya fainali, Aprili 29, 2026 Uwanja wa New Amaan Complex.
SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC uso kwa uso Fainali Muungano Cup 2026 | h2h, Ratiba, Matokeo, Takwimu
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Matokeo ya Muungano Cup 2026 Zanzibar nani kutwaa ubingwa?

Matokeo ya Muungano Cup 2026 Zanzibar hatua ya robo fainali na nusu fainali yameshajulikana. Mnyama alilipa kisasi dhidi ya Mlandege FC baada ya kupata ushindi hatua ya nusu fainali. Walipokutana mara ya mwisho katika Kombe la Mapinduzi, ubao ulisoma Mlandege FC 1-0 Simba SC.
Mlandege FC 0-3 Simba SC matokeo ya mchezo uliopita. Fainali ni Kariakoo Dabi. Mabingwa watetezi Yanga SC watakubali kuachia taji hilo mbele ya mtani?
SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo

Matokeo Muungano Cup 2026
| Timu | Tarehe | Mechi | Hatua | Matokeo |
| Yanga SC | Aprili 21, 2026 | Yanga SC vs Muembe Makumbi | Robo fainali | Yanga SC 4-0 Muembe Makumbi |
| Aprili 25, 2026 | Yanga SC vs Azam FC | Nusu fainali | Yanga SC 2-1 Azam FC | |
| Azam FC | Aprili 22, 2026 | KVZ vs Azam FC | Robo fainali | KVZ 0-2 Azam FC |
| Aprili 25, 2026 | Yanga SC vs Azam FC | Nusu fainali | Yanga SC 2-1 Azam FC | |
| Simba SC | Aprili 23, 2026 | Simba SC vs Mafunzo SC | Robo fainali | Simba SC 1-0 Mafunzo SC |
| Aprili 26, 2026 | Mlandege FC vs Simba SC | Nusu fainali | Mlandege FC 0-3 Simba SC | |
| Mlandege FC | Aprili 23, 2026 | Mlandege FC vs Singida Black Stars | Robo fainali | Mlandege FC 2-1 Singida Black Stars |
| Aprili 26, 2026 | Mlandege FC vs Simba SC | Nusu fainali | Mlandege FC 0-3 Simba SC |
Takwimu za magoli

| Timu | Mechi zilizochezwa | Magoli yaliyofungwa | Magoli yaliyofungwa dhidi yao |
| Yanga SC | 2 | 6 | 1 |
| Azam FC | 2 | 3 | 2 |
| Simba SC | 2 | 4 | 0 |
| Mlandege FC | 2 | 2 | 4 |
Orodha ya wafungaji vinara Muungano Cup
| Mchezaji | Timu | Idadi ya Magoli |
| Prince Dube | Yanga SC | 3 |
| Shekhan Khamis | Yanga SC | 2 |
| Ngita Jean | Azam FC | 2 |
| Seleman Mwalimu | Simba SC | 2 |
SOMA HII: Yanga SC (2) vs Azam FC (1) Muungano Cup | Highlights, goal score | Kariakoo Dabi kupigwa fainali?
Orodha ya Man of The Match

| Hatua | Mechi/Timu husika | Mchezaji aliyechaguliwa |
| Robo fainali | Yanga SC vs Muembe Makumbi | Shekhan Khamis (Yanga SC) |
| Nusu fainali | Yanga SC vs Azam FC | Duke Abuya (Yanga SC) |
| Robo fainali | KVZ vs Azam FC | Ngita Jean (Azam FC) |
| Robo fainali | Simba SC vs Mafunzo SC | Semfuko Daud (Simba SC) |
| Nusu fainali | Mlandege FC vs Simba SC | Neo Maema (Simba SC) |
| Robo fainali | Mlandege FC vs Singida Black Stars | Mbappe (Mlandege FC) |
Hitimisho
Matokeo ya Muungano Cup 2026 Zanzibar yanawakutanisha vigogo fainali Yanga SC vs Simba SC. Mabingwa watetezi imara kwenye ushambuliaji wakifunga magoli 6. Mnyama ithabiti eneo la ukuta akiwa hajaruhusu goli. Nani ataibuka bingwa?Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa.

